Wahandisi watusaidie: Kwanini Tanzania Matumizi ya Matofali yenye Uwazi Katikati ni Madogo sana?

tutafikatu

JF-Expert Member
Dec 17, 2011
3,233
4,451
Kwa uzoefu wangu mdogo, tofali zenye uwazi katikati (Hollow Cement Block) zinatumika kwa uchache sana. Pamoja na faida zake nyingi, najiuliza ni kwa nini?

images-1.jpeg
images-2.jpeg
 
Faida zake "nyingi" ni zipi?
Hili lilimlenga engineer ambaye anajua faids zake. Sijaja kuleta shule ya faida. Hiyo mwaweza google kiganjani. Nauliza kwanini hazitumiki sana?
Sisi zaidi ya kutumia kwenye ukuta hatuna matumizi mengine.

Hebu tupe kazi zingine tujifunze
Mleta mada mwenyewe hajui faida za hayo matofali...
Tupe hizo faida zake tuzijue huenda tukahamia huko.
 
Mleta mada na atcl ni majamaa ujui faida zake baada ukubali umekalia kubsha et ugoogle mara swal lmewalenga ma engineer WAFATE INBOX SASA. ANY WAY PROFILE PICTURE INAJIELEZA
 
Tumia kujengea nyumba yako utajuakwanini hayatumiki
Hizo zinatumika sana DRC, na ni kupunguza gharama ya saruji, kwani kule ni bei kubwa sana, hata ghorofa wanajengea hizo, ila kwa uimala haiwezi kulingana na hizi zetu.
 
Kwa uzoefu wangu mdogo, tofali zenye uwazi katikati (Hollow Cement Block) zinatumika kwa uchache sana. Pamoja na faida zake nyingi, najiuliza ni kwa nini?

Sababu kwanini hayatumiki sana
1.Hayana uwezo wa kubeba mzigo mkubwa (Non load bearing wall).

2.Malighafi za kuyatengeneza hazipatikani kwa urahisi (hasa chipping /clusher dust).

3.Kuta nyingi za maofisini kutumia Aluminium (uwezo wa kuweka na kuondoa).

4.Kama hazitojazwa ndani yake kwa malighafi maalum (insulator /pumba za mbao n.k) huleta joto ndani ya nyumba /cracks).

5.Haziwezi kutumika tena.

6.Hasara katika usafirishaji hasa pale zinapokuwa hazina viwango.

7.Matumizi yake yanahitaji uangalifu hasa kuyakata /joints hivyo kulazimisha vifaa maalum kuyakata ili vipande vungine vitumike kwenye ujenzi.

8.Ni rahisi kutoboa na kuingia ndani /kiusalama si sawa hasa kama jengo ni la chini.

9.Bei kuwa kubwa pengine kuzidi yaliyo na ujazo ndani.

10.Hupatikanaji wake kuwa mgumu.

11.Wajenzi na wenye Ujenzi kutokuyaamini ingawa ni mazuri kama watajitokeza kufuata Ushauri wa kitaalamu kwa Wataalamu wa Majenzi (Kujenga ki Mazoea).

12.Kupunguza uimara wa ukuta hasa unapojenga jengo lenye kima kirefu (Maghala, Makanisa, Karakana n.k) bila kuweka nguzo na mikanda ya zege /beams hivyo kusababisha jengo kuezuliwa au kupata ya nyufa za kulizunguka jengo.

Faida za haya matofari zipo nyingi kuliko hasara ambazo ni
1.......40.
Ili kupata faida hizo tembelea Wataalamu wa Ujenzi popote ulipo.
 
Tunauza mbao kwa bei ya jumla.Njoo ofisini kwetu TEGETA tukuhudumie kwa gharama nafuu sana:-
2*2 fut12=2500
2*2 fut12(treated) ya dawa=2800
2*2 fut18(treated) ya dawa=5000
2*4 fut12 treated(ya dawa)=5000
2*4 fut12 isiyo ya dawa=4500
1*6 fut12=5000
1*8 fut12=8500
1*8fut12 ya fisher board(treated)=9500
1*10 fut12=13500
1*10fut 18 fisher board( treated)=15500
2*4 fut18(treated)=9500
2*6 fut12=8000
1*4 fut12=2800
2*6 fut 18=19000
Tunapatikana muda wote kwa namba za simu zifuatazo:-
----0759630751
----0687371138
----0654830416

vile vile kuna huduma ya kuchana,kuranda na kusize mbao inapatikana ofisini kwetu
 
Sababu kwanini hayatumiki sana
1.Hayana uwezo wa kubeba mzigo mkubwa (Non load bearing wall)...
Umeongelea vyema saana mkuu. Isipokua namba 4. Void tu ni bad conductor of heat. Formula hiyo hutumika pia kwenye Chupa za chai(thermos ) ule uwazi wa ndani, huzuia joto la ndani kwenye nje au la nje kuingia ndani. Tofauti na Solid blocks ambapo joto la nje huingia ndani moja kwa moja kupitia ukuta.

Matofali yenye uwazi (ukuta wenye uwazi) hutumika zaidi sehemu zenye joto kubwa kama nchi za uarabuni au zenye baridi saana kama Urusi n.k. Ili ku regulate internal temperature. Hii hupelekea kupunguza gharama za nishati
 
Back
Top Bottom