Mahubiri ya leo yasisitize juu ya haki maana ndiyo Mama wa Amani

kindikwili

JF-Expert Member
Oct 5, 2016
1,862
2,871
"Sema kwa ajili yao na kuamua kwa haki, Linda haki za masikini na fukara" Methali 31:9

Amani iwe kwenu wana jamiiforums, kwanza namshukuru Mungu baba mwenyezi muumba wa mbingu na nchi kwa kutupa afya njema mpaka wakati huu tunatazamia kumaliza mwaka huu wa 2019. Kwakweli sifa na utukufu ,shangwe na shukrani ziwe juu yake yeye aliye mtukufu sana.

Kwenye mkesha wa krismass na ibada iliyofuata wahubiri karibia wote walisisitiza juu ya watanzania kutunza amani na kuwa watulivu wakati wote. Magazeti yaliyoandikwa siku baada ya mkesha yalikuwa na vichwa vya habari tofauti lakini karibia zote zilikuwa zinahusu kutunza amani, kwani wahubiri kuanzia maaskofu, mapapdre, wachungaji , mitume na manabii nchini walihubiri juu ya wananchi kutunza amani ya nchi.

Binafsi sina tatizo na msisitizo wa kutaka wananchi kutunza amani au hata kuliombea nchi ili iwe na amani, ila ninachoona cha msingi ni watu kusisitizwa kutenda haki. Mtu moja moja asisitizwe kutenda haki kwakwe binafsi, familia yake, majirani na jamii inayomzunguka. Viongozi wa serikali na wote wenye mamlaka wasisitizwe kutendea wananchi na wageni wanaotembelea nchi kwa haki. Msisitizo huu uzingatie haki zote kuanzia zile za binadamu, haki za watu, haki za kisiasa, haki za watoto , haki za wamama na aina nyingine yoyote ya haki.

Viongozi wa tume ya uchaguzi , uongozi wa bunge, uongozi wa mahakama, uongozi wa serikali kuanzia serikali kuu na za mitaa, uongozi wa jeshi la polisi na vyombo vyote vya usalama wasisitizwe kutenda kwa haki. Kila mtanzania atende haki kwa wengine na atendewe kwa haki.

Mtu akikosa aadhibiwe kwa mujibu wa sheria za nchi na si katika namna inayokiuka haki zake. Kama wimbo wa kulinda haki za wengine utaimbwa na kueleweka kama ambavyo wimbo wa kulinda amani unavyoimbwa basi itakuwa ni upotevu wa muda kuombea amani maana amani itakuwepo bila hata kuombewa. AMANI NI MATOKEA YA KUWEPO KWA HAKI mimi nadhani kuombea amani huku ukiacha kusisitiza uwepo wa haki ni makosa makubwa.

Sitaki kuwapangia maaskofu cha kuhubiri ila nawaomba wasome bibilia vizuri wajionee jinsi ambavyo Mungu hupenda haki na anavyotutaka tutende kwa haki. Tuhubiri haki kwa sauti kubwa bila ya kuogopa na popote haki ya mtu inapodhulumiwa tukemee na tusimame naye maana hata Mungu wetu husimama na wenye haki. Haki ni haki maana Mungu hajasema ni haki gani bali kasema katika mithali 14:34 kuwa haki huinua taifa , bali dhambi ni aibu kwa watu wote.

Nawatakia heri ya mwaka mpya Mungu atuwezeshe kuumaliza mwaka salama.

Kindikwili- Masasi
 
Amen!
IMG-20191231-WA0009.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo akofu Bagonza kanena ya Mungu wa kweli ambaye kwake haki ni kitu cha kwanza. Mungu wetu ni Mungu wa haki na ili tuwe wake lazima tutende kwa haki
 
Back
Top Bottom