Maigizo ya Kisarawe leo 28th June 2020. Kila kitu kilipangwa

Huyu jamaa anapewa ubalozi wa kudumu somalia
tapatalk_1593365899396.jpg
 
1. Aliyepewa u-DAS alikua ameandaliwa mapema.

2. Kufukuzwa kwa DAS Mwampamba hakuhusiani kabisa na wake za watu wa Kisarawe.

3. Wakati wote walijifanya hawamjui sana Jokate.

4. Huyu dada alijua mapema kabisa leo anapewa u-DAS.

Mambo mengine tuwaachie lakini ukweli huwa hauachi kujiweka peupe. Dalili zote zilikua zinaonekana.

Siku nyingine leteni movi nzuri kidogo.

Jaffo mtoto wa seremala nakukubali sana, mzee baada ya kustafu yamkini atahamia Kisarawe.

View attachment 1491411View attachment 1491412
2. Kufukuzwa kwa DAS Mwampamba hakuhusiani kabisa na wake za watu wa Kisarawe.

Hebu tung'ate sikio mzuvendi wangu kutimiliwa kwake kunahusiana na nini vile?
 
Kwamba mzee kusema nani anafaa kuwa das as if anatafuta kumbe walisha panga nani apewe.

Katika hali ya kawaida, baada ya DAS kutumbuliwa nafasi yake ingekuwa wazi hivyo kudai kujazwa kwa taratibu za kiofisi. Kwa vyovyote vile, na kwa kuzingatia muundo wa ofisi husika, huyo huyo Afisa Tawala ndiye angekaimu na baada ya muda kuthibitishwa. Kwa hali hiyo watu wasingekuwa ma maswali mengi.
 
Kiongozi wa ofisi ya umma, tena kwa nafasi ya DAS achaguliwe kwenye jukwaa la siasa, bila kufanyika vetting yoyote? Umewahi kuona wapi hiyo boss?

Na kuna mahali CDM wamedai DAS aliyetumbuliwa alikuwa kada wao wa zamani kabla ya kufukuzwa kwa utovu wa nidhamu!. Ndiyo kusema huyo naye hakufanyiwa vetting; vinginevyo asingepata uteuzi mapema. Utumishi wa umma unapitia changamoto nyingi.
 
Na kuna mahali CDM wamedai DAS aliyetumuliwa alikuwa kada wao wa zamani kabla ya kufukuzwa kwa utovu wa nidhamu!. Ndiyo kusema huyo naye hakufanyiwa vetting; vinginevyo asingepata uteuzi mapema. Utumishi wa umma unapitia changamoto nyingi.

Hapo hatuzungumzii kuwa na nidhamu au la, nasemea hilo igizo la kumteua DAS kwenye mkutano wa hadhara.
 
Katika hali ya kawaida, baada ya DAS kutumbuliwa nafasi yake ingekuwa wazi hivyo kudai kujazwa kwa taratibu za kiofisi. Kwa vyovyote vile, na kwa kuzingatia muundo wa ofisi husika, huyo huyo Afisa Tawala ndiye angekaimu na baada ya muda kuthibitishwa. Kwa hali hiyo watu wasingekuwa ma maswali mengi.
Mkuu hayo siku hizi hayapo!Siku hiyo inategemeana na Yesu kaamkaje!
 
Back
Top Bottom