Maigizo: In memories of machiavelli, shaaban robert and shakespeare | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maigizo: In memories of machiavelli, shaaban robert and shakespeare

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tanganyika jeki, Jun 28, 2012.

 1. T

  Tanganyika jeki JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 12, 2011
  Messages: 243
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kwa wasio wavivu wa kusoma literatures mbalimbali unawakumbuka hao. Sasa nisome.
  Serikali inaanza kufanya juhudi kubwa ya kujinasua na kashfa kubwa ya ukiukwaji wa haki za binadamu dhidi ya Dk. Ulimboka. Maelezo yanayojitokeza ni:-

  Mosi, kuonesha kuwa hilo laweza fanywa na watu wahanga (wagonjwa au ndugu zao au wafiwa)wenye hasira na chuki dhidi ya madaktari. Kwa mtazamo wangu. Mmoja wa ndugu mhanga alikodi kikundi cha wajambazi waliowezeshwa kutenda waliyotenda. Polisi watawakamata kuteswa na baadaye watakiri uhusika wao kisha watapelekwa mahakamani kumalizia sehemu iliyobaki ya igizo

  Pili, CHADEMA yahusika. Hili laweza fanywa na wabaya kisiasa wa serikali na CCM ili kuionesha na kuthibitisha ni dhaifu. Hapa CHADEMA km wapinzani wakuu wanausishwa kushiriki kufanya unyama huu ili serikali ya CCM ichukiwe zaidi na umma na pia kuthibitisha kauli ya Mb. Mnyika kuhusu udhaifu wa rais na taasisi anazoziongoza za kiserikali. walichofanya ni kutumia majasusi maalumu waliofuzu. Sinema ikafanyika pia asiuawe ili atoe maelezo yatakayo'implicate serikali (ya CCM)

  Tatu, I love God!! Human being is the most unpredictable and complex creature in the universe! Most of the time here logic is defied. Ulimboka anahusika! Ndiyo. Dr. Ulimboka anahusika kumdhuru Dr. Ulimboka, ili? Serikali imekwenda mahakamani ikaweza kuzuia mgomo. Inaanza kufanikiwa kuwashawishi wahariri ili iandikwe vizuri au isiandikwe vibaya kuhusu uzembe wake. Watu taratibu wanaanza kuwaona madaktari si wazalendo na wabinafsi. kwa hiyo, igizo. Sterling. Dr. Uli. Wasoamaji wa liwaya au watazamaji wa senema ni wengi. Mtunzi ni mmoja au wawili (wachache). Apate nini kwa igizo hilo. Public sympathy and delay kamba iliyoning'nizwa shingoni.

  Nne, CCM yahusika. Toba! Ndiyo. Mchezo ulikuwa hivi. CCM ilianza kupoteza mvuto kwa wananchi kwa kila pembe ya nchi na wapinzani wao hasa CHADEMA 'wakitakata'. Fursa ikajitokeza. Dk. ULIMBOKA. CCM hatumpendi. Anatuharibia mvuto na kuisumbua serikali. Madai yake pia ni makubwa na yatatoa pressure zaidi kwa serikali ya CCM. Uli ni adui namba tatu baada ya CHADEMA, na UAMSHO. Igizo likafanyika. Ili? CHADEMA waonekane wahusika na uovu huo. Ili kuunogesha uhusika wa CHADEMA watu watakamatwa wakiwa ni wanachama wa CHADEMA na kukiri uhusika wao. Maelezo yaliyobaki nenda kasome Chuo cha sanaa hasa art ya uigizaji.

  Tano, CCM yahusika. Tena? Ndiyo. Moja la kundi na mtandao wa kutafuta urais wa mwaka 2015. Linataka nini. Serikali ipatayo maagizo ya Riz 1 na Nape ipwaye na kuchikiwa na wanaCCM wataoona afadhali Loh! hasa, na hivyo wapinzani wake hasa Maembe, Seven minus one, na Mingi Loh! Hivyo wanaccm ili kujinasua waone uongozi sahihi ni wa nywele za uzeeni. Pia, wananchi waone afadhali yeye 'ukali' wake utasaidia. Waigizaji ni majasusi ya kukodiwa.

  Sita, CCM tena! Nywele za uzeeni au seven minus one. Urais 2015. Ili kuidhofisha serikali. kwanza kulipa kisasi. pili kuionesha serikali hii na ccm dhaifu kwa sababu ya ulegevu wake. Wahusika wanausalama wa taifa bila "Usalama wa Taifa" kuhusika. Patamu hapo.

  Hitimisho. Baada ya maigizo haya hebu turudi kwenye uhalisia wa mambo.
  1. Serikali ya CCM na Kikwete haikwepi lawama. Ulinzi na usalama wa raia kikatiba ni wajibu wao.
  2. Km serikali ilitoa ulinzi kwa Dr. Slaa wakati wa uchaguzi 2010 kwa maslahi ya Taifa kwanini haikufanya hivyo kwa Ulimboka?
  3. Siraha zilizotumika, mdhibiti mkuu ni serikali
  4. Ilipopewa taarifa (ya kutekwa au kupotea) kwa nini iliwachukua muda mrefu kuchukua hatua stahiki za uokozi
  5. CCM imekuwa upande mbaya wa kihistoria kwa jambo hili kwa kuwa upande wa serikali blindly

  Nawasilisha.


  'hakika nawaambieni mmoja miongoni mwenu atanisaliti'.
   
Loading...