Mahusiano ya Magufuli na Kikwete (Kweli 9)

The only

JF-Expert Member
May 19, 2011
10,735
14,020
Kabla sijapata mitazamo yenu naomba niziweke kweli hizi :

1. Kikwete hakuwahi kumuandaa wala kujiandaa kuwa kuna siku magufuli angekuwa raisi,nadhani hakuna ubishi kwamba iwapo Kikwete angepewa assignment aweke list ya watu 5 wanaoweza kuwa maraisi mwezi mmoja kabla jina kupendekezwa asingemtaja Anko Magu.

2. Katika kipindi chote cha Jakaya ,Magufuli alikuwa si top 10 ya mawaziri pendwa na JK bali alikuwa analazimika kuteuliwa mosi kwa utendaji wake ,pili kukubalika kwake sana na Wajumbe wa NEC.

3. Mara kwa mara Magu hutamka nchi hii ilifika pabaya ,kauli hii ingefaa sana kama rais angekuwa Mama ngwira tungeeelewa ana-out do JK,Kama tulifika pabaya nani alietufikisha?

4.Utumbuaji wa majipu unagusa zaidi wanachama wa CCM au viongozi wa serikali na taasisi zake,hivyo naweza kusema majipu yanawauma zaidi waliom-support zaidi ,Naamini Home shopping walipigana usiku kucha kuhakikisha manywele haingii na sababu ni walikuwa wanamsaidia rafiki yao JK asidhalilike.Kwa trend hii nilitarajia JPM awalinde kama fadhila na shukran kwa JK na maswahiba zake.

5.Magu aliokota embe chini ya muarobaini,au mbuzi anaefukuzwa alifia jiko la mpika supu,kutokana na msuguano mkali baina ya team lowasa na team JK walijikuta hawana plan B WOTE ,Hivyo team lowassa na team wakongwe (mwinyi,mkapa,...) walijikuta wanaua ndoto za JK za kumweka anaemtaka January or Membe ,wakafanya chaguo la hasira au kukomoa ,team lowassa wakaruka ndege ikiwa hewani wakiwa wameng'oa engine.

Naomba tafakuli yenu sasa kwani kwa haya nashindwa kutoamini kuwa hawa wawili wakijifungia chooni hutukana matusi makali dhidi ya mwenzie ,maana wakiongea una sense unafiki mkali,utamsikia JPM anadai JK amefanya mema mengi ,kesho yake anawatimua waliochaguliwa na JK na kusema watu waligeuza shamba la bibi.
 
Kauli za Magufuli kuanzia kwenye kampeni mpaka alipokua Rais zinaakisi wazi ni jinsi gani hampendi mkwere!!

Bifu ya magu na mkwere ilianza siku nyingi tangu mkwere anapigania kwenda magogoni!! Magu aliongea mbovu kwa Salva kumhusu mkwere!!

Ni Lowassa aliyeshawishi Magu arudi kwenye baraza ila Mkwere hakumtaka kwa kinyongo chake!!!

Magufuli kama alivyo Lowassa si mswahili wala si mnafiki!!

JK na waswahili wengine ni wanafiki wakupitiliza ndio maana ni ngumu kwao kufanikiwa ktk focus zao......
 
Na wakati anayasema hayo JK alikua kashsanatama.huaga naiangalia angalia hiyo video mara kwa mara; halafu kitu cha ajabu Mkapa alikua anatikisha mashavu/kichwa.

Mkapa hata siku ile Lowassa alipokuwa akimpa makavu Kikwete kuhusu Richmond alikua anatabasamu sana hadi pale alipoona Lowassa anaelekea kupindua meza akamwahi kwakusema ajenda izimwe maana aliona JK ameloavilivyo!!!
 
ha ha ha ccm itatawala milele nchi hii kama akili zetu zinawaza hivi... ccm ndio tanzania na tanzania ndio ccm. ona walichofanywa cuf zanzibar.. rais anajifanya hausiki.. mwenyekiti nae yupo majuu anasuluhisha wa libya.. ukawa wametoa macho watu shein wameshamwapisha....

hivi nani asiyejua kama jk aliingia na majina matano mfukoni na kuyapitisha kibabe.... tena utaratibu hakuufuta..

na magufuli ni mojawapo ya majina matano Jk aliyoyatoa mfukoni mwake...

katika watu 40,, mtu awaache watu 35 wote na azame kikaoni na majina 5 tu ya watu asiowapenda kweli...

Jk amekata watu wote 35 asiowataka tena kibabe..

na hata magufuli asingemtaka asingeshindwa kumkata nae..

kakatwa lowassa, jaji ramadhani, mwandosya,, makongoro nyerere jina kubwa... why ashindwe kumkata magufuli??
 
Napataga shida sana kuwajua marafiki halisi wa JK walikua kina nani?
 
Wanajua wenyewe sie mradi mambo yanaenda walijua mungu mdhungu watu huwa wanajisahau hilo ninachokumbuka kwa magufuri alilikumbuka hilo kila alipokanyaga aliwataka watu wamuombe mungu si mwaruka ndala ndefu Kati ya watu mia watano akawasikia coz alijua alipitaje pale wengine waliona umaarufu pesa zao kuzungusha mikono wakasahau kama kuna mungu ila ishallah
 
ha ha ha ccm itatawala milele nchi hii kama akili zetu zinawaza hivi... ccm ndio tanzania na tanzania ndio ccm. ona walichofanywa cuf zanzibar.. rais anajifanya hausiki.. mwenyekiti nae yupo majuu anasuluhisha wa libya.. ukawa wametoa macho watu shein wameshamwapisha....

hivi nani asiyejua kama jk aliingia na majina matano mfukoni na kuyapitisha kibabe.... tena utaratibu hakuufuta..

na magufuli ni mojawapo ya majina matano Jk aliyoyatoa mfukoni mwake...

katika watu 40,, mtu awaache watu 35 wote na azame kikaoni na majina 5 tu ya watu asiowapenda kweli...

Jk amekata watu wote 35 asiowataka tena kibabe..

na hata magufuli asingemtaka asingeshindwa kumkata nae..

kakatwa lowassa, jaji ramadhani, mwandosya,, makongoro nyerere jina kubwa... why ashindwe kumkata magufuli??
Usidanganye wewe kama hujui sema usaidiwe! Haya majina matano hayakuwa choice ya Jk tu bali kamati kuu ya chama (CC) akiwamo mzee la kiburi ben pamoja na mzee wa ruksa n.k. Hata magufuli aliwekwa kimkakati na ben maana ni kijana wake tangu zamani na anamjua vyema. Hao akina January, Membe n.k walikubaliwa kuwekwa ili kumfurahisha tu J.K lakini wenye uzoefu na hzi issue (ze la kiburi) na wenzake walikuwa wanajua ni nini wanafanya! Pia Magufuli ashukuru sana team lowasa vinginevyo hata yeye asingefurukuta kwenye mkutano mkuu maana team lowasa walipiga kura za hasira kumkataa Membe wa J.K
 
mambo ya SIZONJE....ila nyumba yetu ina vyumba vinne vitatu havifunguki(mikataba) ili SIZONJE ni msifie avunje hivyo vyumba ambavyo havifunguki kwanza aanze na hapo
 
Back
Top Bottom