SoC01 Mahusiano ya fikra na ubunifu kwa vijana

Stories of Change - 2021 Competition

Waja k

New Member
Aug 8, 2021
1
1
Kuna sehemu niliona pameandikwa kwa lugha ya kiingereza
“Start with mindset”
-Anza na fikra-

Fikra ni namna unavyochukulia jambo, au ni mawazo ya mtu juu ya jambo fulani maishani au juu ya maisha kwa ujumla, fikra ni dhana.
Fikra na umasikini au utajiri vinaenda sambamba sana. Lakini lazima tujue nini chanzo cha fikra hizo. Fikra chanya au hasi zinaweza kua ni HURKA ya mtu, au zinaweza kusababishwa na SAIKOLOJIA au MAZINGIRA anayoishi muhusika.
Ukiachia mbali hurka, sababu kubwa nyingine za kujenga au kubomoa fikra ya kijana ni SAIKOLOJIA au MAZINGIRA anayoishi, vitu hivyo viwili vina nafasi kubwa sana kwenye kumjenga au kumbomoa kijana katika nyanja zote za maisha, na hasa kiuchumi.
Kabla ya kuangalia hurka, mazingira na saikolojia ngoja tuangalie ubunifu ni nini na athari zake chanya kwenye maendeleo ya kijna mwenyewe, jamii yake na taifa kwa ujumla.

UBUNIFU
Hii ndio injini ya utajiri na mafanikio kwa ujumla ambayo watu wengi hawaijui au hawaitambui, ubunifu ndio ujasiriamali wenywe, ubunifu unahusisha kuunda na kuzalisha mawazo (njia za kutatua matatizo), bidhaa na huduma mpya zitakazoweza kuingiza kipato.

Ubunifu ninaouongelea hata ujikite katika kutatua matatizo kuanzia yaliyopo kwenye jamii zetu mpaka ngazi ya taifa na hata kimataifa (pesa zitakuja tu)
Ubunifu uwepo kuanzia kwa mwajiriwa na mwenye kujiajiri, kifupi vijana wanapaswa kuongeza thamani kwenye kila wanalolifanya.
Ubunifu ujikite kote kwenye mambo mapya na hata yale ambayo sio mapya(kuongeza pale walipoishia wengine)
Ubunifu ukifanywa kikamilifu utaondoa matizo mengi ya vijana , jamii na hata taifa kwa ujumla

  • Kwa kijana mwenyewe ubunifu utampa ajira bila mtaji, pesa ya matumizi kisha utajiri wa hali ya juu mfano Mark na Facebook na wengine wengi
  • Kwa jamii; Ubunifu hujikita kwenye kubuni bidhaa mpya kisha bidhaa iliyobuniwa inaenda kutatua tatizo moja kwa moja mfano simu (mawasiriano), mashine za kutengeneza juice (lishe), sabuni (afya) nakadharika.
  • Ubunifu hurahisisha kazi kupitia uundwaji wa njia mbadala za utekelezaji wa majukumu ya kila siku mfano teknolojia ya mawasiriano, utunzaji taarifa, mtiririko wa majukumu, mifumo ya afya, mifumo ya elimu nakadharika.
  • Kwa taifa ubunfu ndio unaopelekea uwepo wa biashara hivyo ukusanyaji wa kodi, ushuru na upatikanaji wa ajira ni matunda ya moja kwa moja ya ubunifu kwa taifa.
Sasa tuangalia zile sababu tatu zinazompelekea kijana kua na fikra hasi au chanya kwenye maisha yake

HURKA

Kuna vijana au watu ambao wao hata ufanyaje hawana mpango wala mkakati wa kua na aina ya maisha ambayo wengi tunaamini kua ndio maisha bora.

Hawajakata tamaa wala hawana tatizo lolote isipokua wameridhika na namna wanavyoishi. Wapo hivyo leo na watakua hivyo kesho, kifupi hawana wanachokitafuta.

Watu wa aina hii ni ngumu kubadilika mpaka pale wao bifsi watakapoanza kuyatazama maisha kwa jicho la utofauti. Muda pekee ndio sababu inayoweza kumbadilisha fikra mtu wa namna hii

MAZINGIRA
Mazingira ni vitu vyote vinavyotuzunguka, mazingira ndio chakula, elimu na vitendea kazi, vijana wengi wa Tanzania na nchi nyingine ambazo hazijaendelea wamezunguukwa na mazingira mengi magumu yakiwemo

Miundombinu mibovu; haya huathiri harakati za kujikwamua katika Nyanja za usafirishaji, mawasiriano, na technolojia . Ubovu wa miundombinu hii huathiri moja kwa moja fikra za ubunifu kupitia kuonzeka kwa gharama za shughuri mbalimbali za kibunifu mfano adha ya intaneti na ubunifu wa application mbalimbali.

Familia na wazazi; hawa ndio waalimu wa kwnza kwa mtoto au kijana yeyote, hivyo wananafasi kubwa ya kumjenga au kumbomoa. Wazazi ndio wanaomfanya kijana awe na uwezo wa kujiamini, kwa kumfundindisha maadili , bidii na uwezo wa kufanya yanayofaa katika kujihudumia na kuihudumia jamii. Wazazi wanapaswa kuwapa vijana wao uhuru wa kufanya chochote ili mradi kiwe cha halali, hili litaongeza ubunifu kupitia kanuni ya trial and error

Elimu na mifumo ya elimu; hili ndilo eneo mhimu katiaka malezi na makuzi ya kijana au mtoto, hapa kijana anajifunza mahusiano na watu, kile anachotarajia kufanyia kazi na maarifa mapya kuputia historia au mifano iliyo hai.

Elimu ndio inampa kijana uelekeo wake baada kwani anachojifunza leo kijana ni dhahiri kitatambulisha atakachokua akikifanya kesho. Hivyo somo la utafiti, ubunifu na kujitegemea ni muhimu sana kwa ngazi zote.

Kama elimu haitajikita kufundisha utafiti na ubunifu basi upo uwezekano wa kua na wahitimu wasio na uwezo wa kufikiria njia mbadala za utatuzi wa changamoto zinazowakabiri ikiwemo ajira.

Afya na chakula au lishe; tukiondoa imani ya uwepo wa mungu na neema zake, uhai wa mtu hutegemea afya yake, chakula na lishe bora humfanya mtu awe imara kiakiri na kimwili. Ripoti za watu kukosa mlo kamili zimekua zikiripotiwa kwenye baadhi ya maeneo kama Makete mkoani Njobe, hili linaweza kuleta udumavu wa akili (fikra) na mwili. Afya yenye mgogoro huleta hofu na wasiwasi kwa mwanadamu yeyote, usipojiamini hauwezi kukamilisha chochote ikiwemo utafiti na ubunifu.

Utawala; hili ndilo eneo linalobeba familia na jamii, sera kuhusu afya, elimu na vinginevyo hutungwa. Selikari ndio kichocheo cha kukuza au kudumaza vijana na watu wake kupitia sera na muongozo wake kuhusu elimu, afya , michezo na kadharika.

SAIKOLOJIA
Utimamu wa akili, hapa kuna kitu hua nakiangali sana, mfano kuna kitu kinaitwa vicious cycle of poverty, mtu toka azaliwe hajawahi kua na nafuu ya maisha; hii inamfanya aathirike kifikra inampotezea kujiamini katika kufikiri, na kuwasirisha mawazo yake. Matokeo ya mwisho ya hili ni kuharibika kwa uwezo wa kujifunza na mwishowe hawezi kufanya chochote cha tofauti katika jamii yake.

HITIMISHO
Ukiachilia mbali fikra kijana anahitaji mambo mengi ya msingi ili aweze kufanikiwa yeye binafsi, jamii yake na taifa kwa ujumla. Binafsi kama kijana, anahitaji muunganiko wa mambo yafuatayo

Nia-uthubutu, kujiamini na utayari
Elimu- kujifunza vitu vipya na vya zamani kila siku
Ubunifu-kutafuta njia mpya na nzuri za kutatua matizo yalipo kwenye jamii
Bidii na usimamizi sahihi wa kile anachokifanya, apende anachokifanya, awe na bidii bila kukata tamaa
Nidhamu, hakuna mafanikio bila nidhamu ya kipato unachokipata, kuheshimu kazi na muda wako kila siku.

Asanteeni naomba kuwasilisha
 
Back
Top Bottom