Mahusiano yasiyokuwa na tija, yanapukutisha uchumi

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,264
40,045
Mahusiano mengi yamekuwa ndio chanzo, cha kuwafanya wanaume wengi kuendelea kuwa masikini.

Wanaume wanakuwa wanaingia gharama kubwa, ili kuweza kumridhisha mwanamke, iwe kumjengea nyumba, kumnunulia usafiri mkali, au kuhonga chochote kile, ili mradi aweze kukubalika kwa mwanamke.

Mara kutembelea kwenye viwanja vikali, na kupukutisha zaidi ya milioni kwa siku n.k; huku akiwa hana umiliki wa kiwanda chochote.

Na pale mwanaume anapoishiwa hela; anabaki kukimbiwa na yule mwanamke aliyemwamini atakuwa naye kwa mazingira yote.

Ndio maana wanaume wanao-ona mbali, hawatafuti pisi kali, wanatafuta wale wa kawaida ili kuzuia kupukutisha uchumi.​
 
Mwanaume akiwa na million 5 isiyo na kazi lazma aweke bajeti ya kuhonga mdada, Mdada akiwa na million 5 isiyo na kazi, hatatumia iyo hela kumhonga mwanaume yoyote, atawaza hela nyingine atapewa na mwanaume yupi
Mara nyingi mwanaume akishakuwa na hela, kichwa kinaenda kwa spidi; asipofikiria vizuri, hela imeshakata
 
Tambua wajanja wengi wanadu na mademu ila sio kisifa ivyo, tatizo washamba wengi wanashina pesa mapema na wako na ushamba wa wanawake kwa vile wanashindwa kujua kiakili kabisa kutokana na kutofikiria mbali ila tambua binadamu hata iweje Kuna umri anakuja kumbuka Yale ya ujana na kujiona mjinga sana...
Saikolojia wanawake wanapenda sana kujaliwa kuliko wanavyojali kifupi ni wabinafsi!!! Katika mahusiano ya sasa kwa vijana wa town izo trap wanakimbia wanajipenda kupiga pamba kimtindo wao na hawagana shobo ila mademu wanakuja wenyewe..Tambua kama demu ana washkaji wanne basi Kuna mmoja ni kibishoo hakina pesa ila kinajipenda kisafi na kinakula pamba na iko huyo demu ndo anakipenda kwa dhati.

Kumbuka demu kumkubalia mwanaume ni kitu rahisi mno Tena sana kama atakuwa miongoni mwa vigezo kadhaa na swala la kuombwa hela inategemea na jamaa mwenyewe, katika mahusiano usiwe serious kiujumla utakuja kufa bure.

Usitumie gharama kwa demu ambaye hauna future nae kwani pesa nazo hukata na kutoweka ikabaki kapuku.. kumbuka sijawai kuona pisi kali ambayo kiakili unaweza kuitamanu mara mbili baada ya kulala nayo mpaka sasa na kiuhalisia mwanaume huwezi kutumika kwa demu baada ya kulala nae la sivyo kama ataendelea kuchukua kama sio mkeo basi tambua wewe ni wale washamba.
 
Back
Top Bottom