Mahusiano ndani ya ndoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahusiano ndani ya ndoa

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pdidy, Jun 3, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  Jambo linalohuzunisha ni kwamba nusu ya mwanaume na mwanamke wanaoamua kuishi pamoja hushindwa kufikia hii hatua ambayo mateso, maumivu, uchungu na kuvumilia kote huanza kulipa.

  Asilimia kubwa ya ndoa zinazovunjika sababu kubwa ni kukosa maarifa (knowledge) hasa kabla ya wawili kuamua kuishi pamoja hivyo huingia kwenye ndoa wakitegemea ndoa itakuwa tambarare kama nyikani au watakutana na vichuguu kumbe kuna milima na mashimo.

  Hapa mnakuwa mmeshirikiana kutengeneza historia na kwa pamoja mnakubaliana kwamba kweli ndoa haikuwa rahisi hata hivyo mnajisikia proud kwa kuwa mmeshinda hurricanes na storms zote pamoja.

  Kila mmoja anamshukuru mwenzake kwa commitment kubwa na dedication aliyoiweka kuhakikisha ndoa inafika mwisho kwa uvumilivu wa hali ya juu, pia mkiangalia mlikotoa mnajisikia ni kweli ninyi ni wanandoa wa tofauti.
  Kila mmoja anajiskia yupo karibu na mwenzi wake na more connected kimwili, kihisia na kiroho, pia kila mmoja hujisikia amepata hamu mpya na kubwa kwa mwenzi wake hasa Kutokana na kupoteza muda mwingi wa kuwa intimate kwa kushughulikia migogoro kila mmoja anajiskia yupo nyumbani tena.

  Hujikuta zile qualities ambazo uliziona mwanzo kabisa kumbe bado anazo na unaanza kujiunganisha kihisia upya kwa kuwa sasa mnafahamiana vizuri pande zote za maisha yaani strength na weakness.
  Hii ni hatua ya furaha, hatua ya mapenzi ya kweli, true love, divine love, unconditional love.

  Wanandoa wa hatua hii hata watu wengine huwa-admire kutokana na jinsi walivyoshinda aina zote za majaribu.
  Wanakuwa role model kwa jamii.

  Kama wanandoa wote wangejua kwamba ndoa huwa katika hatua mbali mbali na kwamba mbele ya safari inalipa, basi wangekuwa tough kuhakikisha wanavumilia na kushinda.

  Hata hivyo wengi huamini stage (kama kuna matatizo) waliyopo itakuwa ya kudumu na kwamba watakuwa hapo forever, ni kweli ukiwa na wakati mgumu huumiza na hukatisha tama lakini kumbuka “No situation is permanent” hata kama ndoa imefikia hali mbaya kabisa bado huwa na dalili za kuiokoa ni muhimu kuelekeza nguvu hapo.

  Ndoa imara si ile isiyokutana na dhoruba bali ni ndoa ambayo inazishinda aina zote na dhoruba nakuendelea mbele kwa kasi ya ajabu.

  NB:
  Si lazima ndoa yako ipitie hatua zote 4 unaweza kuwa kwenye hatua ya kwanza miaka yako yote huku kukiwa na vimsuguano vidogo vidogo kama utaruhusu Kristo kuwa kiongozi wa ndoa yako kwani kama yeye anavyolipenda kanisa basi mume na mke wanahitaji kuishi kwa mfano wa Kristo na kanisa.
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  Kila mmoja anajua raha ya falling in love or siku za honeymoon je, nini hufuata baada ya hayo?
  Wengi hawajui emotional terrain iliyo mbele, au hills zilipo mbele au bonde utakayopita katika kuendelea na ndoa yako.
  Hapa kuna hatua predictable ambazo ndoa nyingi hupita, naamini ukiijua hii ramani basi utaweza kufika mahali unapoenda.
  Leo tunaendelea na hatua ya pili na ya tatu

  HATUA YA PILI NI MAUZAUZA
  (Nilikuwa nawaza nini)
  Ile hali ya kudondokea kwenye mapenzi (fall in love) huchakaa na ukweli halisi huanza kuonekana.
  Hii ni hatua ngumu kwa sababu unakumbana na anguko kubwa sana la ndoto zako kuhusiana na mpenzi wako.
  Zile tofauti na tumakosa tudogo ambato tulikuwa si kitu sasa huanza kusumbua na kuudhi, mfano kama mwenzi wako alikuwa mzembe kupanga vitu hasa nguo chumbani sasa utaanza kuudhika kwani utajisikia umevulia mno, kama anakoroma sasa utaona usumbufu, kama ana kikwapa sasa unaona kinasumbua, kama ana harufu mbaya mdomoni asubuhi itaanza kukusumbua, tayari sasa vitu vidogo vimekuwa mambo makubwa yanayokuudhi.

  Kila mmoja huanza kulalamika kwamba mwenzake hawi kama anavyotegemea.
  Kunakuwa na disagreement nyingi kuliko agreement na unagundua kwamba mnatofautiana sana katika mitazamo ya vitu vingi.
  Wewe unataka kula hotel unaipenda mwenzako anataka mle nyumbani ili ku save pesa, unapenda usikivu usiku nyumbani mwenzako anataka kusikiliza muziku kwa sauti kubwa.

  Ule kuwa mwenzi wangu ni perfect huanza kupotea na imani yako kwake huanza kupotea kwamba mmm kumbe ni mkali kiasi hiki, kumbe ni mchoyo kiasi hiki, kumbe hapendi sex kiasi hiki, kumbe anajua kukalia mwenzake kiasi hiki nk.
  Hapa tofauti za malezi, tamaduni, dini, kuamini, tofauti kati ya mwanamke na mwanaume hujitokeza na kuwa wazi.
  Katika hatua hii mtu halisi huanza kuonekana na ukweli ni kwamba ndoa huanza kujengwa hapa.
  Wengi huanza kujiuliza mbona watu hawakuniambia kwamba ukioa au kutolewa inakuwa hivi kwani anayaanza kuona ni kinyume na matarajio na wengine huanza kujiuliza kwa nini nilioana naye.
  Wapo ambao huanza kufikiria wachumba wengine (misri) kwamba labda ningeoana na Fulani alikuwa afadhari kuliko huyu.
  Wengi huanza kujiuliza hivi nilikuwa nafikiria nini hadi nikakubali kuoana naye.
  Walio na hekima huanza kumuomba Mungu na kupata ushauri wa watu wanaowaamini

  HATUA YA TATU NI MATESO, MAJONZI NA TABU
  (Miserable stage)
  Wanandoa hushangaana kwa nini kila mmoja amejiweka gundi kwenye njia zake bila kumjali mwenzake.
  Na kila mmoja humwambia mwenzake ungebadilika kila kitu kingekuwa kizuri.
  Kama ni mlevi basi hujichimbia mizizi na kuwa mlevi wa kupindukia, kama ni mlevi wa kazi (workaholic) basi ataondoka nyumbani asubuhi na mapema na kurudi midnight eti ana andaa future.
  Hata akirudi nyumbani hukuta mke amelala na watoto wamelala na yeye mwenyewe yupo exhausted kiasi kwamba hawezi hata kumuhudumia mkewe.
  Hapa ndipo affair nyingi huzaliwa, na ndoa huwa ni vilio, majonzi, Stress, BP, pressure, kukosa usingizi, you name it!
  Wanasheria wa mambo ya ndoa wengi hutajirika kwenye hatua hii ya ndoa hasa nchi zilizoendelea ambako kuachana ni jambo la kawaida tu (divorce)

  Watoto wengi huachwa njia panda na kutojua nini cha kufanya maana mara kwa mara baba na mama hawaelewani.
  Hapa ndipo tunafahamu kwamba kupigiana kelele, kulaumiana, kusuguana, kutishiana hakuwezi kubadilisha wapenzi wetu bali kukubaliana kwamba kuna tofauti na kushirikiana kutatua tatizo kwa hekima na busara hupeleka ndoa kwenda hatua nzuri zaidi.

  Hii ni discovery stage ambayo wanandoa hujuana na ni opportunity ya kujifunza na kuzalisha true love.
  Wale wanaokimbia au kuomba talaka au kutoa talaka huenda kutafuta wapenzi wapya ambao hujikuta wameangukia the same boat na matatizo mapya na makubwa zaidi.

  Na ndoa nyingi huvunjika hapa na kukosa kufikia stage inayofuata ambayo ni true love kati ya wanandoa.
  Ndiyo maana tafiti nyingi zinaonesha kwamba baadhi ya walioachana kwa talaka kuna wakati hutamani kurudiana na wataliki wao au wangejitahidi kuvumilia na hatimaye kutatua matatizo kuliko njia ya kupeana talaka waliochukua.

  Wapo ambao huona haina haja kuendelea na hii cold war na huamua kuchukua uamuzi wa kufanya investigation na kuchukua njia sahihi za kujenga mahusiano imara na yenye afya.
  Hata hivyo wanaoamua kuchukua huu uamuzi bora wa imani huwa na milima na mabonde ya kupita kufikia hatua ya mwisho ambayo huwapa raha na experience ya ndoa mpya.
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  Ndoa ni mahusiano yanayoweza na yanayotakiwa kuwa ndiyo kitu kinacholeta raha na kuridhisha katika maisha kuliko kitu chochote.
  Tafiti nyingi zinaonesha kwamba watu walio kwenye ndoa huishi maisha marefu kuliko singles (sina maana kutaka kukuumiza kwa sababu wewe ni single au ukimbilie kuolewa au kuoa ili uishi miaka mingi, be carefull unaweza kufupisha maisha huo ni utafiti tu na si lengo kuongelea mtu kuwa single)

  Kwa kuwa nusu ya ndoa zinazofungwa huvunjika katika baadhi ya nchi, ni muhimu sana kufahamu vizuri package nzima ya mambo ya ndoa katika pande zote.
  Knowledge is power!

  Pia ni vizuri kukumbuka kwamba (kama hujaolewa au kuoa bado) yale unakutana nayo muda wote wa uchumba hadi honeymoon (unaweza kuwa na honeymoon ya siku kadhaa au miezi kadhaa au mwaka) ni asilimia 10 tu ya masuala ya ndoa na asilimia 90 ni kazi iliyo mbele yako na hii kazi itakupasa kuendelea kuifanya siku zote unavyoendelea na ndoa.
  HATUA YA KWANZA NI KUDONDOKEA KWENYE MAPENZI
  (Infatuation)

  Kibailojia kuna asili ambayo miili yetu huwa msingi katika hatua mbalimbali ambazo hutufanya kuvutiwa na mtu wa jinsia nyingine na kufika hatua tukaona maisha bila huyo mtu hayana maana.
  Kuna aina tatu za kemikali (Phenylethylamine, dopamine na norepinephrine ) ambazo huhusika moja kwa moja na kuwafanya wawili wapendanao kwa mara ya kwanza kujikuta wamedondoka kwenye mapenzi (fall in love).

  Kwa pamoja hizi kemikali huweza kuzalisha na kutibua matokeo ya kushangaza hadi mtu kuwa na positive attitude na anayempenda, piga ua hukubali kumuacha maana umempenda, watasema usiku watalala kwani nimempata anayenipenda.
  Hizi kemikali hutufanya kuwa na nguvu kubwa ya kumpenda mtu na kujisikia tunajisikia very excited na mpenzi mpya.

  Hizi kemikali kama nguvu ya hurricane au storm huweza kuufunika ubongo (amygdale) sehemu inayohusika na kutoa tahadhari.
  Amygdale huweza kutoa tahadhari au onyo kwamba partner uliyempata anaweza kukuumiza hata hivyo kutokana nguvu iliyopo ya falling in love mhusika hupuuzia.

  Mhusika hajui kuonywa ni kitu gani, haogopi watu wanavyosema maana yeye amependa, yupo blind.

  Wengi huangukia kwa wapenzi wasiowajua vizuri na hujishangaa kwa nini wanawapenda kwa kasi ya ajabu kiasi hicho.
  Kuna powerful attraction kiasi kwamba huweza kusababisha hadi mtu kutoa maamuzi ya ajabu kama vile kukana dini, kukana wazazi kukana ndugu na kukubaliana na huyo amempenda.
  Katika hatua hii ya mahusiano wengi hujiona wamefikia na kutimiza ndoto zao.
  Kila kitu huwezekana na kukufanya uridhike maana mpenzi anakupa kile unakihitaji amabcho hata wazazi hawawezi kukupa.

  Ni hatua natural ambayo mke na mume huvutiana na hupelekea kuoana
  Katika hii hatua maisha ni matamu, ahadi kubwa na kedekede kutolewa,
  I miss u,
  I love u,
  You are mine,
  I love u from earth to the moon,
  Nakupenda kwa moyo wangu wote,
  Sina mwingine ila wewe tu.
  Wakiwa wamelala hukumbatiana kama vile amelala mtu mmoja (mwili mmoja) ni raha ni kuhitajiana kwa kiu ya ajabu.
  Wahusika huwa blind na hata kama mwingine ana makosa au vitu fulani anaudhi huonekana si tatizo, na hukubaliana kuoana hivyo hivyo.

  Watafiti wengi wanauona huu upendo katika hatua ya kwanza si upendo wa kweli (not true love) kwani huongozwa na hizo kemikali tatu na kukupa nguvu za attraction za ajabu. Pia haujajaribiwa bado, haujakumbuna na kasheshe bado.

  Hii hatua katika mahusiano ya ndoa huitwa hatua ya ghururi (infatuation, self deceit, arrogance, presumption)

  Hapa ndipo kunapatika vitu vinaitwa uchumba na honeymoon
  Hii natua huweza kudumu hadi miezi 30 muda ambayo hutosha wahusika kuwa na mtoto.

  Je, ni hatua zipi hufuata na kupelekea wanandoa kuwa na true love?
  Je, mahusiano mengi au ndoa nyingi huvunjika katika hatua ipi?
  Na je, ni jambo gani la busara kufanya katika hatua ambayo ndoa nyingi huangukia kwenye shimo?

  Tutaendelea
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  Kukumbatia, kubusu, kushikana mikono na sex (ktk ndoa) ni njia ya mawasiliano ya hisia za upendo au kupendwa.
  Watafiti wengi hasa wa maendeleo ya watoto wamethibitisha kwamba kukumbatia, kumbusu na kumshika mtoto kunampa afya njema kihisia.
  Kuguswa ni kitu muhimu sana katika mawasiliano ya ndoa hasa linapokuja suala la mahaba, kwa kushikana mikono, kubusu, kukumbatiana na kutekenyana kule kunakonyegesha huleta raha sana kwa mke na mume.

  Inawezekana mume wako au mke wako kwake kupendwa ni kukumbatiwa au kupata busu kabla hujaondoka asubuhi na unapokutana naye tena baada ya shughuli za kujenga familia au kutembea mmeshikana naye mikono, pia inawezekana kwako ni jambo gumu na unaona kama ushamba fulani hivi au ulimbukeni.
  Jambo la msingi fahamu kwamba kila mmoja wetu ana aina ya kujisikia anapendwa na ni kitu kidogo lakini kinaweza kufanya ndoa au mahusiano yako kuwa matamu au machungu.

  Unaweza kutumia muda mwingi kumpikia chakula kitamu, au kununulia mizawadi ya gharama, hata hivyo kama mwenzi wako kupendwa ni kupokea mguso wa kimwili bado zawadi zako hazitamkuna vizuri kama ungempa mguso wa kimwili.
  Ktk milango ya mitano fahamu, kugusa ndiyo peke yake kunahusisha mwili mzima ingawa kuna sehemu zingine zikiguswa ni balaa zaidi na zinahusisha watu walio katika ndoa tu.
  Kuona tunatumia macho, kunusa tunatumia pua, kusikia tunatumia masikio, kuonja tunatumia ulimi lakini kugusa ni mwili mzima.

  Sex ni physical touch, ndiyo maana kuna wanawake au wanaume bila kumpa sex anaona bado humpendi hata kama utamnunulia gari au kumpeleka vacation North pole hata hivyo hapa tunazungumzia sex ndani ya ndoa na si vinginevyo.
  Mwili ni kwa ajili ya kuguswa,
  Unaonaje mtu akigoma kukusalimia mikononi?
  Naamini utatambua kwamba kuna mushkeli.Inawezekana mume wako au mke wako kupata mguso wa mwili ni lugha yake ya msingi kuonesha unampenda na anategemea utamgusa mwili wake kila siku kwa kutekenya nywele zake, au kutembea umemshika mkono au kumpa busu na kumkumbatia kila unapoondoka home asubuhi au unaporudi na pia kumpa romance ya uhakika kabla ya sex mkiwa faragha,

  KUSAIDIANA KAZI
  Hii ni kufanya vitu ambavyo mke wako au mume wako anatarajia au anategemea ungefanya kuonesha unampenda na kumjali na kuwa wewe na yeye ni kitu kimoja.

  Inawezekana anategemea ungemsaidia kutandika kitanda, kusafisha nyumba, kupika, kufua nguo, kumsafisha mtoto, kuosha gari, kufyeka majani nk hiyo mnaweza kufanya pamoja na ni njia nzuri ya kueleza kwamba unampenda kwa vitendo.
  Tatizo linakuja kutokana na jamii zetu za kitanzania asilimia kubwa ya familia zetu ni extended, hivyo kwa mfano baba akiamka asubuhi na kuanza kufanya usafi wa nyumba au kupika au kufua nguo za wife nahisi hata majirani wataandamana kuuliza kulikoni kwani yawezekana hapo kwako kuna timu ya watu kutoka kijijini au ndugu zako kama dada, kaka, shemeji, wajomba, baba mdogo, ndugu wa shangazi zako au wafanyakazi ulionao kama house girl, house boy na wale wageni waliokuja kutoka kijijini bila kukupa taarifa nahisi watashangaa.

  Point hapa ni wewe kumsaidia mwenzi wako kazi hasa mwenzi ambaye kwake kupendwa ni kusaidiana kazi.

  MANENO YA SIFA
  (Kusifia, kutia moyo na kushukuru)
  Je ni mara ngapi umesema Asante au kumsifia spouse wako kwa jinsi alivyofaanya kitu ambacho kilionekana kizuri?
  Na je kawaida unapomsifia au ku-appreciate vitu anafanya huwa anajisikiaje?
  Hayo maswali ni ya msingi sana mtu kujiuliza hasa kama unataka kujua mwenzi wako kwake maneno matamu ndiyo KUPENDWA.
  Maneno mazuri au yanayotia moyo au yanayomsifia ambayo ni matamu husababisha mambo yafuatayo kwa mwenzi wakoHuleta upamoja na ukaribu zaidi (intimacy)Huleta uponyaji kwenye majeraha ya hisia zake kama kuna maumivu moyoni mwake (healing) na kumfarijiMwenzi hujisikia kulindwa zaidi na anajisikia yupo katika mikono salama.

  Fahamu kwamba wewe ndiye mtu muhimu kuliko mtu yeyote duniani kwake, hivyo maneno unayoongea either yanamjenga au yanambomoa na si kubomoa tu bali na kumuumiza na unampa wakati mgumu.
  Lengo la upendo si kulalamika kwa kile ambacho hupati
  bali ni kufanya kile ambacho kitamsaidia yule unayempenda,
  yule umechagua uishi naye hadi kifo kitakapowatenganisha.

  Mojawapo la hitaji kuu la ndani la mwanadamu ni kuwa appreciated na kile mtu anafanya.
  Je umewahi kuwa na boss mkali na mwenye maneno ovyo na mtu wa amri?
  Huwa unajisikiaje?
  Fikiria unaishi na mke au mume wa aina hiyo.

  Nami mwenzi wangu yupo kwenye hili kundi, kwake kumpenda ni pamoja na kumpa appreciation ya yale anafanya hadi jinsi anavyovaa, mwanzo wa ndoa ilikuwa ngumu kujua ila nilishangaa ananiambia mbona wenzako wananiambia nimependeza na wewe husemi chochote?
  Kwa kutojua nilikuwa namjibu "ndiyo maana nilikuoa ni kweli unampendeza na hilo najua.

  Hata hivyo sasa nimejifunza kusema asante na kumshukuru na kumpa sifa kwa kila anachovaa hata akivaa akapendeza nakuwa mtu wa kwanza kumwambia bibie leo umependeza na unawake.

  Tutaendelea!
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  Love is the most powerful weapon for good in the world. Wakati mwenzi (Spouse) wako anajisikia kuridhishwa kimapenzi (emotionally na romantically) hujisikia salama kihisia na hujiona ulimwengu unampa vyote na matokeo yake hujitoa zaidi kuhakikisha anajiweka katika kiwango cha juu kwako kuimarisha upendo na mahusiano kwa ujumla.
  Na anapojisikia kutoridhishwa kabisa kimapenzi, hujisikia mweupe, empty na kama vile anatumika au unamtumia tu kufanikisha na kutimiza hitaji lako la mapenzi.
  Moja ya tatizo kubwa katika kuonesha upendo (love) tumeshindwa kufahamu kwamba mke na mume huongea lugha tofauti za upendo.
  Kila mmoja huwa na namna tofauti jinsi anavyojisikia unampenda kwa mfano mwingine ukimpa zawadi yoyote hujisikia unampenda na ukimsifia anaona ni maneno matupu na mwingine ukimsifia basi hujiona raha na hujisikia unamthamini na kumpenda.
  Kuonesha upendo kuna lugha kama zilivyo lugha za mawasiliano na utamu wa lugha ni pale unapoifahamu kwa kuisikia na kwa kuiongea, pia utamu wa upendo katika ndoa au mahusiano ni pale unapofahamu lugha ya upendo kati yako na mpenzi wako.

  Itakuwa vigumu sana kwa anayejua kibena kuanza kuongea na anayejua kimasai na wote wakawa wanadhani inawezekana.
  Kumbuka Babeli haikujengwa ikaisha kwani baaada ya lugha kuharibiwa kila kitu kilisambaratika.
  Kimsingi ili kuelewana na mpenzi wako kuna lugha za msingi tano ambazo kati ya hizo moja wapo inaweza kuwa ni maalumu kwa ajili ya mpenzi wako na kuifahamu au kuzifahamu lugha zake basi unaweza kujenga mahusiano imara.

  Hata hivyo mahusiano bora huanza kwanza na Hofu ya Mungu (Christ in you)
  Lugha tano muhimu ambazo mara nyingi wapendanao hutumia ni:
  1. Kuwa na muda na mwenzi wako (Quality time)
  2. Kupeana zawadi (Receiving gifts)
  3. Kusaidia kazi (Acts of services)
  4. Kumpa maneno ya kumsifia, kumtia moyo kwa kile anafanya (words of Affirmation)
  5. Mguso wa kimwili (physical touch)

  KUWA NA MUDA NA MWENZI WAKO
  (Quality time)
  Msingi wa kuwa na muda na mwenzi wako ni upamoja (togetherness) pamoja na kuwa kimawazo, kimwili na kiakili.
  Kukaa na kuangalia TV pamoja si kuwa na muda na mwenzi wako kwani hapo mnaipa TV qulity time.
  Kuwa na muda na mwenzi wako ni kukaa pamoja na kumpa attention yote, anaongea na wewe unamsikiliza tena ninyi wawili tu. Ni kutembea pamoja yaani mmeamua kwenda kutembea kwa ajili ya kwenda kutembea wewe na yeye tu si kwa sababu mnaenda kanisani au mnaenda kazini.

  Kupeana muda wa pamoja ni kama vile kwenda kula pamoja (outing) ninyi wawili na mkifika hapo kwenye hoteli mnaongea kwa kuangaliana ninyi.

  Kama mpenzi wako yupo kwenye hili kundi yaani kwake kupendwa ni kuwa pamoja basi ni dhahiri ukifanya haya mara kwa mara anatajisikia raha sana na atajisikia unampenda sana.

  Hata hivyo kama mpenzi wako kwake lugha ya upendo ni zawadi ataanza kulalamika why unakuwa na mimi tu muda wote hata zawadi huniletei?
  Maana kwake kupokea zawadi ndo kuonesha unampenda na si kufuatana kila mahali.

  KUPEANA ZAWADI
  (Receiving gifts)
  Zawadi ni kitu chochote unachoweza kukishika kwa mikono na kinakupa hisia kwamba aliyenipa zawadi alikuwa ananifikiria na ananipenda.
  Zawadi huelezea upendo kwamba alikuwa ananiwaza na kuniona mtu wa maana sana kwake.

  Wanandoa wengi hupuuza na kuona kwamba zawadi siyo kitu muhimu ktk mapenzi, pia wapo wengine hudhani zawadi kwa mpenzi hadi kiwe kitu kikubwa kama gari au nyumba, vitu vidogo sana kama pipi, Chocolate au maua ni zawadi za msingi sana na zina maana kubwa sana katika kuimarisha mapenzi katika ndoa.
  Nahisi hata wewe msomaji ulikuwa maarufu sana kutoa zawadi wakati wa uchumba na sasa umeacha, Bisha!

  Zawadi muhimu pia ni wewe kuwepo au kupatikana pale mke wako au mume wako au mpenzi wako anakuhitaji anapokuwa na shida (wapo wakiona shida hukimbia wapenzi), uzoefu inaonesha zawadi hata za kutoa muda wako hukaa ktk kumbukumbu za mhusika kwa miaka mingi bila kusahau na pia huongeza level ya mapenzi kwako.

  Inawezekana mke wako au mumeo ni watu ambao akipewa zawadi basi yeye ndo kupendwa yaani ndo anaguswa zaidi, moyo wake unaamini ukipewa zawadi ndo unapenda.
  Kama mpenzi wako kupewa zawadi ndo lugha yake ya upendo basi ikitokea wewe unampa sifa kwa mambo mazuri anafanya usishangae akikwambia punguza maneno zawadi zipo wapi? Atakwambia anataka matendo si maneno!
   
 6. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Good job. Be blessed.
   
 7. 007/Mrs.bond

  007/Mrs.bond Member

  #7
  Jun 3, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Imetulia ndugu, i think i will contact you for further question regarding marriage issues it you don´t mind. Big thumb
   
 8. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,466
  Likes Received: 5,708
  Trophy Points: 280
  Imetulia ndugu, i think i will contact you for further question regarding marriage issues it you don´t mind. Big thumb

  UR WELCOME BABY
   
Loading...