Mahusiano!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahusiano!!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by MwanajamiiOne, Feb 16, 2010.

 1. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #1
  Feb 16, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,476
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Wapwaz na Mabinamu..........

  Katika pita pita yangu huku na huku nikitafuta kusuuza macho-nimekutana na hii post kule harusi yangu. Nimeona niilete hapa ili tumsaidie huyu dada, maana kule imezua mjadala mkali sana. Ningependa kupata mawazo yenu ndugu zangu wa nyumbani.

  Nanukuu..............."Mimi ni binti wa miaka kadhaa, nina mtoto mmoja lakini nimezaa na mume wa mtu. Hiki kitendo huwa nakijutia sana. natamani kuachana nae, lakini kwa jinsi anavyonipenda na kunitunza inaniwia vigumu. Hana matatizo, anampenda mkewe kama anavyonipenda mimi, na mimi na mheshimu sana mkewe. amekuwa akifanya vitu kwangu na kwa mkewe kwa usawa. nyumba kama aliyojenga ya kwake wanayokaa na mkewe, ndio alivyojenga yangu. gari kama analotembelea mkewe ndio na mimi nililonalo. Simu tunazo sawa. huwa ni mtu wa kusafiri sana nje. safari hii akisafiri na mkewe, inayofata mimi. Kusema ukweli, hamnyanyasi mkewe, ana upendo wa dhati. Na kwangu hana matatizo. ninacho mkataza ni kulala kwangu. na kukaa kwangu zaidi ya saa 2 usiku. huwa namwambia awahi nyumbani kufanya home work na watoto.

  kinachonitatiza ni kuwa nataka niachane nae huyu mtu. Roho inaniuma naona kama nitakuwa simtendei haki. Najua nitamwathiri sana. kuna siku nilimgusia kuachana, aliongea kwa upole akasema, mbona nakupenda sana, si kubagui na mke wangu. nawapenda wote sawa. ebu fikiri utaniacha na hali gani? akasema ukiniacha ndio utanituma niende nikafanye uhuni, na utanifanya nikaanze kunywa tena pombe ovyo, kama ilivyokuwa kabla hatujakuwa pamoja. Nisaidieni wadau. Pleasee msinitukane nahitaji mawazo yenu ya busara."....... Mwisho wa kunukuu.

  Ninashusha kwanza pumzi. Kwa kweli maisha ya mahusiano ni magumu.
  Source: http://www.harusiyangu.com/forumreplies.php?topicid=569
   
 2. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mbona hajatoa sababu ya kutaka kumwacha? nn shida mapenzi yameisha? au?
   
 3. Pearl

  Pearl JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2010
  Joined: Nov 25, 2009
  Messages: 3,042
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Mwana jamii!huyo dada anajidanganya,mtu unamoyo mmoja utapendaje wawili?yyanamuonea huruma huyo mwanamme,kwann hamuonei huruma huyo mama?anauhakika gani kama uduma nyingine anazipata?maana yy anaona yanayoonekana tu,je jamaa anamwambia kuhusu huduma za kimwili?alifanya makosa makubwa hata bible imesema kila mtu na awe na mume wake mwenyewe,yy kann anachukua wa mwenzie?TENA MWAMBIE PEARL ANAKUCHUKIA KWA KITENDO ULICHOFANYA NA NINGEMJUA MKE WA HUYO JAMAA NINGEMWAMBIA.
   
 4. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #4
  Feb 16, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,476
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  kimey (Hili jina naliogopaga maana linafanana na la Chairman wa Board ya ofcn kwetu lol- I hope si mwenyewe)

  Kwenye hayo mahojiano yeye anadai si kuwa mapenzi yamekwisha yeye anajisikia vibaya tu kuendelea na mume wa mtu. Nimechoka ndo maana nikasema ngoja nishushe pumzi kwanza.
   
 5. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 145
  kusafiri naye ni zawadi tu kama zawadi nyingine, asogope kupokea. inabidi ajiulize kama anataka kupata mume wake mwenyewe, itabidi kumuacha huyu kwani wakiendelea naye hataolewa na mwingine na umri utamtupa mkono punde japo hakusema sasa ana miaka mingapi.

  wajadili wakati muafaka wa kumjulisha mkwe kuwa ana mtoto nje ya ndoa. hapo ndipo penye kuhitaji hekima kubwa.

  kuzaa na mtu mtoto si mchezo, utalazimika kumtunza na kuwasiliana naye hadi mwisho wa maisha yenu......................

  kama ni mcha Mungu azingatie kuwa ayafanyayo ni uasherati mbaya na kamtia mume wa mtu katika majaribu ya uzinzi............. neno la Mungu linasema "makwazo hayana budi kuja, lakini ole wake yule yajayo kwa sababu yake, imempasa huyo kufungiwa jiwe la kusagia shingoni mwake na kutupwa baharini ............. kuliko kumkosesha mmoja wa hawa"
   
 6. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #6
  Feb 16, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,476
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Dada wee laiti ungeingia kwenye hiyo link ndo ungejua kinachotembea kwenye vichwa vya wengine.

  Yeye mwenyewe anadai anamheshimu sana bi mkubwa na akiwa na huyu mbaba anahakikisha kuwa halali kwake kwani ikifika saa mbili tu usiku anamfukuza akalale kwa mkewe.
   
 7. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,969
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  halafu tunaambiwa waombeeni waume zenu...mweh! bwana hii hapa ni kama vile huyu mdada kaona mbele, labda huyu baba amepungukiwa kitu fulani kwasasa, labda pesa/huduma anaona zinayumba ndio mana anataka kumuacha,wakiambiwa huko nje yanachunwa tu hayaelewi....
   
 8. bht

  bht JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  nimeshindwa kujizuia wewe twin
  nimecheka utadhani mazuri. sasa ukimchukia kwani itampunguzia nini twin? ila kweli hapo kwenye kumsemelezea ningekusindikiza
  afu mbona hupokei cm ntanuna mimi
   
 9. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,734
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 180
  MWJ'1

  Nionalo mimi hapa huyu Binti anatingisha kibiriti ili huyo mzazi mwenziwe achague either huyo mke wa ndoa au yeye...

  Selfish and stupid woman. Kama hajali yote anayofanyiwa kwa usawa na huyo bwana, vipi haki za mtoto wao pia hazioni?

  Nikiwa ni mwanaume, najua kwanini inakuwa ngumu kwa mwanaume huyo kuachana na mwanamke huyo, kwani "gharama"-(kisaikolojia) za kumtunza huyo mtoto zitakuwa "ghali" kuliko ilivyo sasa.
   
 10. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,768
  Likes Received: 1,678
  Trophy Points: 280
  Hayo macho ulivokuwa unayasafisha, yalichafukia wapi jamani?
   
 11. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #11
  Feb 16, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,969
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0  hapo nina mashaka napo,mpaka wameanzana hadi leo hii anataka kusema huyu baba hajawahi kulala hapo kwake kwenye nyumba aliyomjengea, hapana!

   
 12. bht

  bht JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 10,341
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  angemuheshimu asingemwibia mwenzie mume wake
  asitudanganye hapa
   
 13. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,834
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 180
  1 .. Uke wenza una Mambo

  2 .. Penzi haligawanyiki!

  3 .. Huyo Dada Kicheche! Amepata mali aliyotaka sasa anataka kutimka! p.u.m.b.a.f.u!

  4.. Huyo mke wa "NDOA" ana njaa sana!

  5 .. Huyo Mwanaume hajaawaambukiza hao "wake" VVU/HIV? Maana anachomoa huku anachomeka huku (uchafu!).

  6 .. Niwahi zangu Zero Pub kunywa BIA!
   
 14. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #14
  Feb 16, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,476
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Aksante AK

  Wapo waliotoa ushauri kama wako na wapo waliomweleza vingine.

  Kuna alosema kuwa anataka nini tena wakati kila kitu anapata? Tena amemuonya kuwa asijaribu kumwacha huyo mbaba na kuolewa na mwingine kwani maisha ya ndoa ni balaa ni bora abakie small house tu.

  Na kuna mbaba kachangia kule katoa live kuwa ana nyumba ndogo yenye watoto 2 wakati mkewe halali anao 3.
   
 15. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  ha ha ha hapo kwenye nyekundu usiwe na shaka!! hapo kwenye blue yaani baada ya kujengewa nyumba na kununuliwa gari ndo anajisikia vibaya dah kweli mabinti wa siku izi!
   
 16. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #16
  Feb 16, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,969
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0  yewooomiii, mr wangu nimecheka mpaka ofcn imetetemeka, haaa.
   
 17. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #17
  Feb 16, 2010
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,476
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Dada ingia kwenye link hiyo ujionee mambo yaani nimesoma hadi nimechoka.
  Mwingine kamwambia haoni uchafu kushare mkuki na mwanamke mwingine. huyu akajibiwa kuwa yeye ana uhakika gani kama mkuki wa mumewe hauchomekwi pengine? Yaani nimecheka hadi machozi yakaitoka
   
 18. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #18
  Feb 16, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,768
  Likes Received: 1,678
  Trophy Points: 280
  huyo aliyelileta, nadhani ameshapata alichokitaka, baas..

  actually, ukichunguza, hiyo fukuza fukuza ya saa mbili usiku, ni kwamba from saa tatu anaingi 'baba mwenye nyumba' mwingine.ambaye ndiye aliyetunukiwa pendo la kweli na hiyo nyumba ndogo

  hakuna mwanamke atamfukuza mwanaume saaa mbili eti kwa kumwonea huruma bi mkubwa. Ni kwamba anatengeneza tu mazingira waachane. alichokitaka, ameshakipata

  hebu mabinamu wa hapa, inawezekana uko na mwanaume unaympenda hata kama ana mke usingemconvince alale kwako na wewe ukapata the morning glory?

  kengele ya tahadhari inalia kuwa huyo yuko kikazi zaidi.
   
 19. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #19
  Feb 16, 2010
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,734
  Likes Received: 254
  Trophy Points: 180
  ...:D eti uchafu!
  Kwenye mapenzi kuna uchafu jamani?
   
 20. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #20
  Feb 16, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,768
  Likes Received: 1,678
  Trophy Points: 280
  hahaha mkuu Kimeya nakwambia siku hizi hakuna kitu!
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...