Maisha baada ya kuachwa

Meridah Tough

Senior Member
Nov 27, 2017
136
363
Hello?
Baada ya muda mrefu wa masikitiko ya kuachwa na aliyekua mpenzi wangu leo ninaandika nikiwa na furaha na amani.
Kiukweli nilipoachwa niliumia sana. Niliwaza, nikaomba msamaha, nikaomba ushauri huku na kule, nikaomba na kufunga ex wangu arudi. Na kweli, kumuomba misamaha na kuhangaika kumtafuta kila mara kulinifanya niache mlango wa yeye kurudi na kuondoka alipotaka.
Nilimpa uhuru huo. Alirudi mara kwa mara na aliondoka kila alipojisikia. Kwa kua nilimuonyesha kua sina upinzani juu yake.
Aliweza kununa pasipo na sababu ya msingi na kuniblock hata kama sijamkosea.
Mara ya mwisho, nilimwambia sihitaji tena mahusiano yasiyoeleweka. Kama ananipenda tutulie na kuweka malengo. Kama hataki tubaki marafiki tu. Kwa kua alijua sina upinzani nae tena, akaamua kuondoka. Akijua wazi nitamuomba msamaha na ataendelea na tabia ya kuja na kuondoka.
Nilikaa chini kujifikiria wapi nakosea. Kitu gani kinamfanya yeye anidharau nk.
Nikaamua jambo moja. Kufocus kwenye maisha yangu. Kutomtafuta tena katika maisha, kufanya mambo yangu ya msingi kwa ajili ya maisha yangu na kuhangaika na dreams zangu.
Tuna miaka mingi toka tulipokua pamoja. Katika muda wote huo haijawahi kutokea hatujawasiliana nae. Hata akiniblock nimezoea kumtafuta kwa msg au mitandaoni.
Nadhani alijua siwezi fika wiki 1 bila kumuomba msamaha.
Mungu amenisaidia. Amenipa marafiki na ndugu wanaonipenda. Kwa kiasi kikubwa nimeweza kuwa busy na kumsahau taratibu.
Baada ya wiki 2 yeye sasa ameanza kunisumbua kwa msg na calls.
Wadada na wakaka, ni lazima tujue thamani yetu kwanza kabla ya kutaka mtu baki akuthamini. Kosa langu lilikua kumuonyesha kuwa bila yeye siwezi ishi, Sina maisha mengine zaidi ya yeye. Thamani yangu nikaishusha. Maana kama anaweza kumpata yeyote, What makes me unique? Vipi aone thamani yangu wakati mwenyewe siioni?
Wale ambao mnapitia changamoto kama yangu, tafadhali jifunze kupitia mimi. Muda ni wa thamani. Kama hujashtuka mapema unaweza jikuta unakaribishwa kwenye harusi na mtu ambaye unadhani ndio mume wako. Ni bora akuache au akukubali ijulikane moja. Kukaa mguu ndani mguu nje inapoteza muda na kujibebesha shida tu. Nawasilisha.
 
baby calls na message zangu hujibu!!! bado haijatosha umekuja nitangaza mpaka na uku: usifanyie ivo nipe third chance
 
Hongera sana...lakini ukumbuke hakunaga wapenzi wanaokuja kuwa marafiki wa kawaida tu. Halafu hujasema alivyokutafuta umemjibu nini ila ujue kwa jinsi ulivyojiweka jamaa atakuja kupasha kiporo tu. Ukitaka kuachana na mtu kiukweli make sure u burn all the bridges.
 
Basi nijibu piem kabla sijamwambia kwamba unantaka...
Piem yangu anayo babe atakujibu yeye
IMG_20190209_002622_260.jpeg
 
Kama mleta mada angelikuwa ni mwanaume ningeamini kilichoandikwa lakini kwa kuwa ni mwanamke......
 
Similar Discussions

44 Reactions
Reply
Back
Top Bottom