Mahujaji Manyara wapokelewa kwa furaha na mamia ya watu

John Walter

Member
Aug 14, 2017
64
62
Mahujaji waTanzania wameanza kuwasili nchini tangu walipoelekea Saudi Arabia kwa ajili ya kutekeleza nguzo ya tano ya dini ya kiislamu ya kuhiji Makkah inayofanywa na watu mbalimbali duniani.

Kwa mwaka huu mkoa wa Manyara mahujaji wawili kutoka wilaya ya Babati walipata nafasi ya kwenda kutimiza nguzo hiyo kuu na muhimu ya dini ya kiislam,ambao ni Alhaji Sheikh Shabani Msii pamoja na Alhaji Sheikh Nuhu Ibrahim Ngaso ambapo wamewataka waislamu na wasio waislamu kutenda yale ya kumpendeza Mungu.

Akizungumza na kituo hiki Alhaji Sheikh Nuhu Ngaso amesema kuwa wapo wislamu wengi wangependa kwenda hijja ila wanakosa hamasa kutoka kwa viongozi wao na kuwataka viongozi kusisitiza hilo.

Naye sheik mkuu wa mkoa wa Manyara Mohammad Hamisi Kadidi akawaagiza viongozi wote wa dini ya Kiislam mkoa wa Manyara kutoa elimu kuhusu hijj.

Mamia ya waislamu mkoani hapa walijitokeza kwa wingi kuwalaki mahujaji hao ambao walifikia katika msikiti wa Bakwata Babati mjini na hatimaye kuwatembelea na kuwasalimu waislamu waliopo Galapo na Mamire.
 
Kwanini ulifungua na kuisoma?
Muulize uwezo wa kufikiri hawana ndio maana wanashindwa kugundua sikuu zao amezipanga nani wenyewe nikusherekea tu hamna kufikiri wala kuhoji waweke nawao hija kama mungu atakubali wanafikiri nimchezo bila mungu kukubali
 
Back
Top Bottom