mahudhurio ya wabunge bungeni ni hiari au wajibu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mahudhurio ya wabunge bungeni ni hiari au wajibu.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Iron Lady, Feb 8, 2012.

 1. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,079
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  nimekuwa sielewi kabisa ninapoona viti vipo tupu bungeni huwa najiuliza ni kwamba viti vimekuwa vingi sana? au wabunge hawahudhurii?

  kikao cha kwanza cha mkutano huwa wanajaa halafu ghafla hupungua hadi kufikia ndogo kiasi cha kuona viti vitupu, jioni ndio kabisa sasa huwa wanaamua tu kutokwenda, wanakuwa na majukumu mengine au ni nini? na kama huwa watoro nasi tunalichekeaje jambo kama hili? kama wamekwenda bungeni kwa ajili ya kutumikia nchi iweje asikae bungeni kusikiliza mambo mbalimbali na kushiriki kikamilifu.
  na kama wanatumwa kwa ninin uwe muda wa kukaa bungeni watumwe muda mwingine. hawa wabunge wapo makini kweli au ni hiari kuingia ama kutoingia bungeni.
   
 2. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #2
  Nov 1, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,079
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  kwa kweli kitendo cha bunge kuwa tupu kinaendelea kunikera kiasi cha kufanifanya niendelee kutoelewa kwa nini bunge lipo tupo kwa kiasi hiki. ka ni kazi nyinigne kwa nini ziwe kipindi cha bunge? kwa nini zisifanywe wakati mwingine na wakati wa bunge wote wawepo bungeni. labda mnieleweshe jamani nashindwa kuelewa hili.
   
 3. g

  gastone JF-Expert Member

  #3
  Nov 1, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 329
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  honestly, wabunge wengi hawako serious na kazi yao! Wakishasaini asubuhi na kuwa na uhakika wa posho basi, kazi kwisha! Ni kuzurura tu kwenye viunga vya mji wa dodoma kana kwamba ndicho kilichowaleta hapa. Nadhani spika anapaswa kwenda mbali zaidi kwa kuwa mkali - kwa kutumia ile kanuni 'spika atakavyoona inafaa' basi zile karatasi za kusaini mahudhurio zipitishwe bila muda maalum angalau mara 4 kwa siku, asiyekuwepo na lake halipo!
   
 4. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #4
  Nov 1, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,079
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  si tu spika hayuko mkali hata sisi wananchi nahisi hatuoni kama hili ni tatizo kama tunalipa kodi zetu na kodi hizi ndio zinawaweka wabunge hapo ukiachilia kura zetu tulizowapa kwa uaminifu inauma kuona sisi haohao hatuoji wala kustuka.
   
 5. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #5
  Nov 1, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,079
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  nafikiri mahudhurio ya bunge yanapaswa kuangaliwa kwa umakini mkubwa sababu zisizo na msingi zaidi ya ugonjwa na dharura kwa mawaziri zinaweza kueleweka, lakini eti wana kazi nyingine kazi gani hiyo isiyoweza kusubiri vipindi vya bunge kuisha?
   
 6. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #6
  Nov 1, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,079
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  na tabia ya wabunge kuwepo katika kazi za kamati wakati wengine wapo wanaendelea bungeni kujadiliana mambo mbalimbali ni kuwanyima haki yao ya kuchangia na pia kutunyima sisi wananchi haki yetu ya kutetewa endapo engebidi na hao wawakilishi wetu ambao hawapo kwa muda huo bungeni. nielewesheni jamani nini sababu ya hii tabia ya kutohudhuria bungeni kuonekana kama jambo la kawaida?
   
 7. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #7
  Nov 1, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,079
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  nilishawahi kumsikia spika makinda akisema wabunge wasiokuja huwa hawasaini posho, lakini kwa nini mbunge asiende bungeni hata kama hatasaini hizo posho kwenda kuhushuria ni kujisikia au ni wajibu?
   
 8. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #8
  Nov 1, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,079
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  wakati mwingine unaona wanaingia wamechelewa na kwa kujivuta vuta kweli utafikiri sijui hawataki. hakuna kuadabishana ndio maana wanafanya hivi.
  nafikiri wangeadabishwa ipasavyo na kuwa na sheria kali wasingefanya mzaha katika hili.
   
 9. Kennedy

  Kennedy JF-Expert Member

  #9
  Nov 1, 2012
  Joined: Dec 28, 2011
  Messages: 11,243
  Likes Received: 2,924
  Trophy Points: 280
  Tija ya mwananchi ni ktk uchaguzi tu,kazi wabunge walio wengi imewashinda kbs. Wanajari posho na miradi yao tu thamani ya mwananchi 2015.
   
 10. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #10
  Nov 1, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,079
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  kiongozi,
  hata sisi pia kazi ya kuwataka wafanye kama inavyowapasa imetushinda au na sisi ndio tunachukulia poa?
  kama tumewaweka basi wafanye inavyowapasa, sasa sisi mbona tumekaa kimya hawatabadilika hawa.
  wakitoa hoja utasikia watu wangu wamenituma, sasa tukiwataka wawe na adabu ya mahudhurio itakuwa mbaya?
   
 11. g

  gastone JF-Expert Member

  #11
  Nov 1, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 329
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu, vp kuhusu 'vitu' maalum?!
   
 12. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #12
  Nov 1, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,079
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  vipi hivyo?
   
 13. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #13
  Nov 1, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 170
  Trophy Points: 160
  Kuna siku patakuwa peupe pale afu kikao kitaahirishwa, serikari ya jk hii!! tutaona mengi
   
 14. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #14
  Nov 1, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  mimi sina tatizo la wabunge kutohudhuria vikao, tatizo langu ni je wasipohudhuria vikao bado wanalipwa posho zao kwa siku? kama wanalipwa then huo ni ujambazi wa hali ya juu unaonfanywa na hao so called wabunge ni kuhakikisha tunawajua ni akina nani so that ifikapo uchaguzi ujayo hawachaguliwi tena kurudi bungeni
   
 15. J

  Jajani Senior Member

  #15
  Nov 2, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 138
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Makinda anawachekea, wakati wa kuwatembelea wananchi ni wakati mwingini wote isipokuwa wakati wa vikao.
  Taarifa zikusanywe wakati wa kuwa majimboni au kwa kutumia makatibu wao au kwa njia ya sms.
  Wabunge wengi hawahudhurii vikao muda mwingi kwa sababu zisizo za kisheria ila ni za kisiasa.
   
Loading...