Mahusiano ya Maji ya Uvuguvugu (Moto) na Uzazi wa Watoto wa Kiume | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahusiano ya Maji ya Uvuguvugu (Moto) na Uzazi wa Watoto wa Kiume

Discussion in 'JF Doctor' started by IshaLubuva, Sep 16, 2010.

 1. I

  IshaLubuva JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2010
  Joined: Dec 4, 2008
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kumekuwa na imani kwamba kuogea maji ya vuguvugu hupelekea mwili wa mtu kuzeeka mapema. Juzi usiku Daktari Isack Ndodi alidokeza kwamba mwanamume anayetaka kuzaa mtoto wa kiume anatakiwa kuwa anaogea maji ya vuguvugu kwani akiogea maji ya baridi yanazorotesha mbagu zake zenye uwezo wa kutungisha mimba ya mtoto wa kiume.

  Wadau wenye ufahamu wa masuala haya watupe ukweli wa mambo haya tafadhal.
   
 2. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2010
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  wataalam mko wapi?tupeni majibu mi mwenyewe nahitaji mtoto wa kiume,
   
 3. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  bado nasubiri
   
 4. upele

  upele JF-Expert Member

  #4
  Sep 17, 2010
  Joined: Mar 3, 2010
  Messages: 365
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  doctor ndodi yupo kibiashara zaidi kakuambia nani kuwa maji ya baridi yana zoofisha mbegu huyo maiti anatiwa maji ya baridi kufanya mwili uwe ktk hali yake ya kawaida poleni sana wenye upeo mdogo wakuelewa wa tz sasa biashara matangazo na wajinga huwaga wanafuata angalia mkuu sometimes facky
  Conquest-watz tunaibiwa kiakili au kuzubaa kwetu
   
 5. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2010
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,584
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Hapo pekundu - Hiyo ni imani isiyo sahihi. Thibitisha kiutaalamu kwamba watu wote wa ukanda wa Pwani huzeeka haraka. Maji yao ni ya vuguvugu.

  Hapo pa bluu - Sio kweli kabisa. Wanaume au wanawake kuzaliwa sio function ya temperature ya maji uogayo.

  Umenikumbusha Professor wa Human Sexuality (Jina lake la pili lilikuwa Nagel, nimesahau la kwanza) aliyetoa lecture UDSM around 1979/80 kuhusu kuinfluence kisayansi jinsi (sex) ya mtoto mtarajiwa.

  Kwa ufupi alisema mbegu (atoazo mwanaume) ndizo husababisha mtoto wa kiume au wa kike. Zile za mtoto wa kiume ni fast kutembea (kuingia ukeni na kutafuta yai ili kuungana nalo kuunda mtoto) lakini hazina stamina kubwa - zinakufa haraka. Hivyo kama yai liko tayari wakati wa tendo la ndoa zenyewe zitawahi. Zile za mtoto wa kike ni slow kutembea lakini zinasurvive kwa muda mrefu, hivyo kama yai halipatikani haraka zenyewe, kwa vile zina stamina zaidi, zitafaulu. Hivyo wanandoa wakiujua vizuri kabisa mwenendo wa hedhi wa mwanamke wanaweza kutegea - tendo lifanyike yai likiwa pevu tayari kupata mtoto wa kiume, au tendo liwe kabla ya yai kupevuka kupata mtoto wa kike.

  Sifa za mbegu atoazo mwanaume zilizotajwa juu, na mwenendo wa mzunguko wa hedhi wa mwanamke (na siku anazokuwa katika joto) ndizo huathiri jinsi ya mtoto atakayezaliwa. Hivyo yamkini ya kupanga jinsi ya mtoto ipo mtu akifuatilia na kuzingatia utaalamu huo.

  Sisemi ni kazi rahisi ila kitaalamu, kulingana na usemi wa msomi yule, inawezekana - na mwenye interest lazima awasiliane na wataalamu zaidi kufanikisha uchaguzi wa jinsia ya mtoto kisayansi.
   
Loading...