Maisha baada ya kifo : Naomba kujua tofauti za kufa ukiwa mtu mashuhuri na kufa ukiwa wa kawaida sana

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,302
2,000
Kuna watu wanakufa wakiwa matajiri , viongozi wakubwa , maarufu na wanakuwa gumzo kila kila kona ya nchi /dunia. Jamii makundi kwa makundi hupaza sauti za kusikitika, kusononeka kila wakati zikieleza mazuri mengi ambayo mrefu amewahi kufanya au kuwa na mchango fulani mkubwa.

Kuna binadamu wengine wanakufa kifo cha kawaida, hakuna mstuko mkubwa , hawasemwisemwi , hawana reference yoyote wa mambo ambayo wameyafanya kwa ukubwa fulani at national /international levels.

Kwa hisia zako kama binadamu ,tofauti za maisha ya hawa watu baada ya kifo zikoje ?

Nderemo,huzuni na ushuhuda wa walimwengu utamfanya atalazwe mahala pema peponi kweli hata kama alikuwa na maovu yake?

Tujadili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mapipando

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
2,798
2,000
Mungu kamwe hahongwi kwa sifa na vilio vyetu pindi watu mashuhuri wanapofariki.

Mungu anapenda watu wenye kumtii,sasa si ajabu hao mashuhuri wanaojulikana nchi/dunia nzima wakalazwa pasipo pema kutokana na dhambi walizotenda na yule asiye mashuhuri mwenye kujulikana tu kwenye mtaa wake na mcha Mungu akalazwa mahala pema peponi...
 
gigabyte

JF-Expert Member
May 27, 2015
1,693
2,000
Kwani umaarufu unasaidia nini ukishakufa.kifo ni kifo hakina cha tajiri wala maskini,mbele ya kifo sisi wote ni sawa ndo maana wako binadamu waliwai kua maarufu uko nyuma hadi wakaandikwa kwenye vitabu vya dini mbali mbali lakini wakati wao ulipopita hautakua tofauti na tutakavyopita nasisi.wote tutakua na jina moja tu la Marehemu.kuna wale wanaitwa Hayati lakini haibadilishi chochote.Swala la wapi tunaenda ilo ni jambo lakila mtu na imani yake.
 
Jay One

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
14,153
2,000
Mtu mashuhuri akifa hata angekuwa na maovu kiasi gani na mtu wa shetani kiasi gani, akifa tu anageuka kuwa MTAKATIFU, mtu mwema sana na vilio kibaoooo... Ila yoote ni UNAFIKI ndio yanaongoza kusema haya..!!

Mtu wa kawaida au maskini, hata angekuwa mwema kiasi gani, akifa hajulikani na watu watamkimbia na hata kuzikwa ni kazi na wengine watasema kimoyo moyo kheri kaondoka..!!
 
ikigijo

JF-Expert Member
Aug 23, 2017
1,023
2,000
Kuna watu wanakufa wakiwa matajiri , viongozi wakubwa , maarufu na wanakuwa gumzo kila kila kona ya nchi /dunia. Jamii makundi kwa makundi hupaza sauti za kusikitika, kusononeka kila wakati zikieleza mazuri mengi ambayo mrefu amewahi kufanya au kuwa na mchango fulani mkubwa.

Kuna binadamu wengine wanakufa kifo cha kawaida, hakuna mstuko mkubwa , hawasemwisemwi , hawana reference yoyote wa mambo ambayo wameyafanya kwa ukubwa fulani at national /international levels.

Kwa hisia zako kama binadamu ,tofauti za maisha ya hawa watu baada ya kifo zikoje ?

Nderemo,huzuni na ushuhuda wa walimwengu utamfanya atalazwe mahala pema peponi kweli hata kama alikuwa na maovu yake?

Tujadili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu samahani naweza kuwa Nje ya mada ila nimeona nikuambie kuwa Ile mada yako ya "NIULIZE CHOCHOTE KUHUSU CCM"
Napendekeza uwe una update watu majibu...ni Nzuri sana sana Kaka...Nakupongeza pia kwa ile Mada.
 
Humphnicky

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
2,031
2,000
Ufunuo wa Yohana : Mlango 14

13 Nikasikia sauti kutoka mbinguni ikisema, Andika, Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa. Naam, asema Roho, wapate kupumzika baada ya taabu zao; kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.Kuvuna Mavuno ya Nchi

mzamifu

JF-Expert Member
Mar 10, 2010
5,219
2,000
Ukifa unarudi udongoni na huko vile viasili vilivyoko mwilini mwako hutumika tena kukuza viumbe wengine. Mfano kama kuna mwembe utafyonza hivo viasili na kutengeneza matunda ambayo viumbe wengine watakula na kuishi. Maisha yanaendelea. Watu ni wale wanaoishi sasa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewemwenyewe

JF-Expert Member
Nov 23, 2018
282
500

Ukifa, you’re nothing. That’s why wanachimba 6 feet deep ili usije leta kero ya harufu.
Now you’re somebody
 
Madeteeli

Member
Jun 23, 2020
14
45
Ndugu kama kichwa kilivo hapo juu mm naitwa Eliya Madete naomba kuuliza baada ya kufa kuna sehemu tunaenda au tunapotea tu
 
SeliSelina

JF-Expert Member
Jun 27, 2014
230
1,000
BAADA YA KUFA UTAZIKWA KWENYE KABURI, HAPO NDIO MAISHA YAKO YATAKAPOOANZA, MPAKA SIKU YA MWISHO WA DUNIA, WATAKUFA WOTE WALIOBAKI, IKISHA WATAFUFULIWA WOOTE WALIOKUFA TOKA KUANZA KWA DUNIA, HAPO SASA NDIO HESABU ITAKAPOKUWA.
MWENYE KUTENDA MEMA ATAINGIZWA KWENYE PEPO, NA MWENYE KUTENDA MAOVU ATAINGIZWA KWENYE MOTO.
KUNA AMBAO HAWATAKAA MILELE MOTONI, WATATOKA BAADAE NA KWENDA KUISHI PEPONI.
ILA KUNA WENGINE WATAISHI MILELE MOTONI.
ANAINGIA KWENYE PEPO NDIO KESHAINGIA HATOKI TENA.
HIYO KWA UFUPI.
KWA FAIDA
JITAHIDI SANA KUISHI DUNIANI KWA WEMA NA IHSAAN. NA KUFUATA YALE YOTE YALIOAMRISHWA KUFUATA NA KUASHA YOTE YALIOKATAZWA.
 
Entreprenuare

JF-Expert Member
Aug 24, 2019
1,629

Kumbe teyar unajua nn kitatokea?? Basi hata siku yako ya kufa utakuwa unaijua aisee, you are good
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom