Mahusiano na majirani gharama

bhakamu

JF-Expert Member
Sep 6, 2016
770
720
Waungwana niwashirikishe hili, nimefanikiwa kujenga kakibanda ili niondokane na kupanga japo hakijaisha lakini nimeamua kuhamia hivyo hivyo tu.

Sasa kinachonisibu ni kwamba kuna jirani yangu ukuta wake wa fensi uliangukia upande wa nyumba yangu hivyo kufanya eneo la nyumba kujaa vifusi vya tofari na kabla sijahamia nilimtafuta na kumuomba vile vipande nivitumie kufukia ndani alikataa alisema anamatumizi navyo sikua na kinyongo nae nilimwelewa.

Chakushangaza alivojua tu kuwa nimehamia ananipigia simu anasema hivyo vipande nichukue! nimemwambia kwa Sasa sina matumizi navyo na kumtaka aviondoe kwenye eneo langu na wiki sasa jamaa hajafika na anaishi eneo tofauti na uko.

Nifanyeje wadau ikizingatia kuwa mahusiano ni gharama.
 
Kwanza inabidi tujue unataka njia ya shali iwe shali au ya kistaarabu maana njia zote zipo mezani🥴
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom