Mahusiano ya Kodi na Hali ya Uchumi kwa Wananchi

Joema the king

New Member
Jul 16, 2021
1
0
Lazima kuwe na MAHUSIANO kati ya gharama za Kodi na uchumi wa WANANCHI kwa taifa lolote nyingi.

Haiwezekani kuwe na Taifa linye Kodi kubwa kuliko uchumi wa mmoja mmoja kwenye hilo Taifa ndio maana TAIFA lenye Kodi nyingi ni mataifa ambayo kipato Cha mmoja mmoja katika Hilo taifa NI kikubwa.

Mpaka leo hii TAIFA LA Tanzania mishahara ya wafanyakazi ina changamoto yakuongezeka kulingana na kanuni zao
Pia wafanyabiashara Wana changamoto nyingi juu ya masoko ya biashara wanazofanya.

Sasa basi kabla ya SERIKALI hawajaamua kuongeza Kodi za maendeleo lazima wafanye tathmini juu kipato Cha mmoja mmoja ili watambue wanamsaidia vipi katika RISONG OF STANDARD OF LIVING

TAIFA letu la Tanzania limekuwa likipata mikopo kutoka nchi za nje kwa ajili ya kutengeneza miundombinu kwa WATANZANIA ya kujiongezea vipato vyao Kama miundombinu ya barabara ,ndege,baharini kuongeza viwanda vitavyozidi kuwapa ajira na pia serikali kujipatia KODI.

TATIZO LINAKUJA MIRADI YA KISERIKALI KWA JICHO LA KAWAIDA BADO haijaanza kuleta pesa kwa WANANCHI Kama masoko yaliyojengwa bado hajaanza kufanyiwa biashara miradi mikubwa ya kitaifa bado haijamalizika lakini chakushangaza ONGEZEKO LA KODI LIMEANZA kwa kiasi JE KWA NCHI KUNA MAHUSIANO KWELI YA KODI NA UCHUMI WA WATANZANIA?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom