Mahusiano ya kimapenzi, uchumba na ndoa yanahusiana sana na umri kuliko kipato

BioPsychologist

JF-Expert Member
Aug 23, 2017
724
1,014
Hello JF members, nawasalimu wote!!!

Kwanza nitoe pongezi kwa wazee, babu bibi na baba na mama zetu hapo kale walioa na kuolewa kwa mda muafaka regardless kipato chao kama leo tunavyohubili kuwa mapenzi bila pesa hayaendi,,,mmhh oky!!!

Karibu

KATIKA KUPENDA KUSOMA SANA VITABU MBALI MBALI VYA SAIKOLOJIA, UCHUMI NA MAHUSIANO, NILIKUTANA NA ANDIKO MOJA LA REACH ADVISORS 2012 ANASEMA HIVI;

Katika majiji (Cities) mengi sana duniani wanawake single kati ya miaka 22-30 wanamiliki kipato (pesa) kubwa zaidi ya wanaume single wa umri huo huo wa 22-30, hii ni kutokana na wanawake au wasichana kupata vipaumbele kutoka katika wale wanao wategemea na wana nguvu ya ushawishi wa kiuchumi kuliko wavulana, kitu ambacho huwafanya kupata kazi kirahisi, kusaidiwa na familia kirahisi, kupewa pesa nyingi na wapenzi wao n.k mambo haya yote huwafanya asilimia kubwa ya wasichana kuishi maisha mazuri na kuwa na kipato kikubwa zaidi.```

NILICHOJIFUNZA NA KUKIONA HATA HAPA KWETU TZ HASA NDANI YA JIJI LA DAR ES SALAAM, ARUSHA NA MWANZA KWA UCHACHE NI HIKI HAPA

```Kutokana na nature (asili) ya wanawake na wanaume katika kugawana majukumu hutokea Mara nyingi wasichana hawa licha ya kufikisha umri wa kuolewa bado huitaji kutafuta (wanaume wenye pesa) wanaowazidi kipato kwa maana kuwa hawafikilii kama wanaweza kutumia pesa zao kuanzisha familia ikawa bora bali wanafahamu na kukariri kuwa majukumu ni ya wanaume pekee na pesa ya mwanamke ni ya matumizi yake binafsi, wakati huohuo vijana wa kiume nao huofia kuanzisha mahusiano na wasichana hao kwa sababu ya kuogopa kuonekana wadhaifu mbele yao na kudhani watapoteza SIFA za uanaume WAO

Hali hii imepelekea wasichana wengi wa umri tajwa kuwa single kwa mda mrefu na wanapochoka kuwa single baada ya miaka 30 huwa tayari kuolewa na watu wa aina yeyote mfano; mzee au kijana wa umri mdogo zaidi, vijana wa kiume pia huvuta miaka yao sana wakati wakitafuta maisha na pale mambo yanapokuwa magumu huwa tayari kuoa au kutunzwa na sugar momy.```

MATOKEO YAKE

1. Kwa mabinti wa kike wa umri wa 22-30 huwa wanapata sana approach za kimapenzi kutoka kwa men wengi lakini kukosa utulivu au kupungukiwa uwezo wa kumjua mkweli hujikuta wanachezewa sana.na wanaume kwenye umri huu,lakin pia ni umri wa kugeuza dunia afanye atakavyo kitu ambacho huwafanya wajisahau kuwa cell zinazeeka kidogo kidogo, miaka 30+ bila kuolewa sio dhambi lakini jiulize kati ya wote uliowahi kuwa nao kimahusiano hawakufaa kuwa wanaume wa kuoa ?

2. Kijana wa kiume una jukumu kubwa sana la kujikwamua maana utaitwa baba Fulani mda sio mrefu, umezaliwa kupambana hivyo endelea kutafuta maana hutaheshimiwa kama huwezi kutimiza majukumu yako ipasavyo ,changamoto za AJIRA zipo kila mahali usife moyo na kuanza kutapatapa kutafuta JIMAMA wa kukulea japo sio dhambi lakini kumbuka utaishi maisha ya kifungo cha nje hadi lini ?

KUNA HAJA YA LAZIMA YA KUJITAMBUA KUTOKANA NA UMRI ULIONAYO,KAMA UNAKUMBUKA KUSHEREHEKEA HAPPY BIRTHDAY KUMBUKA NA KUHESABU MAFANIKIO YA MAISHA YAKO NA WEWE BINAFSI KATIKA UMRI HUO IKIWEMO FAMILIA

Nakaribisha mtazamo tofauti,nyongeza au maoni !!!!
 
mwanaume aliyekamilika kila idara....wanawake hawajui walipo, wana vigezo vyao wanavyojua wenyewe na mwisho wa siku anajikuta ana 35 yupo yupo tu, watu wanachapa wanasepa,...
 
mwanaume aliyekamilika kila idara....wanawake hawajui walipo, wana vigezo vyao wanavyojua wenyewe na mwisho wa siku anajikuta ana 35 yupo yupo tu, watu wanachapa wanasepa,...
Wana sema haina haja ya HARAKA kuolewa wanakula kwanza usichana hapa huwa hawajui kuwa kuna majukumu ya kuja kuwa mama na wanaume wana angalia umri pia?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom