Mahusiano yanapovunjika, wanawake ndio huumia zaidi...!

Kuweka source kama hivi
hata kama hiyo tafiti itapingwa na wengine itasaidia sana
angalau mtu akisoma atajua hizo tafiti zilifanywa wapi
mfano ukisema tafiti ilifanya Norway itasaidia kwa mtu anaeishi
Magomeni kujua aamini hiyo tafiti au la..

Big up,

Sio tafiti inafanywa Norway halafu unakuja kusema "wanawake" bila ku qualify kwamba sample space ni wanafunzi 300 wa vyuo vikuu vya Oslo walio kati ya miaka 18 na 25 waliochaguliwa kiholela.
 
BT, mmi nakumbuka niliacha ilihali bado napenda but sikuwa na jinsi. oh no by that time i thout it was end of my life. aah baadae nikazoea tu. sasa nimekua mwalimu na ambassador. looh maisha haya ni shule

Hilo pia hutokea kwani kwenye mahusiano sometimes unatakiwa ufanye maamuzi magumu hasa ukiona mtu unampenda sana lakini haeleweki potelea mbali hata kama inauma (NA INAUMA KWELIKWELI), kikiubwa ni upepo tu utapita
 
Challenges zangu zimekuwa backed up na kanuni za statistics nilizozitaja hapo juu kwamba ili probability yako iwe meaningful, inabidi iwe specific.The more specific your sample space is, the more meaningful your statistics are.The more general you are (as in wanawake without further qualification) the more baloney your figures will be...Mpaka sasa sijapewa jibu wanawake gani anaoongelea.

Sijaona nilipojicontradict..Lakini hata kama utasema hii tafiti haionyeshi specificity mimi nadhani sio kweli. Mfano anaposema 'Kati ya wanawake 10 na wanaume 10 walioachwa'..hivi huoni tayari ka'specify' kutoka kwenye wanawake na wanaume wa kawaida hadi wale walioachwa..sijui hapa unachopinga ni nini?. Kwa hiyo specimen hapa ni wale walioachwa kwenye mapenzi.

Lakini kama nilivyosema pale mwanzo ungesoma 'context' nzima usingepinga kwa kiwango hiki...Kwa nilivyoelewa Mtambuzi anataka kutuonyesha tofauti ya wanawake na wanaume katika 'scenario' moja..ambayo ni kuachwa kimapenzi na kuumia zaidi' Wepi ambao wanauguza madonda kwa muda mrefu.

Ni kweli inawezekana tungependa kujua methodology ya hii tafiti lakini kwa vile hajaiweka huenda tafiti yake imekuwa assumed kwa kila 'race', 'nationalities' nk. Na kama kungekuwa na haja i hope angetuambia kuwa huu utafiti unakuwa applicable in such and such countries.
 
Ni kweli Mtambuzi kwani wanawake wengi wapo committed kwenye mahusiano kwani uzoefu unaonyesha kwamba unapompata mwanamke kwa mara ya kwanza kwani wao ndio huwa wa kwanza kuonyesha mahusiano yao kwamba kwa sasa ana belong kwa mtu flani tofauti na wanaume unless mrembo uliemtokea awe ana sifa flani ya kucheza na akili za wanaume pia huwa wa kwanza kuwatambulisha wapenzi wao kwa marafiki mbalimbali. Pia wao ndio watu wa conflict management maana hata kama kakosea huwa ni mwepesi kusamehe na kumpa umaarufu mwanaume hata kama kosa hajafanya. Katika situation kama hii lazima wataumia tu hakuna jinsi ILA TAHADHARI akichoka mwanamke akaamua kusema mahusiano basi hapo kuna baadhi ya wanaume huteteleka maana hata ubembeleze vipi mrembo anagoma.
 
Last edited by a moderator:
MMU gone scientific, l like it! Nakubaliana na Kiranga, kweli hii generalization inasumbua sana, na ndio maana nilibisha ile issue ya wanawake wanene na stress, ilikuwa kiulaya ulaya zaidi.

I think it is high time, kwa wabongo kuanza kufanya tafiti za mahusiano za kibongo zaidi. Najua tuna mambo mengi ya maendeleo yanayotakiwa kifanyiwa utafiti, lkn mahusiano nayo ni muhimu pia!
 
Last edited by a moderator:
Sijaona nilipojicontradict..Lakini hata kama utasema hii tafiti haionyeshi specificity mimi nadhani sio kweli. Mfano anaposema 'Kati ya wanawake 10 na wanaume 10 walioachwa'..hivi huoni tayari ka'specify' kutoka kwenye wanawake na wanaume wa kawaida hadi wale walioachwa..sijui hapa unachopinga ni nini?. Kwa hiyo specimen hapa ni wale walioachwa kwenye mapenzi.

Lakini kama nilivyosema pale mwanzo ungesoma 'context' nzima usingepinga kwa kiwango hiki...Kwa nilivyoelewa Mtambuzi anataka kutuonyesha tofauti ya wanawake na wanaume katika 'scenario' moja..ambayo ni kuachwa kimapenzi na kuumia zaidi' Wepi ambao wanauguza madonda kwa muda mrefu.

Ni kweli inawezekana tungependa kujua methodology ya hii tafiti lakini kwa vile hajaiweka huenda tafiti yake imekuwa assumed kwa kila 'race', 'nationalities' nk. Na kama kungekuwa na haja i hope angetuambia kuwa huu utafiti unakuwa applicable in such and such countries.

Kati ya wanawake 10 walioachwa wa geographical location gani? Wa social-economic bracket gani? Wa elimu gani? Wa "race" gani?

Hivi mnataka kutuambia wanawake woooote, dunia nzima, wana respond sawa kwenye kuachwa?

Tuwalundike wanawake wote wawe kitu kimoja?

Hata hao mapacha wa kufanana nao mara nyingine wanakuwa na tofauti, sembuse wanawake wote wa dunia nzima?

Si ndiyo hizi habari za "Unatoka Afrika? Ahaa, unajua kupika Fufu eeh..."

Wafrika wote mnaonekana mnakula Fufu.

Pleease.

If Africa is not a country, it equally follows that women (and men) are not monolithic and deserve to be treated as so.
 
Hilo pia hutokea kwani kwenye mahusiano sometimes unatakiwa ufanye maamuzi magumu hasa ukiona mtu unampenda sana lakini haeleweki potelea mbali hata kama inauma (NA INAUMA KWELIKWELI), kikiubwa ni upepo tu utapita

kweli kabisa, haya mambo ukiyaacha hivi hivi yatakufanya uwe mtumwa bure....
 
MMU gone scientific, l like it! Nakubaliana na Kiranga, kweli hii generalization inasumbua sana, na ndio maana nilibisha ile issue ya wanawake wanene na stress, ilikuwa kiulaya ulaya zaidi.

I think it is high time, kwa wabongo kuanza kufanya tafiti za mahusiano za kibongo zaidi. Najua tuna mambo mengi ya maendeleo yanayotakiwa kifanyiwa utafiti, lkn mahusiano nayo ni muhimu pia!

Zikifanyika tafiti zetu humu tutashangaa..
wanene wenye ma wowowo ndo 'wanaotesa' lol
wembamba ndo unaweza kukuta wana stress za kutopata
'attention' wanayopata wanene lol mpaka wanatafuta dawa za kichina kuongeza shepu..
while Ulaya ni tofauti lol
 
Sijaona nilipojicontradict..Lakini hata kama utasema hii tafiti haionyeshi specificity mimi nadhani sio kweli. Mfano anaposema 'Kati ya wanawake 10 na wanaume 10 walioachwa'..hivi huoni tayari ka'specify' kutoka kwenye wanawake na wanaume wa kawaida hadi wale walioachwa..sijui hapa unachopinga ni nini?. Kwa hiyo specimen hapa ni wale walioachwa kwenye mapenzi.

Lakini kama nilivyosema pale mwanzo ungesoma 'context' nzima usingepinga kwa kiwango hiki...Kwa nilivyoelewa Mtambuzi anataka kutuonyesha tofauti ya wanawake na wanaume katika 'scenario' moja..ambayo ni kuachwa kimapenzi na kuumia zaidi' Wepi ambao wanauguza madonda kwa muda mrefu.

Ni kweli inawezekana tungependa kujua methodology ya hii tafiti lakini kwa vile hajaiweka huenda tafiti yake imekuwa assumed kwa kila 'race', 'nationalities' nk. Na kama kungekuwa na haja i hope angetuambia kuwa huu utafiti unakuwa applicable in such and such countries.

Mbona kiongozi unahangaika kutoa maelezo mengi utasema hizi finding zimeletwa kwa ajili ya kuzijadili ili kuboresha zaidi, hapa Mtambuzi ameleta hii kitu kuona kama kile kilichomo kina reflect na maisha yetu ya kila siku na ndio maana wadau wanachangia based on their experience in relation to the topic.
 
Binafsi sioni kama nahangaika as u put it..But was trying to respond to Kiranga .
Kama utafuatilia comments zangu utaona na mimi nimejaribu kurespond as per context
Najua tafiti zina 'limitations' nyingi thus why nilitaka tujikite kwenye maudhui kuliko methodology!!
 
Last edited by a moderator:
Nijuavyo mimi kuna mambo yanawahusu wanawake kama wanawake,unapolifanyia utafiti huna haja ya kutafuta wanawake wa "race",imani,kipato tofauti,kinachoangaliwa hapa ni hisia za mwanamke.Mnaobisha kwa kuleta challenge za kipato,race n.k hebu mtuambie hayo yanaathirije alichokisema Mtambuzi mpaka kisababishe tofauti ya outcome aliyoileta hapa?Yaani mnataka utafiti huu uwe umehusika mpaka kule Rombo wakati mwanamke aliyeko Tokyo,Lima,Abuja na Kigoma wote ni wanawake na kinachofanywa kinawahusu wanawake kihisia na kimaumbile!
 
Maudhui hayawezi kusimama kama methodology haijasimama.

Ndio tutarudi kwenye ule mfano wa mtangazaji wa BBC aliyechukua washkaji zake wanne, akaenda nao bar, akawauliza kama wanasikiliza kipindi chake, wakasema wanasikiliza, watatu waliosikiliza wana degree za Masters, mmoja ana secondary school education.

Kesho jamaa kaenda kwenye kipindi anatangaza "75% ya wasikilizaji wa kipindi changu wana degree ya Masters".

Kama unatafuta maudhui tu bila kuuliza methodology unakubali kirahisi tu statistic hiyo.
 
Nijuavyo mimi kuna mambo yanawahusu wanawake kama wanawake,unapolifanyia utafiti huna haja ya kutafuta wanawake wa "race",imani,kipato tofauti,kinachoangaliwa hapa ni hisia za mwanamke.Mnaobisha kwa kuleta challenge za kipato,race n.k hebu mtuambie hayo yanaathirije alichokisema Mtambuzi mpaka kisababishe tofauti ya outcome aliyoileta hapa?Yaani mnataka utafiti huu uwe umehusika mpaka kule Rombo wakati mwanamke aliyeko Tokyo,Lima,Abuja na Kigoma wote ni wanawake na kinachofanywa kinawahusu wanawake kihisia na kimaumbile!

Wewe kimsingi unachosema ni kwamba wanawake wote wako sawa.

Tuonyeshe umejuaje hilo?
 
Hivi mnataka kutuambia wanawake woooote, dunia nzima, wana respond sawa kwenye kuachwa?

Sidhani kama ni sahihi kila kitu akutafunie Mtambuzi
Unaweza kuja na tafiti yako itakayoonyesha utofauti..
As long unaargue kwamba sio lazima wanawake wote wa'respond' equally wanapoachwa
Unaweza kuja na tafiti zinazoonyesha hii kitu..
Wakati mwingine haijengi tunapokuwa watu wa ku'critisize' tu bila kuonyesha the other way around..
 
Last edited by a moderator:
Kiranga una matatizo ya uelewa.Labda ni kuambie kwa ufupi,yapo mambo ambayo utafiti wake unawahusu watu wa eneo utafiti uliofanyika tu.Lakini yapo mambo ambayo huhitaji kuzunguka dunia kwa kila mtu,mfano wa hili ni utafiti aliouleta Mtambuzi.Au utafiti wa tiba za madawa hauna haja ya kufanyia majaribio watu wa dunia nzima kwa sababu linawahusu binadamu na binadamu wote wako sawa linapokuja suala la tiba!!!!
 
Mtambuzi ndiye aliyeleta tafiti, mimi sikuleta tafiti.

Ni wajibu wa aliyeleta tafiti kutuonyesha kwamba tafiti zake zinasimama, si wajibu wangu kuonyesha tafiti zake hazisimami.

Hii ni basic rule ya logic of argument. Mleta hoja/ claim ndiye mwenye onus ya kutetea hoja, mpinga hoja anaweza kuipinga hoja kwa challenge ya swali tu. Swali likishindwa kujibiwa kikamilifu hoja inaonekana ina matobo.

Na mpaka sasa si wewe wala Mtambuzi aliyeweza kujibu swali la kwamba mtajustify vipi kutoa figures hizi bila qualification yoyote.

Hoja haijasimama, hatujui kama figures zimetolewa kwenye kofia za watu au hata kama kuna ka research ka uongo na kweli kalifanyika.
 
Kiranga una matatizo ya uelewa.Labda ni kuambie kwa ufupi,yapo mambo ambayo utafiti wake unawahusu watu wa eneo utafiti uliofanyika tu.Lakini yapo mambo ambayo huhitaji kuzunguka dunia kwa kila mtu,mfano wa hili ni utafiti aliouleta Mtambuzi.Au utafiti wa tiba za madawa hauna haja ya kufanyia majaribio watu wa dunia nzima kwa sababu linawahusu binadamu na binadamu wote wako sawa linapokuja suala la tiba!!!!

Utafiti wa madawa unaweza usihitaji kufanyika dunia nzima kwa sababu wataalam wanaweza kujua kwamba madawa yanareact na cells na cells za binadamu dunia nzima ziko sawa, kwa hiyo kwa minajili hii inawezekana kusihitajike regional reserches.

Lakini hili halimaanishi kwamba wanawake wa Silicon Valley ambao baba zao walikuwa Internet billionaires wakapewa uwezo na kuambiwa tangu wadogo kwamba ukitaka kuwa makenika kuwa tu, mwanamke na mwanamme ni sawa, wakaenda kusoma na kuwa wanaanga wasiotaka kuolewa kwa sababu wanathamini zaidi kazi zao, na wanawake wa Msanga-Kisiju ambao tangu wanazaliwa walipigiwa hesabu za mahari na kuonekana hawafai kusoma, populations zao zote ziwe defined na statistic hii ya "wanawake 7 kati ya 10"

Absurd!
 
Zikifanyika tafiti zetu humu tutashangaa..
wanene wenye ma wowowo ndo 'wanaotesa' lol
wembamba ndo unaweza kukuta wana stress za kutopata
'attention' wanayopata wanene lol mpaka wanatafuta dawa za kichina kuongeza shepu..
while Ulaya ni tofauti lol

Umeona eeh?

Halafu mtu eti aje akuletee habari ya copy paste kutoka gazeti la New York City (bila hata ya ku disclose hilo), utafiti unaonyesha watu 7 kati ya kumi wanene wanataka kupunguza miili yao ili kupata wapenzi. Wanasumbuka sana na diet.

Wakati kwetu watu wanatafuta "unene" kwa udi na uvumba! Unene kwetu ni alama ya kujiweza. Ona hapa https://www.jamiiforums.com/jf-doctor/304526-msaada-dawa-ya-kunenepa.html

Ukiwaambia watu ku disclose methodology na sample space muhimu, wanakubishia.
 
Back
Top Bottom