Mahusiano!!!!

MwanajamiiOne

Platinum Member
Jul 24, 2008
10,470
6,562
Wapwaz na Mabinamu..........

Katika pita pita yangu huku na huku nikitafuta kusuuza macho-nimekutana na hii post kule harusi yangu. Nimeona niilete hapa ili tumsaidie huyu dada, maana kule imezua mjadala mkali sana. Ningependa kupata mawazo yenu ndugu zangu wa nyumbani.

Nanukuu..............."Mimi ni binti wa miaka kadhaa, nina mtoto mmoja lakini nimezaa na mume wa mtu. Hiki kitendo huwa nakijutia sana. natamani kuachana nae, lakini kwa jinsi anavyonipenda na kunitunza inaniwia vigumu. Hana matatizo, anampenda mkewe kama anavyonipenda mimi, na mimi na mheshimu sana mkewe. amekuwa akifanya vitu kwangu na kwa mkewe kwa usawa. nyumba kama aliyojenga ya kwake wanayokaa na mkewe, ndio alivyojenga yangu. gari kama analotembelea mkewe ndio na mimi nililonalo. Simu tunazo sawa. huwa ni mtu wa kusafiri sana nje. safari hii akisafiri na mkewe, inayofata mimi. Kusema ukweli, hamnyanyasi mkewe, ana upendo wa dhati. Na kwangu hana matatizo. ninacho mkataza ni kulala kwangu. na kukaa kwangu zaidi ya saa 2 usiku. huwa namwambia awahi nyumbani kufanya home work na watoto.

kinachonitatiza ni kuwa nataka niachane nae huyu mtu. Roho inaniuma naona kama nitakuwa simtendei haki. Najua nitamwathiri sana. kuna siku nilimgusia kuachana, aliongea kwa upole akasema, mbona nakupenda sana, si kubagui na mke wangu. nawapenda wote sawa. ebu fikiri utaniacha na hali gani? akasema ukiniacha ndio utanituma niende nikafanye uhuni, na utanifanya nikaanze kunywa tena pombe ovyo, kama ilivyokuwa kabla hatujakuwa pamoja. Nisaidieni wadau. Pleasee msinitukane nahitaji mawazo yenu ya busara."....... Mwisho wa kunukuu.

Ninashusha kwanza pumzi. Kwa kweli maisha ya mahusiano ni magumu.
Source: http://www.harusiyangu.com/forumreplies.php?topicid=569
 
kinachonitatiza ni kuwa nataka niachane nae huyu mtu. Roho inaniuma naona kama nitakuwa simtendei haki. Najua nitamwathiri sana. kuna siku nilimgusia kuachana, aliongea kwa upole akasema, mbona nakupenda sana, si kubagui na mke wangu. nawapenda wote sawa. ebu fikiri utaniacha na hali gani?
Mbona hajatoa sababu ya kutaka kumwacha? nn shida mapenzi yameisha? au?
 
Mwana jamii!huyo dada anajidanganya,mtu unamoyo mmoja utapendaje wawili?yyanamuonea huruma huyo mwanamme,kwann hamuonei huruma huyo mama?anauhakika gani kama uduma nyingine anazipata?maana yy anaona yanayoonekana tu,je jamaa anamwambia kuhusu huduma za kimwili?alifanya makosa makubwa hata bible imesema kila mtu na awe na mume wake mwenyewe,yy kann anachukua wa mwenzie?TENA MWAMBIE PEARL ANAKUCHUKIA KWA KITENDO ULICHOFANYA NA NINGEMJUA MKE WA HUYO JAMAA NINGEMWAMBIA.
 
Mbona hajatoa sababu ya kutaka kumwacha? nn shida mapenzi yameisha? au?

kimey (Hili jina naliogopaga maana linafanana na la Chairman wa Board ya ofcn kwetu lol- I hope si mwenyewe)

Kwenye hayo mahojiano yeye anadai si kuwa mapenzi yamekwisha yeye anajisikia vibaya tu kuendelea na mume wa mtu. Nimechoka ndo maana nikasema ngoja nishushe pumzi kwanza.
 
kusafiri naye ni zawadi tu kama zawadi nyingine, asogope kupokea. inabidi ajiulize kama anataka kupata mume wake mwenyewe, itabidi kumuacha huyu kwani wakiendelea naye hataolewa na mwingine na umri utamtupa mkono punde japo hakusema sasa ana miaka mingapi.

wajadili wakati muafaka wa kumjulisha mkwe kuwa ana mtoto nje ya ndoa. hapo ndipo penye kuhitaji hekima kubwa.

kuzaa na mtu mtoto si mchezo, utalazimika kumtunza na kuwasiliana naye hadi mwisho wa maisha yenu......................

kama ni mcha Mungu azingatie kuwa ayafanyayo ni uasherati mbaya na kamtia mume wa mtu katika majaribu ya uzinzi............. neno la Mungu linasema "makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake yule yajayo kwa sababu yake, imempasa huyo kufungiwa jiwe la kusagia shingoni mwake na kutupwa baharini ............. kuliko kumkosesha mmoja wa hawa"
 
Mwana jamii!huyo dada anajidanganya,mtu unamoyo mmoja utapendaje wawili?yyanamuonea huruma huyo mwanamme,kwann hamuonei huruma huyo mama?anauhakika gani kama uduma nyingine anazipata?maana yy anaona yanayoonekana tu,je jamaa anamwambia kuhusu huduma za kimwili?alifanya makosa makubwa hata bible imesema kila mtu na awe na mume wake mwenyewe,yy kann anachukua wa mwenzie?TENA MWAMBIE PEARL ANAKUCHUKIA KWA KITENDO ULICHOFANYA NA NINGEMJUA MKE WA HUYO JAMAA NINGEMWAMBIA.

Dada wee laiti ungeingia kwenye hiyo link ndo ungejua kinachotembea kwenye vichwa vya wengine.

Yeye mwenyewe anadai anamheshimu sana bi mkubwa na akiwa na huyu mbaba anahakikisha kuwa halali kwake kwani ikifika saa mbili tu usiku anamfukuza akalale kwa mkewe.
 
halafu tunaambiwa waombeeni waume zenu...mweh! bwana hii hapa ni kama vile huyu mdada kaona mbele, labda huyu baba amepungukiwa kitu fulani kwasasa, labda pesa/huduma anaona zinayumba ndio mana anataka kumuacha,wakiambiwa huko nje yanachunwa tu hayaelewi....
 
Mwana jamii!huyo dada anajidanganya,mtu unamoyo mmoja utapendaje wawili?yyanamuonea huruma huyo mwanamme,kwann hamuonei huruma huyo mama?anauhakika gani kama uduma nyingine anazipata?maana yy anaona yanayoonekana tu,je jamaa anamwambia kuhusu huduma za kimwili?alifanya makosa makubwa hata bible imesema kila mtu na awe na mume wake mwenyewe,yy kann anachukua wa mwenzie?TENA MWAMBIE PEARL ANAKUCHUKIA KWA KITENDO ULICHOFANYA NA NINGEMJUA MKE WA HUYO JAMAA NINGEMWAMBIA.

nimeshindwa kujizuia wewe twin
nimecheka utadhani mazuri. sasa ukimchukia kwani itampunguzia nini twin? ila kweli hapo kwenye kumsemelezea ningekusindikiza
afu mbona hupokei cm ntanuna mimi
 
.........."Mimi ni binti wa miaka kadhaa, nina mtoto mmoja lakini nimezaa na mume wa mtu. Hiki kitendo huwa nakijutia sana. natamani kuachana nae, lakini kwa jinsi anavyonipenda na kunitunza inaniwia vigumu. Hana matatizo, anampenda mkewe kama anavyonipenda mimi, na mimi na mheshimu sana mkewe. amekuwa akifanya vitu kwangu na kwa mkewe kwa usawa. nyumba kama aliyojenga ya kwake wanayokaa na mkewe, ndio alivyojenga yangu. gari kama analotembelea mkewe ndio na mimi nililonalo. Simu tunazo sawa. huwa ni mtu wa kusafiri sana nje. safari hii akisafiri na mkewe, inayofata mimi. Kusema ukweli, hamnyanyasi mkewe, ana upendo wa dhati. Na kwangu hana matatizo. ninacho mkataza ni kulala kwangu. na kukaa kwangu zaidi ya saa 2 usiku. huwa namwambia awahi nyumbani kufanya home work na watoto.

kinachonitatiza ni kuwa nataka niachane nae huyu mtu. Roho inaniuma naona kama nitakuwa simtendei haki. Najua nitamwathiri sana. kuna siku nilimgusia kuachana, aliongea kwa upole akasema, mbona nakupenda sana, si kubagui na mke wangu. nawapenda wote sawa. ebu fikiri utaniacha na hali gani? akasema ukiniacha ndio utanituma niende nikafanye uhuni, na utanifanya nikaanze kunywa tena pombe ovyo, kama ilivyokuwa kabla hatujakuwa pamoja. Nisaidieni wadau. Pleasee msinitukane nahitaji mawazo yenu ya busara."...

MWJ'1

Nionalo mimi hapa huyu Binti anatingisha kibiriti ili huyo mzazi mwenziwe achague either huyo mke wa ndoa au yeye...

Selfish and stupid woman. Kama hajali yote anayofanyiwa kwa usawa na huyo bwana, vipi haki za mtoto wao pia hazioni?

Nikiwa ni mwanaume, najua kwanini inakuwa ngumu kwa mwanaume huyo kuachana na mwanamke huyo, kwani "gharama"-(kisaikolojia) za kumtunza huyo mtoto zitakuwa "ghali" kuliko ilivyo sasa.
 
Dada wee laiti ungeingia kwenye hiyo link ndo ungejua kinachotembea kwenye vichwa vya wengine.

Yeye mwenyewe anadai anamheshimu sana bi mkubwa na akiwa na huyu mbaba anahakikisha kuwa halali kwake kwani ikifika saa mbili tu usiku anamfukuza akalale kwa mkewe.

hapo nina mashaka napo,mpaka wameanzana hadi leo hii anataka kusema huyu baba hajawahi kulala hapo kwake kwenye nyumba aliyomjengea, hapana!

angemuheshimu asingemwibia mwenzie mume wake
asitudanganye hapa
 
1 .. Uke wenza una Mambo

2 .. Penzi haligawanyiki!

3 .. Huyo Dada Kicheche! Amepata mali aliyotaka sasa anataka kutimka! p.u.m.b.a.f.u!

4.. Huyo mke wa "NDOA" ana njaa sana!

5 .. Huyo Mwanaume hajaawaambukiza hao "wake" VVU/HIV? Maana anachomoa huku anachomeka huku (uchafu!).

6 .. Niwahi zangu Zero Pub kunywa BIA!
 
kusafiri naye ni zawadi tu kama zawadi nyingine, asogope kupokea. inabidi ajiulize kama anataka kupata mume wake mwenyewe, itabidi kumuacha huyu kwani wakiendelea naye hataolewa na mwingine na umri utamtupa mkono punde japo hakusema sasa ana miaka mingapi.

wajadili wakati muafaka wa kumjulisha mkwe kuwa ana mtoto nje ya ndoa. hapo ndipo penye kuhitaji hekima kubwa.

kuzaa na mtu mtoto si mchezo, utalazimika kumtunza na kuwasiliana naye hadi mwisho wa maisha yenu......................

kama ni mcha Mungu azingatie kuwa ayafanyayo ni uasherati mbaya na kamtia mume wa mtu katika majaribu ya uzinzi............. neno la Mungu linasema "makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake yule yajayo kwa sababu yake, imempasa huyo kufungiwa jiwe la kusagia shingoni mwake na kutupwa baharini ............. kuliko kumkosesha mmoja wa hawa"

Aksante AK

Wapo waliotoa ushauri kama wako na wapo waliomweleza vingine.

Kuna alosema kuwa anataka nini tena wakati kila kitu anapata? Tena amemuonya kuwa asijaribu kumwacha huyo mbaba na kuolewa na mwingine kwani maisha ya ndoa ni balaa ni bora abakie small house tu.

Na kuna mbaba kachangia kule katoa live kuwa ana nyumba ndogo yenye watoto 2 wakati mkewe halali anao 3.
 
kimey (Hili jina naliogopaga maana linafanana na la Chairman wa Board ya ofcn kwetu lol- I hope si mwenyewe)

Kwenye hayo mahojiano yeye anadai si kuwa mapenzi yamekwisha yeye anajisikia vibaya tu kuendelea na mume wa mtu. Nimechoka ndo maana nikasema ngoja nishushe pumzi kwanza.
ha ha ha hapo kwenye nyekundu usiwe na shaka!! hapo kwenye blue yaani baada ya kujengewa nyumba na kununuliwa gari ndo anajisikia vibaya dah kweli mabinti wa siku izi!
 
hapo nina mashaka napo,mpaka wameanzana hadi leo hii anataka kusema huyu baba hajawahi kulala hapo kwake kwenye nyumba aliyomjengea, hapana!
[/COLOR]

Dada ingia kwenye link hiyo ujionee mambo yaani nimesoma hadi nimechoka.
Mwingine kamwambia haoni uchafu kushare mkuki na mwanamke mwingine. huyu akajibiwa kuwa yeye ana uhakika gani kama mkuki wa mumewe hauchomekwi pengine? Yaani nimecheka hadi machozi yakaitoka
 
huyo aliyelileta, nadhani ameshapata alichokitaka, baas..

actually, ukichunguza, hiyo fukuza fukuza ya saa mbili usiku, ni kwamba from saa tatu anaingi 'baba mwenye nyumba' mwingine.ambaye ndiye aliyetunukiwa pendo la kweli na hiyo nyumba ndogo

hakuna mwanamke atamfukuza mwanaume saaa mbili eti kwa kumwonea huruma bi mkubwa. Ni kwamba anatengeneza tu mazingira waachane. alichokitaka, ameshakipata

hebu mabinamu wa hapa, inawezekana uko na mwanaume unaympenda hata kama ana mke usingemconvince alale kwako na wewe ukapata the morning glory?

kengele ya tahadhari inalia kuwa huyo yuko kikazi zaidi.
 
ha ha ha hapo kwenye nyekundu usiwe na shaka!! hapo kwenye blue yaani baada ya kujengewa nyumba na kununuliwa gari ndo anajisikia vibaya dah kweli mabinti wa siku izi!

hahaha mkuu Kimeya nakwambia siku hizi hakuna kitu!
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom