Maisha bila familia ni kazi bure, ni sawa na Utumwa

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,269
40,056
Maisha bila familia ni kazi bure, ni sawa na utumwa.

Ni vizuri familia kuipa nafasi katika maisha yako kama sehemu ya mafanikio. Wapo watakaosema familia haina umuhimu, wakiamini kama kuna mafanikio ya kiuchumi familia haina maana. Kwa mtazamo wangu mi naona familia kwanza, ndio mengine yanafuata. Wakuu, njooni tujadili.

quotee.jpg
 
Mijadala kama ya O'level hii eti mnajadili "Education is better than money". Kwani ukiwa na vyote kuna ubaya gani? Na familia tunaongelea hizi extended za Kiafrika au na za kizungu (mke na mme tu) nazo zinakwolifai? Kuna faida gani ya kuwa na familia hasa katika mazingira ya kisasa? Mjadala tenge huu !!!
 
Kwa tafsiri ya kawaida, familia ni ndoa; mume na mke kisha watoto hufuatia hapo na inaweza kuongezeka mpaka kufikia kuwa vizazi vitokanavyo na ukoo mmoja.

Lakini kuna wale ambao msamiati huu ni tofauti kidogo kwao. Kuna ambao kwao familia ni watu wowote wale ambao wana mahusiano nao ya karibu na si lazima wawe ndugu wa damu.

Kuna watu ambao si ndugu wa damu kabisa na wanaishi na kushirikiana katika masuala mbalimbali kama ndugu wa familia moja wakati huohuo kuna ndugu ambao wanaishi kama paka na panya ama jambazi na polisi kutokana na sababu mbalimbali.

Pia kuna watu ambao wametengwa na familia zao kwa sababu siziso za msingi kabisa na wanaishi na marafiki tu kama ndio ndugu zao. Wahenga miaka fulani waliwahi kuja na msemo wao kuhusu undugu waki-suggest namna unavyotakiwa uwe.

Kwahiyo, inategemea hiyo familia ni katika hali na mtazamo upi.
 
Kila mtu ana mawazo yake na tunatofautiana sana kuanzia makuzi na jamii tulizolelewa na kukua nazo..lakini nafikir huyu ndg anajaribu kuonesha priority 1 kwake ni familia..iwe nuclear au extended..mfano mrahisi ni pe mtu anafamilia Dar anapata kazi arusha ambayo kwake inamalsahi makubwa tu kuliko aliyonayo Dar lakini Dar ndiko familia yake ilipo na akiwaza kwenda nayo anaona itakuwa usumbufu..kwa mtu type hii tegemea kazi hiyo atapiga chini na kuendelea na maisha Dar...real mfano kazini kwetu june 30 mtu ameamua kuacha kazi maana alitakiwa kwenda mwanza na tuko hapa Dar...
 
Kwa mtazamo wako unaona ipi bora, kuishi mwenyewe mwenyewe au kuwa na familia?
 
Kila mtu ana mawazo yake na tunatofautiana sana kuanzia makuzi na jamii tulizolelewa na kukua nazo..lakini nafikir huyu ndg anajaribu kuonesha priority 1 kwake ni familia..iwe nuclear au extended..mfano mrahisi ni pe mtu anafamilia Dar anapata kazi arusha ambayo kwake inamalsahi makubwa tu kuliko aliyonayo Dar lakini Dar ndiko familia yake ilipo na akiwaza kwenda nayo anaona itakuwa usumbufu..kwa mtu type hii tegemea kazi hiyo atapiga chini na kuendelea na maisha Dar...real mfano kazini kwetu june 30 mtu ameamua kuacha kazi maana alitakiwa kwenda mwanza na tuko hapa Dar...
Uko sahihi; hapa ndipo wazo la kujiajiri au kuwa na kampuni yako uanzia.
 
Kwa tafsiri ya kawaida, familia ni ndoa; mume na mke kisha watoto hufuatia hapo na inaweza kuongezeka mpaka kufikia kuwa vizazi vitokanavyo na ukoo mmoja.

Lakini kuna wale ambao msamiati huu ni tofauti kidogo kwao. Kuna ambao kwao familia ni watu wowote wale ambao wana mahusiano nao ya karibu na si lazima wawe ndugu wa damu.

Kuna watu ambao si ndugu wa damu kabisa na wanaishi na kushirikiana katika masuala mbalimbali kama ndugu wa familia moja wakati huohuo kuna ndugu ambao wanaishi kama paka na panya ama jambazi na polisi kutokana na sababu mbalimbali.

Pia kuna watu ambao wametengwa na familia zao kwa sababu siziso za msingi kabisa na wanaishi na marafiki tu kama ndio ndugu zao. Wahenga miaka fulani waliwahi kuja na msemo wao kuhusu undugu waki-suggest namna unavyotakiwa uwe.

Kwahiyo, inategemea hiyo familia ni katika hali na mtazamo upi.
Changamoto hizo zipo, ila kwenye mada tujikite kwa: mme + mke + watoto
 
Back
Top Bottom