Maisha chini ya chama kimoja cha siasa yapoje?

Wakuu habari za muda huu!

Tukiwa tunapokea matokeo kutoka sehemu mbalimbali ya Tanzania, ikionyesha CCM inashinda kila mahali kwa kura nyingi sana.

Mimi ni kijana nilizaliwa (1995) nilikuta mfumo wa vyama vingi vya siasa, katika somo ya Civics nimesoma kitu kimoja kinaitwa check and balance. Natafakari hapa maisha ya chama kimoja yatakuwaje.

Sina hakika kama kutakuwa na mbunge wa CCM anaweza kuikosoa serikali yake kwa utawala huu.

Ubeze usibeze upinzani una umuhimu wake katika kujenga taifa hasa katika kuibua maovu yanayofanywa na serilikali.

Naombeni mloishi miaka ya nyuma kidogo maisha ya chama kimoja yapoje nijiandae kuyapokea.
If China can do it hata Tanzania can. Tofauti ni kwamba zamani hatukuwa na marais makini, huyu tuliye naye hivi sasa hana mchezo....yeye anataka kutuletea maendeleo Tanzania na si vinginevyo.
 
If China can do it hata Tanzania can. Tofauti ni kwamba zamani hatukuwa na marais makini, huyu tuliye naye hivi sasa hana mchezo....yeye anataka kutuletea maendeleo Tanzania na si vinginevyo.
Jamaa_Mbishi, pengine mimi ni mbumbumbu! Nimekuwa nikisiia kauli kama hii ya kwako kutoka kwa waBongolanders wengine kuwa huyu ni rais makini na anataka kutuletea maendeleo kuliko watangulizi wake. Mimi sijaona kitu cho chote tofauti - anatimiza wajibu alioomba kutimiza na kufanya kwa kisiasi fulani kama watangulizi: km walijenga barabara ambazo yeye kama waziri wa ujenzi alisimamia lakini hawakuwaletea wananchi maji safi na salama wala madarasa, madawati, mashimo ya vyoo ya kutosha katika shule za watoto wetu. nk, nk , kama ambavyo yeye anakazia maflaiova na madege ya atcl (shirika hasara) lakini wananchi wanagombania maji ya madimbwi na mifugo yao (sijui kama umewahi kutembelea Dodoma siku za karibuni?). Nisaidie, mimi mbumbumbu.
 
Maisha yataendelea...

Ila yatakua ya resi sana, kila mtu kujipendeza kwa superior ili aonekane yeye ndiyo bora...



Cc: mahondaw
 
Sio kushindwa....mmeiba mchana peupe and everybody knows...na wewe binafsi know!

Tangu kuanzishwa nchi hii hakujawahi tokea bunge likawa na 100% CCM,never!

Hiyo si demokrasia,huo ni uonevu,and you will pay dearly!

And then upo hapa kutetea Single Party state?

Yaani na kusoma kote sekondari na kufanya swali la Multiparty is Better than Single Party State na ukapata 100% ila leo kwa unafiki wa mamba umetoa mimacho unatetea single party state sababu ya China tu?

Duniani kuna nchi zaidi ya 300,kati ya zote hizo zilifeli halafu unachukua China kama mfano uliofaulu as if una probability ya 1 out of 300 ambayo ni 0.3% success rate ya wewe kufaulu?

Yaani una bet on 0.3% probability ya wewe kufaulu unaacha 99.7% ya ufaulu ya record ya democracy?yaani wewe ni maiti mbuzi wa nyama kabisa!

Tuko hapa tunaongelea kuiga upumbavu wa China wa possibility ya kufaulu ya 0.3%?Like really?

Ni maajabu sana,unatetea serikali inayoleta hizo ndege na flyover kua inapenda wananchi,then serikali hiyo hiyo inapogeuka inaua watu hao hao inayosema inawapenda wewe badala ya kua upande wa hao wananchi wanaouwawa,upo upande wa serikali hiyo inayoua!

Yaani wewe una claim unaipenda seriklia sababu inapenda wananchi kwa kuleta mandege nakadhalika,inapoua watu,wewe haupo upande wa hao wananchi wanaouwawa,upo upande wa kuitetea hiyo serikali!

Wote hampo upande wa wananchi,mpo upande wa serikali pekee yake!
Dogo, ebu jiridhishe kisha jipige vidole kwa raha zako mwenyewe hatutakuingilia.
 
Back
Top Bottom