Mahusiano kati ya Tanzania na China yanaimarishwa

Nyabukika

JF-Expert Member
Jun 15, 2022
1,402
942
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya Ziara ya Kitaifa nchini China kuanzia tarehe 2-4 Novemba 2022. Hii ni kufuatia Mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping. Taarifa hiyo imetolewa leo na Wizara ya Mambo ya Nje China.

Tanzania na China tumekuwa ni ndugu na tumekuwa tukishirikiana kwenye mambo mengi ya ujenzi wa taifa letu. Rais Samia Suluhu anaendelea kuimarisha uhusiano wetu

China pia imefadhili miradi mingi nchini na pia ni soko kwa bidhaa nyingi kutoka nchini. Kwa hii ziara Mh rais anaenda kuendeleza uhusiano utakao saidia kukuza uchumi nchini, ufadhili pamoja na uwejezaji katika sekta mbali mbali ikiwemo miundombinu, viwanda na teknolojia.

Hakika Rais Samia ni gwiji katika diplomasia ya kimataifa. Nchi inafunguka na fursa zinatafutwa kwa maendeleo ya nchi yetu.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya Ziara ya Kitaifa nchini China kuanzia tarehe 2-4 Novemba 2022. Hii ni kufuatia Mwaliko wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa China, Xi Jinping. Taarifa hiyo imetolewa leo na Wizara ya Mambo ya Nje China.

Tanzania na China tumekuwa ni ndugu na tumekuwa tukishirikiana kwenye mambo mengi ya ujenzi wa taifa letu. Rais Samia Suluhu anaendelea kuimarisha uhusiano wetu
Ni jambo jema, Rais Samia anakazana kweli kuiinua Tanzania katika nyanja za maendeleo. Suala la mahusiano na China lina sura mbili.

Moja, China ni mfadhili mzuri katika uendelezaji wA MIUNDO MBINU yaani barabara, majengo mawasiliano.

Pili China ambayo huko nyuma ilikuwa mbele katika huduma za kijamii kama afya nk, lakini sivyo hii leo.

Sababu yake nini?

Wakati huo huo mshindani mkuu wa China yaani Marekani ambaye ni mchuuzi mkubwa wa madini yetu, ndio amekazana kweli kweli kwenye UKIMWI / Afya nk.
 
Rais Samia Suluhu anaendelea kuimarisha diplomasia ya uchumi
 
Back
Top Bottom