Maisha bora kwa kila Mtanzania: A reflection from Maternity ward | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maisha bora kwa kila Mtanzania: A reflection from Maternity ward

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mapinduzi, Mar 11, 2009.

 1. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Maternity ward: Hospitali ya Wilaya ya Temeke, Jijini Dar es Salaam

  Wataalamu wa afya na usanifu majengo watuambie kama hicho chumba kinauwezo wa kuhimili watu wote hao i.e ventilation?

  Wakina mama waliolala vitandani inasadikika ni wale waliojifungua tayari na waliolala chini ni wajawazito wenye matatizo na wanaosubiri kujifungua?

  Je ni afya vichanga kuwekwa kwenye chumba crowded namna hiyo? Vipi kaa mmoja wa waliolazwa hapo ana ugonjwa wa kuambukiza?

  Kama hali ni hii jijini Dar es Salaam, vipi huko vijijini?

  Mabilioni ya EPA kwa nini yasitumike kuboresha huduma mahospitalini?
  Picha kutoka hapa


  View attachment 3822

  View attachment 3823
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Mar 11, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Three words that sum up everything are............
   
 3. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #3
  Mar 11, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Hayo ndo maisha bora kwa kila mtanzania. Unajua huku vijijini tuna hali nzuri kidogo kuliko mijini. Imagine watu wote hao ni wazazi waliojifungua na wanaosubiri kujifungu.

  Ukiangalia hiii hali unasikitika. Hivi kweli jamani hakuna mfadhili anaweza kujitolea kutujengea walau ward ya wanawake kubwaaaaaaaaaaa wapunguze ujenzi wa mahoteli makubwa.

  Kuna mtu kafungua Hospitali ya wamama masaki karibia na Hotel ya Coral beach hivi kweli kati ya wanawake waliolazwa hapo kwenye picha kuna mtu anaweza kanyaga kule. Kule mpaka uwe na usafiri binafsi ukichukua tax si chini ya elfu 20. Tunakufa tunaona something which is not good.
   
 4. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #4
  Mar 11, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Halafu tunasema uchumi umekua, umekuwa wapi wakati wakinamama kitanda kimoja hospitalini kinalala watu wanne (akina mama wawili na vichanga vyao).

  Imefika wakati sasa serikali itie kipaumbele kwenye huduma za afya. Wanunue vitanda vya watoto na wajenge nursery rooms ili watoto wachanga watenganishwe na crowd ya watu wazima.
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Mar 11, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  This further proves and reinforces my point....
   
 6. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #6
  Mar 11, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Na hapo Dar Mahamiaji sasa wamezidi....
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Mar 11, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  "Tunasema" kina nani? maana mimi sijawahi kusema hivyo hata siku moja
   
 8. Nkamangi

  Nkamangi JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 642
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mfadhili wa kazi gani! Haya mawazo tegemezi ndio yanatufanya hatupigi hatua yoyote. We need to reset our priorities tu. Aibu aibu! halafu serikali inanunua mafwd
   
 9. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #9
  Mar 11, 2009
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,918
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Weeee mbona balaa hapo. Halafu utasikia story nyingi ooh tumefanya hiki na kile, ooh bla bla .....I hate i hate my leaders!
   
 10. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #10
  Mar 11, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Uchaguzi wa serikali za mitaa si mwaka huu..? Basi madiwani kazi wanayo!
   
 11. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #11
  Mar 11, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Maendeleo ya Sultani CCM ,ndio hayo ,ila wasisahau kuipeleka kura yao kwa Sultani CCM ,kwani hayo ndio malipo yake ,halafu niwaangaliwa naona ni wale wale wanaofanya kaazi kwenye vijiofisi vya CCM na wengi wao hao wana maneno makali sana kwa kuilinda CCM ,hawasikii wala hawaoni eti utawasikia wakisema CCM ndio baba huku ananyanyua nguo ,yaani huwa ndo anaonyesha na kuringa kanisa.

  Haya ndio mafanikio ya wafuasi wa Sultani CCM wasiotaka kuondoka madarakani ,wafuasi ambao hawajali maisha ya mtu yeyote zaidi ya maslahi binafsi,wafuasi hawa ambao ni wachache hufaidika na rasilimali za nchi kwa wao na familia zao kutibiwa nje ya nchi au kutumia fdha nyingi kupata matibabu katika hospitali za bei mbaya ,mahospitali ambayo mwananchi wa kawaida kama tunaowaona hapo ,wanabakia na matamanio na ndoto kuwa labda na wao ipo siku watafaidika na matibabu ya kisasa na kupata kutibiwa kwenye hospitali zilizo free na msongamano.

  Hii ni aibu kwa Taifa ni aibu kwa waTanzania ambayo ni nchi iliyojaa kila aina ya mali na sio kwamba mali hizo hazijagunduliwa au kuchimbwa bali ni hazina ambayo kila saa na sekunde inachimbwa na kutoweka nje ya nchi ,wachache wakifaidika.

  Haya si ya leo au jana ni matatizo ya zamani ambayo yapo kila kona ya Nchi hii ya Tanzania ,nani wa kulaumiwa kama si Sultani CCM na utawala wake ,ambao wanatimiza miaka 50 kuwepo madarakani ,Nchi waliichukua kutoka kwa mkoloni ikiwa na mandhari safi na huduma za kisasa kuliko sasa. Nchi ilikuwa safi magari ya kuzolea takataka kila kona yakipita asubuhi na jioni leo yapo wapi ? Hospitali ukienda itakubidi utafute mkoba wa kubebea dawa leo wapi ? karatasi ya kuandikia cheti hakuna .

  Utawala si kukaa kwenye majukwaa na kutoa burudani ya maneno mazuri na kuwapa wananchi ahadi ,Utawala ni utekelezaji kwa vitendo na maendeleo kuonekana ,mabilioni ya fedha za ndani na za kigeni zimeibiwa ,sasa unakatika mwaka wa pili hakuna hata aliethibitishwa kama ameiba zaidi ya kuzungulusha mafaili ,kama haliko mahakamani utaambiwa liko utaambiwa lipo polisi na zaidi uchunguzi haujakamilika faili limerudishwa kusikojulikana.

  Haya ni mambo ya ubabe ambayo yanafanywa na CCM ,maana si katiba wala mahakama zinazoweza kuwafanya kitu ,wote katika vyombo hivyo ni wao kwa wao ,haki ya mwananchi itapatikana wapi ?
   
 12. Recta

  Recta JF-Expert Member

  #12
  Mar 11, 2009
  Joined: Dec 8, 2006
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Nchi hii ina maajabu kweli. Yaani katika mkutano mkubwa na wawekezaji wanaonyesha mambo ya utalii, mawasiliano, kilimo, viwanda halafu wala hawaonyeshi wapi waliposhindwa na penye tatizo kubwa kama kwenye sekta ya afya (hasa afya ya mama na mtoto).

  Inatisha sana. Sijui PRIORITIES za nchi hii ni nini hasa. Maana kwa mawazo yangu, serikali ingejitahidi walau kuhakikisha akina mama na watoto wanakuwa salama wawapo mikononi mwao (Hospital za serikali) kabla hata hawajawa kwenye mikono ya wengine. Kwa utaratibu huu, tunawezaje kusema serikali zetu zinajali afya na usalama wa mama na mtoto?

  Wanachojua ni kupata pesa za wahisani tu, ili wakanunulie magari ya fahari, wasafiri nje zaidi, waandae warsha, kongamano na semina ili wapate posho tu. Wakati huo huo, nguvu kazi mpya inayozaliwa kila siku ikipata maswahibu yanayo hatarisha maisha yao. Nguvu kazi ya nchi ikiwa inazaliwa kwenye hali ngumu na ya kutisha namna hii. Hii inatia mashaka sana nia ya serikali kuleta maisha bora kwa watu wake. Hata uchumi ukikua kwa kiasi gani, kama akina mama wanajifungua kwa mateso makubwa namna hii, haina maana kabisa.

  Watu wako busy kutaka kuhalalisha miradi mikubwa ya umeme, vitambulisho, na mengineyo, wakati watumiaji wanazaliwa katika hali za hatari kama hizo. Yaani hawaoni umuhimu wa kulinda afya za watu na badala yake wanaona umuhimu wa mambo ambayo wala hayana maana kama yalivyo ya usalama na afya za watu wake. Nchi hii itafikaje kwenye malengo yake?

  Ndio maana hatuendelei. Laana zetu zinatokana na kutelekeza watoto wetu. Ona sasa maisha ya akina mama hao wanaohitaji msaada (seriously) wa serikali yao.

  Wakati umefika kwa serikali kuweka mbele mambo muhimu kwa jamii na kuacha kupiga siasa zisizozaa matunda.
   
 13. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #13
  Mar 11, 2009
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hivi kikwete ameshaona picha kama hii,

  hili baraa hivi kama mmoja wapo anaingia na kipindupindu kisichoisha dar kuna uhai wa watoto kweli hapo, mafanikio gani CCM wanajivunia kama Temeka hali ndio hiyo

  Nafikiri picha za aina hii zinabeba ujumbe mwingi kuliko maneno ambayo watu wangekuwa wameuliza source, picha hakuna haja ya kuuliza source bali unaona kila kitu mwenyewe.
   
 14. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #14
  Mar 11, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Kibunango wakati mwingine nashindwa kukuelewa na kama ni mvinyo wa CCM basi uko chakari. Tunayo serikali iliyowaahidi wananchi maisha bora, serikali inayotamba kuwa uchumi wetu unapaa, serikali inayoundwa na chama kinachojivunia sera zake na ambacho kwa mbwembwe kinadai kitabaki madarakani hata kwa miaka mia ijayo !! Hebu fikiria Tanzania itakuwa wapi kama mwenendo wenyewe ni huu.

  Kibunango, unapoangalia picha kama hizi huwezi kujiuliza kuwa kama baada ya miaka karibu hamsini, mambo ndiyo haya - kuna tumaini gani kwa watanzania chini ya hiki chama ? Do we really really need more of the same and expect different results ? Tunajua kelele zetu wengine haziwanyimi usingizi lakini unapoangalia hali za hawa kina mama, hata huruma hupati - ni ulevi gani huo !!

  Kibunango najua wewe ni mwana CCM na naheshimu msimamo wako lakini hata nafsi haikusuti na huku kupiga kwetu kambi kwenye bonde la kashfa na nchi kukosa mwelekeo ? Hakuna hata siku moja unaamka unatamani na wewe ungejitoa kwenye hilo tope na uvundo ukavute hewa safi ? Umekazania kudai hakuna chama mbadala, je nani wajenge hicho chama hali wewe umekwama na hutaki kujinusuru kuwaunga mkono ?
   
 15. M

  Mapinduzi JF-Expert Member

  #15
  Mar 11, 2009
  Joined: Aug 23, 2008
  Messages: 2,427
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Daktari akiwa anapita round, inabidi wagonjwa wasimame ili kumpa nafasi apite, au inabidi awaruke ili akawa-attend wale walio kule mwisho?

  Vipi mgonjwa aliyemwisho wa chumba karibu na sink kule, akitaka kujifungua ghafla, au ikatokea emergency yeyote kama vile moto, au mtu akatoa false alarm 'jamani moto' hao kina mama si watakufa kwa kukanyagana!

  Nyuso zao zinaonyesha kukata tamaa, kukosa tumaini. Hakuna mwenye uhakika kama atarudi nyumbani na mtoto wote wakiwa hai, au mmoja wao atapoteza maisha! So sad.
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  Mar 11, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  I don't exactly get what the fuss is all about here...things like this have always been there....but some people in here seem to be shell shocked...why? It ain't nothing new....
   
 17. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #17
  Mar 11, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Jamani hicho ni chumba cha mapumziko tu baada ya kujifungua siyo wodi wodi ya kuugulia. Hao kina mama wakishapumzika baadaye ndiyo wanatoka na watoto wao kuendelea na shughuli zao. Kwa kawaida wana muda wa kutosha kupiga soga, na kuzungumza na kufahamiana. Wengine wanaweza kutumia nafasi hiyo kuingia madili ya kibiashara n.k

  Kuna kiasi cha bilioni 200 za mradi wa vitambulisho vya smart card! Sasa, hawa kina mama wakishapatiwa vitambulisho vya kisasa kabisa vitawasaidia kutopotea kwenye wodi au kupoteza watoto wao. - Waziri wa Afya na Vitambulisho!
   
 18. m

  mkombosi Senior Member

  #18
  Mar 11, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 101
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Rais kilaza hayo ndio matunda kwa vilaza waliomchagua
   
 19. M

  MzalendoHalisi JF-Expert Member

  #19
  Mar 11, 2009
  Joined: Jun 24, 2007
  Messages: 3,869
  Likes Received: 116
  Trophy Points: 160
  We lack Innovative and practical ideas in advance planning in the health sector!
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  Mar 11, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,735
  Trophy Points: 280
  Inasikitisha kwa kweli kuitazama hiyo picha. Tanzania si maskini kiasi hicho cha kushindwa kununua vitanda na kuhakikisha hao akina mama wajawazito na watoto wao kwa wale waliojifungua wanapata mahali pazuri pa kujipumzisha kabla na baada ya kujifungua.

  Rasilimali zetu zinachukuliwa bila manufaa yoyote kwa Watanzania. Dhahabu sasa hivi katika soko la dunia imeongezeka sana lakini bado tunapata 3% ya mapato yanayotokana na dhahabu yetu. Pamoja na Kikwete kuahidi kwamba ataingalia upya mikataba ya uchimbaji wa madini hadi hii leo mwaka wa nne tangu aingie madarakani hajafanya chochote.

  Juzi juzi serikali ilinunua mashangingi 800 na kutetea ununuzi wa mashangingi hayo eti ni muhimu kwa vile barabara nyingine za mikoani hazipitiki ila kwa mashangingi. Sijui ni safari ngapi zinazodanywa mikoani kila mwaka za kuhalalisha ununuzi wa mashangingi hayo ambalo moja lina gharama kati ya shilingi milioni 100 mpaka 150. Kwa maoni yangu bei ya shangingi moja ingetosha kabisa kuzipatia hospitali za Temeke, Mwananyamala na Amana vitanda na kuwaondolea adha kubwa wanayopata wagonjwa na wajawazito ya kulala chini au kushara vitanda. Hii ni aibu ya hali juu. Halafu viongozi wa CCM wanaoita huku na huko kujinadi kwamba wanaiongoza nchi vizuri kitu ambacho hakina ukweli wowote. :(
   
Loading...