Uchaguzi 2020 Maisha Baada ya Uchaguzi: CCM won the Battle and lost the War

Wakati siasa imebanwa kwa upinzani CCM ilikuwa ina fanya shughuli zake za kisiasa kama kawaida hata kwa TV na kila anakopita.
 
Baba wa Taifa aliwahi kusema mpumbavu ni sawa na MTU mfupi ambae huwezi kumrefusha na ukilazimisha kumrefusha utamuua.Nchi imeshachanika wajinga wanaweza kuelewaelewa hv ila usitarajie wapumbavu wataelewa mambo haya sio rahisi ksbisa .
 
Bwawa la umeme la Nyerere linakisiwa kugharibu Shilingi Trilioni 9.

Haya makisio yanasemekana ni ya chini na inaweza kuwa mara mbili yake.

Mradi huu unalipwa in $. Utalii ambao ni biggest earner wa $ upo chini for the next two years.

Donors watapunguza misaada na wengine hawatatoa kabisa. Sekta ya Afya na Elimu itapata shida.

Hapa kuna watu wanashangilia. Bado miradi mingine mingi ipo haijafikia hata 50%, mfano SGR.

Bado ATCL inahitaji ruzuku.
😂He know the mess he did thats why whenever he talks about employment he always talking about how building these projects employs people.Nigga spent all of his saving on projects,cant even employ on official sector.
 
Binafsi nilitegemea matokeo ya aina hii,unapo aribu uchaguzi na kuwanyima watu nafasi ya kuchagua viongozi wanaowataka unawapa sababu ya kutafuta njia mbadala ya kupata viongozi , mchakato wa uchaguzi umepoteza maana na viongozi wanaotokana na uhuni wa aina hii hawana kibali (legitimacy) ya wanaowatawala.
 
Nimekuja kujifunza kitu muhimu sana. CCM na ule mkutano mkuu wao wa kuchagua wagombea wa nafasi ya Urais huwa ndio wenye maamuzi ya mwisho.

Yeyote atakayepitishwa pale, watanzania tupende tusipende ndie atakae kuja kuwa Rais, sasa tatizo linakuja huyo wanaempitisha wamewahi kumfanyia vetting ya kutosha kujiridhisha kama ana weledi na hekima ya kutosha kuliongoza taifa letu.

Inavyoonekana na 2015 in particular, JK alikurupuka kumpitisha huyu mtu, hasa baada ya ushindani uliokuwepo baina ya Membe na Lowassa, akaona bora awatose wote ampitishe jiwe, mazingira ya wakati ule yalimlazimisha kufanya vile, matokeo yake akampa madaraka mtu aliejua vizuri hana tofauti na kichaa, mwenyewe akamuita "bulldozer", matokeo yake sasa kila mtu anajutia matendo ya huyo "bulldozer"

CCM kwa sababu wanalindwa na TISS na vyombo vingine vya usalama, ni wajibu wao kumfanyia uchunguzi wa kutosha mtu wanaetarajia kumpa nafasi ya urais, ili wakati ukifika wasije kuwa na wasiwasi na tabia au matendo ya huyo mgombea wao.

Kinyume na hapo watanzania tutaendelea kuumizwa kwasababu ya ulinzi wanaopewa CCM na TISS, lakini pia; maamuzi ya hovyo yanayofanywa na mwenyekiti wa CCM kwenye kumchagua mgombea wao wa urais.

Uchaguzi wa mwaka huu nadiriki kusema bila shaka; TISS ndio wamehusika kuwapa ubunge Tulia - Mbeya Mjini, Gambo- Arusha Mjini, yule mgombea wao wa Hai, na yule wa Moshi Mjini, na pengine pote ambapo upinzani ulikuwa mkubwa. Wananchi hawakuwa na maamuzi yoyote kwenye kuwachagua hao wagombea wa CCM.
 
Hakuna aliyetegemea uchaguzi uwe wa huru na haki. Lakini hakuna aliyetegemea wizi uwe wa wazi na wa kijinga hivi.

Chama Cha Mapinduzi, kama chama kikongwe barani Afrika, kimethihirisha hakipo tayari kuachia madaraka kwa njia ya sanduku la kura. Si Bara wala si Visiwani..
Tuliandika kitambo "umoja na amani haviletwi kwa mabavu" ikiwa hakuna maridhiano tutarajie utengano na chuki kutamalaki huku mitaani.

Wafu watawazika wafu wao.
 
Kama unajua maana ya check and balance huwezi kushangilia haya matokeo...
Upinzani wa dizain hii bora ufutwe tu. Hauna maana yeyote acha watu wakipata akili labda utakuja upinzani wa maana ila huuu wa sasa ni utopolo tu.
 
Kwenye mazingira kama haya halafu unasikia kuna magaidi huko kusini, huo umoja utatoka wapi?

Kuongoza nchi lazima hekima iwepo, japo una madaraka na nguvu kubwa, lakini vyema ukajua namna ya kucheza na psychology za unaowaongoza, ukihisi upande fulani hawana amani, fanya jambo uwafurahishe, lakini sio kukaa kimya na kuendelea na matendo ya hovyo kila siku.

Amani inayohubiriwa kila siku lazima iambatane na matendo, kuimba amani. Amani, huku matendo yako ni ya kinyama unawakera wasikilizaji.
 
😂He know the mess he did thats why whenever he talks about employment he always talking about how building these projects employs people.Nigga spent all of his saving on projects,cant even employ on official sector.

Wakandarasi wa hii miradi wote ni wa nje. Wafanyakazi wazawa wengi ni casual laborers tu.

Unakusanya kodi kwa asilimia kubwa kwa shilingi, miradi unalipa kwa dola kwa kampuni za kigeni.

Hapo nusu ya makusanyo ni kulipa madeni ambayo pia ni dola, euro n.k.

Kwa sababu umeongeza waimba kwaya wa kusifu na kuabudu gharama za kuendesha serikali nazo zitaongezeka.

Tutakuja hapa kutafutana mchawi wetu nani.
 
Wakandarasi wa hii miradi wote ni wa nje. Wafanyakazi wazawa wengi ni casual laborers tu.

Unakusanya kodi kwa asilimia kubwa kwa shilingi, miradi unalipa kwa dola kwa kampuni za kigeni....
Kwasababu miradi pia itakuja kutumika na watu wa nje
 
Back
Top Bottom