Maisha Bora kwa Kila Mtanzania: Tanzania yashindwa kupunguza vifo vya watoto Masikini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maisha Bora kwa Kila Mtanzania: Tanzania yashindwa kupunguza vifo vya watoto Masikini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rev. Kishoka, Sep 11, 2010.

 1. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #1
  Sep 11, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180
  Leo hii nimesoma habari inayosema kuwa Tanzania imeshindwa kupunguza vifo vya watoto walio chini ya miaka mitano ambao wanatoka kwenye familia masikini na fukara.

  Nimejiuliza, tumeweka juhudi kubwa kama Taifa kujenga mfumo wa maisha ya anasa na hata katika kampeni hizi za uchaguzi, tunaahidiwa vitamanisha macho, viwanja vya ndege, meli, simu, majumba na ahadi zingine lukuki, lakin sijasikia ahadi hasa kutoka Chama tawala au kuona utekelezaji kwa ufanisi kupunguza umasikin wa lile kundi la watu ambao ni mafukara.

  Sijasikia leo CCM katika kujisifu na utawala wao bora uliowaletea neema Watanzania kuwa wameweka juhudi za kulinda uhai wa Mtanzania ambaye hana uwezo wa kujitegemea na ni fukara. Leo Mtanzania huyu, atapewa kadi ya chama, kofia na fulana akipigie chama kura kwa kuwa kimeliongoza Tanzania kwa miaka 50 na Rais wetu kamleta Rais wa Marekani lakin chama hikihiki, hakiwezi mhakikishia Mtanzania huyu uhakika wa uhai wake dhidi ya magonjwa na lishe kwake na kwa watoto wake!

  Natumaini habari hii vyama vya upinzani vitaziona na kuzifanyia kazi.

   
 2. KIWAVI

  KIWAVI JF-Expert Member

  #2
  Sep 11, 2010
  Joined: Jan 12, 2010
  Messages: 1,747
  Likes Received: 376
  Trophy Points: 180
  we are going to have our own dubai pale kigoma na viwanja vya ndege lukuki pamoja na kwamba tuna ndege moja

  hayo ya akina mama ntakuja na ahadi mpya baada ya uchaguzi
   
 3. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #3
  Sep 12, 2010
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Kuna neno moja muhimu ambalo Rev umelisahau katika bandiko lako hili, "vinavyoepukika". Tumeshindwa kupunguza vifo vinavyoepukika vya watoto walio chini ya miaka mitano ambao wanatoka kwenye familia masikini na fukara. Wanaweza kukuambia kuwa kila kifo ni mapenzi ya mungu hata pale ambapo watoto wanakufa au kupata vilema vya kudumu kutokana na kukosa chanjo muhimu.
   
 4. k

  kisoti Member

  #4
  Sep 12, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 81
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  One of the very potential and valuable resources one could ever dare to lose is children.

  God bless Tanzania, God bless Africa. Amen!

   
 5. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #5
  Sep 12, 2010
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mimi ningesema natumai wananchi wataiona na kufanya chaguo lililo sahihi kwenye uchaguzi wa mwaka huu. Kwasababu hilo sio geni kwa vyama vya upinzani linapigiwa kelele kila uchao.
   
 6. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #6
  Sep 12, 2010
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  yep hilo lingekuwa jema zaidi hata mimi naunga mkono hoja
   
 7. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #7
  Sep 12, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Tatizo wananchi ambao ndio tungetegemea walione hili na kufanya uchaguzi sahihi ndio wanaorubuniwa na kofia na t-shirt. Zaidi ni wapinzani kuendelea kulipigia kelele suala hili mpaka hapo watu watakapoelewa kuwa maisha bora si kumiliki simu, magari n.k!
   
 8. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #8
  Sep 12, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Labda Bajaj zilizoahidiwa zitapunguza tatizo hili jamani - zitatumika pia kuwawahisha watoto hospitali.
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Sep 12, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,650
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Watu walioamini kuletwa hayo maisha bora wananishangaza sana!!!!
   
 10. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #10
  Sep 12, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Hivi una uhakika na hicho chanzo cha habari?????Go to WHO and see how we are rated!!!Doh!!JF kuna waokota mambo hapa.Tunabomoa.
  (i) Vifo vya watoto chini ya miaka 5 vimepungua kutoka 158 kwa kila 1000​
  mwaka 2005 hadi 75 kwa kila 1000 mwaka 2010.

  http://www.cms.ccmtz.org/doc/ilani.pdf
   
 11. Rev. Kishoka

  Rev. Kishoka JF-Expert Member

  #11
  Sep 12, 2010
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 4,470
  Likes Received: 277
  Trophy Points: 180

  Ni heri wala usingeleta hilo la Ilani ya CCM maana kila kilichoandikwa humo kina urembo wa uongo. Kama jinsi usivyoamini vyanzo vingine, ndivyo nasi tusivyoamini vyanzo vyako vya habari, Ilani ya CCM!
   
 12. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #12
  Sep 12, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Mimi nafikilia alipaswa apigwe manati wakati akiyasema hayo....unatuambia uwanja wa ndege wakati usafiri wa walala hoi ni treni, badala uboreshe ndiyo kwanza shirika la reli limekuwa la majaribio...asilimia ngapi ya watu kigoma wana uwezo wa kupanda hiyo ndege kama si kuwa tukana watu wa kigoma, je huo uwanja ndege yake kifisadi itaweza kutua au inaweza kutua USA na UK....CCM acheni kutufanya watanzania wote wajinga
   
 13. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #13
  Sep 12, 2010
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  hapa JF huwezi kuwandaya watu, kama mjini hali mbaya kiasi hiki vipi vijijini..
   
 14. TandaleOne

  TandaleOne JF-Expert Member

  #14
  Sep 12, 2010
  Joined: Sep 4, 2010
  Messages: 1,618
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  Toa takwimu.Wangapi kati ya wangapi wameathirika na hilo??????Amka:becky:
   
 15. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #15
  Sep 12, 2010
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Maisha bora zaidi tunasubiri
   
 16. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #16
  Sep 13, 2010
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Mkuu ni kweli idadi ya vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano imepungua kama takwimu hizo zinavyoonyesha ila hili bandiko la hapa linazungumzia vifo hivi likihusisha wazazi wenye vipato vya chini (lowest income quintile). Bandiko hili halipingi au kukinza takwimu za kushuka kwa idadi ya vifo bali linaashiria ya kwamba idadi kubwa ya kushuka kwa vifo hivi imetokea kwa wazazi ambao hali zao za kifedha si duni
   
 17. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #17
  Sep 13, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Kila mtoto wa primary kutumia Computer yake mwenyewe iliyounganiswa na mtandao BY JK :becky: - sijui mgombea huyu anajua kwamba hawa hawa watoto anaotaka watumie computer ndiyo wanaendelea kufa kwa magonjwa ambayo yanaweza kutibika?
   
 18. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #18
  Sep 13, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Hivi ufukara umeletwa na nini? kama si uvivu wa watanzania vijijini na kuzaa sana, kula sana na kuomba omba sana, kulewa sana, kuoa wake wengi na kuoza mabinti kwa umri mdogo kwa vibabu. hakika yule afanyaye kazi kwa bidii Mungu hatamwacha aangamie. jaribu kufany kazi uone kama utabaki maskini. ggoluck to chagas.
   
 19. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #19
  Sep 13, 2010
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Mkisubiri kuletewa hayo maisha bora mtayaona, yatakuja tu, mbona hat biblia imesema msisumbukie ya kesho?
   
 20. M

  Mkandara Verified User

  #20
  Sep 13, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Remmy,
  Mkuu wangu kukinga maradhi na kuepuka vifo hayana kufanya kazi kwa bidii. Nakuiomba usitake kutumia imani yako ya dini kuhalalisha mabovu ya utendaji wa serikali. Hujafa hujaumbika mkuu wangu....wabantu tunasema...tema mate..
   
Loading...