Mahususi kwako wewe mwenye kujielewa

anco

anco

Member
Joined
Jun 1, 2014
Messages
37
Points
95
anco

anco

Member
Joined Jun 1, 2014
37 95
Bila ya kupoteza muda wana MMU.

Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka kati ya 26~30.

Nimekuja kwenu hasa wanawake wenye kujitambua na kujielewa naomba wanisaidie hili. Ingawa Wanaume pia mnaruhusiwa

Hivi kwa dunia hii inavyoenda kasi, hakuna mwanamke yeyote yule ambae anahitaji kupata tulizo la moyo wake kutoka kwa mwanaume shupavu na hodari wa kila kitu!

Yawezekana anajitosheleza kiasi fulani kimaisha lakini hana tulizo la moyo katika mapenzi. Naamini sio wote Wapenda hela, ila wanazihitaji tu.

Nauliza hivi kwa sababu baada ya kumaliza masomo yangu ya chuo, nilianza kuzunguka na bahasha maofisini kutafuta ajira bila ya mafanikio.
Nikawa na wazo la kujiajiri yaani wazo hili ni plan B baada ya plan A kufeli.
Lakini imejitokeza changamoto kwenye kujiajiri, changamoto ya ukosefu wa mtaji.

Nimejaribu kuwashirikisha baadhi ya Wanaume wenzangu juu ya hili lakini naona baadhi yao wanaona kuhonga ili wapate wanachohitaji kwa wanawake ni bora kuliko lolote. Hapa ndipo paliponiuma haswa kuwa hivi wanawake hawana huruma kuwa lazima tutoe sisi, au lazima tuwawezeshe sisi. Bila kujali na sisi wengine ni Wanaume suruali tu!

Sasa nimeamua niwaelekee wanawake wenye kujielewa. Akili yangu na mawazo yakinifu ya kupambana na maisha bado ipo active sana yaani bado ina upeo wa kutafuta fursa na kuzipambania.

Changamoto ya mtaji kwangu ni kero kubwa sana ingawa nina uzoefu wa mapambano mbali mbali na kazi mbali mbali za kimaisha lakini ndio hivyo.

Kwa sasa nimeweka vyeti vyangu vyote pembeni ili nijitoe mzima mzima.

Lakini mwisho wa yote umri wangu unayoyoma, sina kazi, sina fedha, lakini pia siwezi kumiliki mke mwenye kuhitaji kuhudumiwa kifedha kwa sasa kutokana na uhalisia uliopo.

Niliwahi kuwa na kipenzi changu lakini kutokana na ukosefu wa kuweza kumkidhia mahitaji yake. Nimemruhusu aende.

Nahitaji mwanamke ambae yeye awe kama mdhamini wangu lakini pia kama atakubali tuje kuwa mume na mke (wapendanao).

Nina uwezo wa kuishi popote iwe Tanzania au nje ya Tanzania katika kusaka maisha.

Nitambue Mimi nilivyo kwa sifa kumi hizi.

1. Mimi si mfupi na wala si mrefu.
2. Sina ubaya wa sura lakini siyo handsome boy kivilee ila navutia km mume wa mtu ni mzuri zaidi kwenye ubongo wangu (akili).
3. Mimi si mweusi lakini sina weupe ule wa sifa ya weupe.
4. Mimi si mwembamba na wala si mnene (sio kibonge)
5. Mimi sina hela ila nina akili, nguvu, nia na imani ya kutafuta fedha na nikafanikiwa kuzipata kwa kudura na mapenzi ya muumba.
6. Mimi ni muumini wa dini yaani sina imani za kishirikina.
7. Nimetimia kwa viungo vyangu vyote vya kimwili.
8. Nina nguvu zote anazohitajika kuwa nazo mwanaume.
9. Mimi si mpole, lakini pia si kilopolopo. Ila mimi ni muongezeaji mzuri tu na ni mcheshi.
10. Ni mwepesi wa kuomba msamaha na kuhitaji suluhu pale ninapokosea.

Hii I'd yangu imekuwa kama mpya baada ya kuisahau password yangu kutokana na kutoingia humu ndani kws muda mrefu katika kupambania maisha. Lakini mimi ni memba msomaji tangu 2013 na nilijiunga rasmi humu 2015. Hivyo ni mgeni mzoefu lakini maisha tu uniweka mbali na JF.
Baada ya kupoteza password yaani nimeisahau ndipo nilipopeleka maombi ya kupata password ndio imekuja hivi...

Nikimpata mwanamke wa kuweza kufanikisha hili nitafurahi sana kwa sababu yeye ndiye atakuwa anaujua uchungu halisi wa mali au pesa alizonipa, alizonikopesha, alizonidhamini kuliko mwanamke ambae atakuja kwangu baada ya kuona nina pesa.

Nakaribisha maoni na ushauri wenu. Mwenye kuguswa na hili na mweye kuhitaji tulizo la moyo kama nilivyoeleza huko juu karibu PM na wala sitoifunga mpaka nimpate yule barafu wa moyo. Ili nisirudi nyuma kwa mapambano.
 
Bikini

Bikini

Senior Member
Joined
Oct 16, 2018
Messages
191
Points
250
Bikini

Bikini

Senior Member
Joined Oct 16, 2018
191 250
Dah..... Umarioo usiku huu mkuu? Unataka kuolewa???? Angalia hii mimi nilipitia maisha ya misukosuko sana ila nilipambana bila kukata tamaa hatimaye naweza sema Mungu kaniona... Naishi nitakavyo, kazi za vibarua zipo kibao acheni ublazamen wa chuoni.. utatolewa linda na mkanda wa Bikini...

All the best.
 
anco

anco

Member
Joined
Jun 1, 2014
Messages
37
Points
95
anco

anco

Member
Joined Jun 1, 2014
37 95
Utampenda?
Au wewe unapenda yeyote tu?
Nitampenda mwenye kunipenda. Akija kwa kunikopesha sawa, kunidhamini sawa au kuja Jumla jumla ili tuje kuijenga familia pia sawa.
Ila Vigezo na masharti yangu ndio hayo hapo juu
 
Madam vivian original

Madam vivian original

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2018
Messages
361
Points
1,000
Madam vivian original

Madam vivian original

JF-Expert Member
Joined Jul 14, 2018
361 1,000
Sijakuelewa mkuu unahitaji nn hasa,

1) Unatafuta mpz baadae muwe mke na mume

2) unatafuta partner wa kike wa kufanya biashara.

3) unatafuta MTU akusaidie mtaji/ akukipeshe ufanye biashara

Ushauri wangu kwako ndugu,

Tafuta mtu au ndugu yko mwenye nafuu ya maisha akusaidie mtaji wa biashara, ukikosa kabisa nenda kakope hata kwenye visaccos ukipata mtaji hata wa laki3 tafuta site nzuri anza kuchakalika, fungus hata banda LA chips ndani ya miez6 utafika mbali trust me.

Sikushauri uingie kwenye biashara na mwanamke au msichana utafeli kijana, pambana mwenyewe utafanikiwa. Kila LA kheri
 
anco

anco

Member
Joined
Jun 1, 2014
Messages
37
Points
95
anco

anco

Member
Joined Jun 1, 2014
37 95
Dah..... Umarioo usiku huu mkuu? Unataka kuolewa???? Angalia hii mimi nilipitia maisha ya misukosuko sana ila nilipambana bila kukata tamaa hatimaye naweza sema Mungu kaniona... Naishi nitakavyo, kazi za vibarua zipo kibao acheni ublazamen wa chuoni.. utatolewa linda na mkanda wa Bikini...

All the best.
Nimekuelewa mkuu. Epusha huo umarioo kwa kutoa hizo nafasi za vibarua kwa mimi mwanaume mwenzako ambae nimekaza mkanda wa suruari yangu ili wewe uwe tofauti na wale wasema hovyo lakini hufundisha wengine waseme mazuri
 
anco

anco

Member
Joined
Jun 1, 2014
Messages
37
Points
95
anco

anco

Member
Joined Jun 1, 2014
37 95
umri kati 26-30.

26+30=56

56÷2=28

nimemrahisishia mke wako kupata umri wako kamili maana wanawake hawapendi hesabu/mathematics.
Upo sahihi ila si wanawake wote hawapendi hesabu. Hizo namba umezichanga vema lakini mimi si mzee. Maana hiyo 56 hainihusu.
 

Forum statistics

Threads 1,335,546
Members 512,359
Posts 32,509,312
Top