Maige awashukia viongozi wa Tanapa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maige awashukia viongozi wa Tanapa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Dec 21, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,158
  Likes Received: 417,585
  Trophy Points: 280
  Maige awashukia viongozi wa Tanapa


  na Hellen Ngoromera


  [​IMG] WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige, amewakemea viongozi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na kuwataka kuepuka matumizi ya fedha yasiyoendana na shughuli za uhifadhi hasa ufanyaji wa safari za nje zisizo na tija. Alikemea pia ununuzi wa magari ya kifahari na kusema anataka kuona ununuzi wa magari unafanyika hasa kwa magari ya porini pekee.
  Maige alisema hayo jana jijini Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari muda mfupi baada ya kumaliza kufanya kikao cha pamoja na bodi ya TANAPA.
  “Epukeni matumizi ya fedha yasiyoendana na uhifadhi, safari za nje na posho za ajabu ajabu, msiruhusu pia ununuzi wa magari ya kifahari,” alisema Waziri Maige.
  Kwa mujibu wa waziri huyo, haimwingii akilini kumwona kiongozi wa wizara akishiriki kwenye maonyesho kwa wiki mbili katika nchi fulani bila manufaa na kwamba hali hiyo inamkera.
  Badala yake aliitaka TANAPA kuelekeza nguvu zake kuajiri askari wengi wa wanyamapori ili kuongeza tija katika utendaji kazi wa askari hao katika kudhibiti majangili.
  Aliwataka pia kupitia upya rasilimali walizonazo pamoja na pia kuweka mipango thabiti ya muda mfupi kupambana na vitendo vya ujangili.
   
 2. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #2
  Dec 21, 2010
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Maige naye kumbe wamo.Ila tusubiri tuone,isije ikawa maneno matupu yasiyo na tija kama ADNIP.
   
Loading...