MAINTAINING STATUS QUO??!!; Magogoni yamwapisha waziri asiye na wizara maalumu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MAINTAINING STATUS QUO??!!; Magogoni yamwapisha waziri asiye na wizara maalumu!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiganyi, May 22, 2012.

 1. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  Waziri wa nchi katika ofisi ya Rais asiye na Wizara maalum Profesa Mark Mwandosya akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.Na watatu kulia ni Karani wa Baraza la Mawaziri Bwana Gerson Mdemu.


  [​IMG]
  Profesa Mwandosya akipokea miongozo ya kazi baada ya kula kiapo ikulu leo asubuhi.


  [​IMG]
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza na kumtakia mafanikio Profesa Mwandosya muda mfupi baada ya kumuapisha ikulu jijini Dar es Salaam leo.
  [​IMG]
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimsaidia Waziri wa nchi katika ofisi ya Rais asiye na Wizara maalumu Profesa Mark Mwandosya kushuka katika ngazi za ikulu baada ya kumuapisha leo asubuhi.
  [​IMG]
  Waziri Profesa Mark Mwandosya akiwa katika mazungumzo na Rais Dkt.Jakaya Kikwete muda mfupi baada ya kula kiapo ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi(picha na Freddy Maro)
   
 2. Ileje

  Ileje JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 3,872
  Likes Received: 1,658
  Trophy Points: 280
  Tufikirie uwezekano wa kuanzisha mabaraza ya watu wenye hekima, wanataaluma mbalimbali, viongozi wakuu wastaafu watakaokuwa washauri wa serikali katika masuala ya siasa, uongozi, sheria na taaluma mbalimbali.

  Professor kwa namna alivyochoka angefaa sana kuwa katika moja ya mabaraza hayo.
   
 3. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Ileje kama ulikuwa kwenye mawazo yangu
  na hivi utaratibu wa mtu kujiona kuwa jukumu alilopewa may be ni kubwa sana kwake kutokana na afya yake au kutokana na sababu nyinginezo akaukataa uteuzi huo kwa heshima
  Maana Prof angekuwa kwa sasa anakaa anatoa machapisho may be ambayo hayamsumbui anajiamulia kufanya au kutofanya
  Ila kwa kuwa hapa ni waziri asiye na wizara mhhh yote yawezekana tanzania yetu hii
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,335
  Likes Received: 1,797
  Trophy Points: 280
  Nashukuru mzee ameweza kunyanyuka leo. Nakutakia afya njema.
   
 5. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Kwanini asingeanzisha Wizara ya Hospital ya Appolo angalau ingesimamia afya za viongozi wetu na ningependekeza Chami ,Mwakiembe au Mwandosiya aongoze Wizara hiyo
   
 6. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  ''ingekuwa ni vyema kama rais angeniacha nipumzike''--------kauli ya mwandosya
   
 7. Jallen

  Jallen JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 497
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 45
  Hiyo nafasi aliyopewa ni sawa na baraza la ushauri tu. Rais ameona ni vyema amuweke karibu ili aweze kuchota ushauri na hekima kutoka kwa huyo mzee.
   
Loading...