MwanajamiiOne
Platinum Member
- Jul 24, 2008
- 10,470
- 6,562
Wapwaz na Mabinamu..........
Katika pita pita yangu huku na huku nikitafuta kusuuza macho-nimekutana na hii post kule harusi yangu. Nimeona niilete hapa ili tumsaidie huyu dada, maana kule imezua mjadala mkali sana. Ningependa kupata mawazo yenu ndugu zangu wa nyumbani.
Nanukuu..............."Mimi ni binti wa miaka kadhaa, nina mtoto mmoja lakini nimezaa na mume wa mtu. Hiki kitendo huwa nakijutia sana. natamani kuachana nae, lakini kwa jinsi anavyonipenda na kunitunza inaniwia vigumu. Hana matatizo, anampenda mkewe kama anavyonipenda mimi, na mimi na mheshimu sana mkewe. amekuwa akifanya vitu kwangu na kwa mkewe kwa usawa. nyumba kama aliyojenga ya kwake wanayokaa na mkewe, ndio alivyojenga yangu. gari kama analotembelea mkewe ndio na mimi nililonalo. Simu tunazo sawa. huwa ni mtu wa kusafiri sana nje. safari hii akisafiri na mkewe, inayofata mimi. Kusema ukweli, hamnyanyasi mkewe, ana upendo wa dhati. Na kwangu hana matatizo. ninacho mkataza ni kulala kwangu. na kukaa kwangu zaidi ya saa 2 usiku. huwa namwambia awahi nyumbani kufanya home work na watoto.
kinachonitatiza ni kuwa nataka niachane nae huyu mtu. Roho inaniuma naona kama nitakuwa simtendei haki. Najua nitamwathiri sana. kuna siku nilimgusia kuachana, aliongea kwa upole akasema, mbona nakupenda sana, si kubagui na mke wangu. nawapenda wote sawa. ebu fikiri utaniacha na hali gani? akasema ukiniacha ndio utanituma niende nikafanye uhuni, na utanifanya nikaanze kunywa tena pombe ovyo, kama ilivyokuwa kabla hatujakuwa pamoja. Nisaidieni wadau. Pleasee msinitukane nahitaji mawazo yenu ya busara."....... Mwisho wa kunukuu.
Ninashusha kwanza pumzi. Kwa kweli maisha ya mahusiano ni magumu.
Source: http://www.harusiyangu.com/forumreplies.php?topicid=569