Invisible
JF Admin
- Feb 26, 2006
- 16,285
- 8,363
Kwanza nikuombeni radhi nyote ambao mlikuwa mmeandika michango yenu na ikazimika ghafla. Ni kutokana na matatizo ya kiutendaji. Forum hii inahitaji mod mwenye busara kubwa kuwahudumia wanachama wake.
Tuliamua kuiweka offline kwa muda kuangalia uwezekano wa kuirejesha kwa mtizamo chanya ambao tunaamini mtatuelewa na kutilia maanani mapendekezo yetu.
Mapendekezo yetu yako hivi:
1. Kutakuwa na uchelewaji wa kutoa majibu moja kwa moja katika majukwaa (forums) mengi kutokana na uwingi wa michango inayoandikwa kila siku JF. Hivyo uwezekano wa kupata majibu ya haraka toka kwa viranja ama mods kama tulivyozoea kuwaita utakuwa mdogo. Tunaomba wanachama ambao wanajua nafsi zao ziko 'dedicated' katika kuwasaidia wenzao watusaidie kuwajibu na kuhakikisha kila kitu kinaenda salama. Hatutarajii matusi na kashfa kama ilivyotokea kwenye forum ya Dini. Heshimianeni.
2. MUHIMU SANA: Picha za uchi; video za uchi ama ngono hazitaruhusiwa hapa. Ukitaka kufanya mambo kama hayo tafadhali omba ruksa ya kutembelea Jukwaa la 'Mambo ya Kikubwa'. Huendi huko kirahisi bila kuomba kibali maalum na kuidhinishwa. Hatutamvumilia atakayeweka picha za uchi eneo hili ama video za ngono. Atafungiwa kwa muda usiopungua juma moja.
3. Lugha kali za mapenzi ikiwa ni pamoja na zile zisizokuwa na tafsida zitafutwa na mwanachama aliyetoa kauli husika atachukuliwa hatua kali ikiwa ni pamoja na kufungiwa. Sehemu za siri ziitwe hivyo na tusipende kuita koleo kuwa koleo. Ieleweke wazi kuwa hili ni jukwaa huru na wanatembelea watoto. Waonee huruma kuwaharibia maisha. Vinginevyo tutafunga moja kwa moja jukwaa hili kwa kukiuka kipengele hiki. Mtoto wa mwenzio si mkubwa mwenzio; mlee alinufaishe taifa.
Mwisho nawatakia mijadala myema na kuwatakia ufanisi katika kila mfanyalo katika mwaka 2008 na miaka ijayo.
Invisible
For JF Management