MAISHA BORA au MAISHA DUNI kwa kila Mtanzania ?

KakaNanii

JF-Expert Member
Sep 28, 2008
325
52
Huyu Jakaya wakati anaomba ridhaa kwa Watanzania ili aingie ikulu aliahidi ataleta MAISHA BORA kwa kila Mtanzania. Lakini ukiangalia kinachoendelea sasa ni MAISHA DUNI kwa kila Mtanzania.

Nasema hivyo kwa sababu tangu aingie Ikulu vitu vimekuwa vikipanda bei kila kukicha. Kwa mfano mchele sasa unakimbilia kilo moja shilingi elfu mbili na miatano(2,500). Hiyo sukari ndio usiseme, kila siku inapanda bei.

Kama hiyo haitoshi,hapa juzi tu tayari bei ya umeme imepanda kwa 40 %. Kule Kigamboni napo bei ya Kivuko imepanda kwa 100%. Nauliza hivi, haya ni MAISHA BORA au MAISHA DUNI kwa kila Mtanzania ?
 
Wakati mwingine kumlaumu JK ni kumuonea, tulijua jambo hili haliwezekani na bado tukamchagua kwa hiyo mimi wala huwa simlaumu tena, kwa kuwa ni sisi tunaomlaumu ambao pia ndio tulio mchagua, ama ndio ambao hatupigi kura kwa kisingizio hata nikipiga atashinda jambo ambalo si kweli.
 
Maısha bora kwa wachache na Maısha dunı kwa wengı. Hauwezı kusema Raıs ana maısha dunı, labda kama mımı sıelewı maana ya maısha dunı.
 
Ukistaajabu ya malaria sugu utaona ...........

"Wajibu mkubwa wa Serikali kwa sasa ni kuhakikisha fedha za umma zinawanenepesha wananchi badala ya kunenepesha maofisa wachache wa umma."
~Kikwete
 
Back
Top Bottom