Maingiliano ya kiutamaduni na baina ya watu kati ya China na Afrika yamezaa matunda katika kipindi cha miaka kumi iliyopita

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,000
1,019
VCG111166325353.jpg


Urafiki baina ya mtu na mtu mara nyingi huwa ndio chachu au msingi wa uhusiano kati ya taifa moja na jingine, ambapo urafiki huu unaimarisha maelewano na maingiliano ya pande zote mbili. Ni miaka kumi sasa tangu rais Xi Jinping aingie madarakani, na katika kipindi chote hicho hakika yameshuhudiwa mabadiliko makubwa kwenye nyanya hii ya maingiliano baina ya watu na watu na mawasiliano ya utamaduni kati ya China na Afrika.

Kwa sasa China na nchi za Afrika zimekumbatia zaidi mawasiliano ya kiutamaduni, vyombo vya habari, sayansi na teknolojia, pamoja na washauri bingwa, halikadhalika kurahisisha mazungumzo baina ya vijana na wanawake. Juhudi zote hizi zimekuza uhusiano kati ya watu na watu na kuweka msingi imara kwa ajili ya kupata maendeleo zaidi.

Katika miaka ya karibuni mawasiliano haya yamebeba jukumu kubwa katika kuhimiza maingiliano, kujifunza kwa pamoja, na kuishi pamoja kwa maelewano kati ya watu wa pande hizi mbili, jambo ambalo limewafanya wawe karibu zaidi, na hata kuimarisha ushirikiano wao katika masuala ya utamaduni kati ya China na Afrika.

Pande mbili zimeendelea kusaini makubaliano mbalimbali ya utekelezaji wa programu na matokeo yake yamekuwa yakitia hamasa kwa pande mbili kuendelea mbele zaidi na uhusiano wao. Mfano mzuri ni mradi uliofadhiliwa na China unaojulikana kama “Upatikanaji wa TV za Satelite katika Vijiji 10,000 vya Afrika”. Mradi huu umenufaisha vijiji vingi vya Afrika ambavyo hapo awali ilikuwa shida sana kwa wanavijiji hao kuulewa ulimwengu wa nje. Mbali na televisheni hizi kuungwa majumbani, pia zinapatikana hata kwenye zahanati, shule za msingi, na maeneo mengine ya umma, zikiwa na lengo la kuboresha maisha ya wanakijiji.

Katika kukabiliana na kasi ya utandawazi na ushirikiano wa kikanda serikali ya China, chini ya kiongozi wake rais Xi Jinping, inahamasisha mashirika yasiyo ya kiserikali ya China yaliyopo katika nyanja zote za kijamii kushiriki katika diplomasia kati ya watu wa China na Afrika na kuwa na mawasiliano ya kiutamaduni, mbinu ambayo inaweza kuimarisha mazungumzo baina ya watu na kuleta maelewano ya kiutamaduni kati ya China na Afrika.

Hadi kufikia Disemba 2020, mipango 346 ya utekelezaji ilitiwa saini na kutekelezwa. Na kabla ya hapo kutoka mwaka 2013 hadi 2020, Vikundi vya Sanaa 140 vya China vilikuwa tayari vimeshatembelea Afrika na kufanya maonesho, huku vikundi 28 kutoka nchi za Afrika vikiwa vimealikwa kuja China kutumbuiza.

Mawasiliano ya utamaduni yamefungua fursa nyingi sana katika kipindi hiki cha miaka 10 ya utawala wa rais Xi, hasa tangu China ianze kutumia filamu na tamthilia zake kutambulisha na kueneza utamaduni wake kwa nchi za Afrika. Kwa mara ya kwanza tamthilia maarufu ya “Doudou na Mama Wakwe Zake” ilioneshwa Tanzania mwaka 2011, kutokana na filamu hii kujibebea umaarufu mkubwa, iliweza kutandika njia kwa tamthilia nyingine nyingi tu za China kuonekana katika nchi za Afrika. Kupitia njia hii Waafrika wengi wamenufaika hasa kwa kupatiwa ajira, na kubwa zaidi kukuza maingiliano ya kiutamaduni.

Kuna matukio mengi tu yanayofanyika kupitia mawasiliano kati ya watu wa China na Afrika pamoja na maingiliano ya kiutamaduni, kama vile Mkutano wa Wanahabari wa China na Afrika na Jukwaa la Ushirikiano wa Vyombo vya Habari kati ya China na Afrika. Vyombo 30 vya habari vya Afrika vimejiunga na Muungano wa Habari za “Ukanda Mmoja Njia Moja”, na nchi 42 za Afrika zimeshiriki katika Kongamano la Mkutano wa Jumuiya ya Vyombo vya Habari vya“Ukanda Mmoja Njia Moja”.

Kwa upande wa elimu licha ya kwamba China kila mwaka inatoa udhamini wa masomo kwa wanafunzi wa Afrika kuja China kusoma ama kuwafadhili kwa kuwawezesha kusoma katika vyuo vikuu vya nchi zao, pia China na Afrika zimekuwa zikiungana mkono kwenye ushirikiano kati ya taasisi za utafiti wa kielimu, washauri bingwa na hata vyuo vikuu mbalimbali.

Watu wa China na watu wa Afrika wameonesha kwa vitendo kwamba hakuna kisichowezekana chini ya jua, na kufanya nchi zao kuwa mahali pazuri ambapo watu wa pande zote mbili wanaweza kuishi kwa amani na usalama huku wakiwa na maelewano makubwa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom