Mahubiri kama haya hayamjengi mtu, yanampotosha tu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahubiri kama haya hayamjengi mtu, yanampotosha tu!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magobe T, Dec 7, 2009.

 1. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #1
  Dec 7, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Usiku wa kuamkia leo - Jumatatu - (saa tatu na robo hivi) nilifungua Radio Station moja ya Kiislamu hapa Tanzania na kusikiliza mahubiri yaliyonisikitisha sana. Mhubiri/mwalimu (sheikh mmoja au mtaalamu wa dini ya Kiislamu) alikuwa akikosoa sana kongamano lliloandaliwa na Mwalimu Nyerere Foundation hivi karibuni. Aliwakosoa waliochangia mada katika ‘conference’ hiyo.

  Aliponda sana Serikali ya Awamu ya Kwanza, akasifia ya Awamu ya Pili na hii ya Awamu ya Nne. Ya Awamu ya Tatu sikusikia akiitaja. Nadhani aliiweka kwenye kundi sawa na ya Awamu ya Kwanza. Alidai katika Awamu ya Kwanza hali ya umaskini ilikuwa mbaya sana nchini na neema iliaanza kuja wakati wa Awamu ya Pili. Na hiyo, alisema ilitokana na uongozi mzuri wa Rais Mstaafu Ali Hassani Mwinyi.

  Aliuliza, “Mbona rushwa ilikuwepo sana enzi za Serikali ya Awamu ya Kwanza na hakuna aliyejitokeza waziwazi kuikosoa Serikali kama baadhi ya watu wanavyofanya leo hii? Hii inasababishwa na nini?” Mimi sikuelewa kabisa mantiki yake. Yaani, kama kitu hakikukosolewa enzi za Mwalimu Nyerere basi kisikosolewe tena hadi mwisho wa dunia?

  Mbona mazingira yamebadilika na watu pia wamebadilika? Ni kama kusema kwa vile hapakuwepo maendeleo fulani wakatu ule basi yasiwepo tena! Kwa vile barabara wakati ule zilikuwa chache basi ziendelee kuwa hizohizo! Mbona ni mawazo mgando sana kutoka kwenye kinywa cha kiongozi wa kiroho? Huyu kwa mtazamo wake finyu hawezi kuwakosesha watu anaowaongoza kama watafuata mawazo yake mgando hayo?

  Kuhusu kongamano, alisema wote waliochangia ni wanafiki na wana ‘underplay’ juhudi za Rais Jakaya Kikwete kwa vile ni Mwislamu. “Mbona hawakufanya hivyo enzi za Mwalimu Julius Nyerere?” alihoji.

  Alinukuu mchango wa askofu mmoja wa KKKT aliyechangia: “Shule za Kata zitaleta ukabila.” Baada ya nukuu hii akasema, “Kwa juu juu mtu anaweza kusema ni kweli alichosema askofu wa KKKT kwani wanafunzi wanasoma katika mazingira yaleyale kuanzia shule ya msingi hadi sekondari, hivyo hawataweza kuchanganyikana na wenzao wanaotoka kata/wilaya/mikoa mingine ya Tanzania. Lakini ukiangalia kwa makini sana, ‘issue’ siyo ukabila bali ubaguzi wa kidini.”

  “Hawa maaskofu wana akili sana. Wameona kuwa kukiwa na shule nyingi za kata, Waislamu wengi watapata elimu na ili kuwanyima hiyo fursa, wanakuja na mbinu mpya eti shule hizi zitaleta ukabila. Huu ni uongo wa kutunga unaoenezwa na viongozi wa Kikristo kwa nia ya kuwafanya Waislamu wakose nafasi ya kusoma,” alisisitiza.

  Halafu alihoji inakuwaje ‘enrolment’ katika shule za msingi watoto wengi wanatoka familia za Kiislamu lakini wanaanza kuenguliwa wanapoingia elimu ya sekondari na chuo kikuu na badala yake wanachukuliwa Wakristo kwa zaidi ya 80%. Alisema kwa upande wa elimu ya sekondari ni 30% tu ya watoto kutoka familia za Kiislamu wanaochukuliwa kujiunga na elimu hiyo lakini kwa Wakristo ni 70%. “Ndiyo maana hata kwenye ajira utakuta wengi wa walioajiriwa ni Wakristo,” alisema na kuuliza: “Hii inakuaje kama siyo mchezo mchafu unaochezwa?”

  Halafu kaja kwa askofu Methodius Kilaini. Akasema: “Kilaini alisema hapa Tanzania tunatembea uchi na ni vizuri kuona watu wanaanza kuamka na kushughulikia maswala yanayohusu maisha yao. Endeleeni kupiga kelele, msichoke. Pambaneni na ufisadi…”

  Akasema: “Kama askofu Kilaini anasema watu wanatembea uchi basi vazi sahihi ni hijabu tu… Yeye anajifanya kupinga ufisadi wakati wao wenyewe ndio mafisadi.”

  Nilisikitika sana kusikia kiongozi kama huyo anayesikilizwa na kuaminiwa na waumini wake na pengine na wasikizaji wengine wasio waumini wa dini ya Kiislamu anaweza kuongea pumba kama hizo.

  Kwa upande wangu waliochangia kwenye kongamano walitoa maoni yao kwa kuangalia nchi inaelekea wapi na ‘issues’ walizozizungumzia zinahusu maslahi ya Watanzania wote. Cha kushangaza ni kuona baadhi ya watu wanajaribu kupotosha kabisa lengo la kongamano lenyewe.

  Hivi Watz tumebaki tu watu wa kusifia viongozi wetu hata kama tunaona udhaifu na kama wakitokea watu wa kukosoa kitu wanaonekana hawafai? Binafsi, hata Rais Kikwete mwenyewe anaona unafiki wa wale ‘apologetics’. In fact, watu wanapokosoa Serikali inawezekana hata Rais Kikwete mwenyewe anafurahi kuona mambo ambayo yangetakiwa kufanyika na hayafanyiki yakiibuliwa ili wahusika wawajibike.

  Ila anajua fika wanaopinga mchango chanya ni wapiga debe (opportunists) tu, hawasemi kinachotoka moyoni mwao. Na mambo yatakapoharibika zaidi watu haohao watamgeuka. Kweli kwa kuona hali tuliyo nayo hapa nchini kwa kulinganisha na raslimali tulizonazo mtu anadiriki kukubali kabisa ‘we’re on the right path’ na hakuna cha kurekebisha? Maana kukosoa kuna maana kwamba baadhi ya mambo yangeweza kufanywa vizuri zaidi kuliko ilivyo sasa hivi. Kwa nini tusitunie muda huo kujifunza kuboresha zaidi hayo yanayokosolewa?

  Nakubaliana kabisa na wote wanaoikosoa Serikali na hii ni kwa sababu naipenda Serikali yetu kuliko Serikali yoyote duniani na ninataka iendelee kufanya vizuri na ili ifanye hivyo inabidi irekebishe baadhi ya mambo.

  Hebu angalia adha ya usafiri – msongamano wa abiria ndani ya gari moja (zero distance). Na tunafanya hivyo ili tuwahi kazini kwani hakuna atakayechelewa na kusema usafiri ulikuwa mgumu na boss wake kukubali hoja yake. Na mtu anaona kuchelewa kila siku kazi inaweza kumwiishia. Hivyo anaamua tu kuikubali hali yenyewe ili aendelee kuwa kibaruani.

  Jioni baada ya kutoka kazini ni shida pia. Na unakuta akina mama wakichelewa waume zao hawatasema ni tatizo la usafiri. Baadhi yao tunasikia wanavyopigiwa simu na waume zao na wanavyojitetea, lakini aliye nyumbani anadhani ni fix tu na wakati mwingine kumwabia mkewe ikifika muda fulani hajafika asikanyage nyumbani kwake!

  Hebu angali mgambo wanavyonyanyasa wamachinga lakini wameshindwa kuwadhibiti wapiga debe ambao sasa hivi ndio wanaopanga nauli za magari ya abiria. Nenda Kariakoo jioni kuanzia saa 12 au hata kabla. Ikifika saa moja hivi baadhi ya magari yanasitisha 'routes’ zao na kuanza kupakia abiria wa kwenda Mbagala kwa nauli inayotangazwa na wapiga debe kuanzia Sh500, Sh1,000 na wakati mwingine Sh1,500 badala ya Sh250. Kwa vile mtu amekaa kituoni muda mrefu akisubiri usafiri bila kupata, analazimika kulipa hicho kiasi, afanye nini?

  Hebu angalia sekta binafsi: ‘junior staff’ wanakaa miaka nenda rudi bila kupandishwa mshahara lakini vitu vinapanda karibu kila mwezi. Je, kweli hawa wataweza kuinuka kiuchumi? Lini wataweza kutunza hela ili waweze kujenga nyumba au hata kusomesha watoto kwenye shule nzuri? Wakinunua kiwanja kilichopimwa, kina time limit – miaka mitatu. Kama hawatakuwa wamekiendeleza (na mara nyingi ni kwa sababu kipato chao ni kidogo, wananyang’anywa) na kupewa wenye uwezo.

  Hebu angalia maisha ya wananchi wa kawaida Kanda ya Ziwa Viktoria – wala mapanki. Sehemu wanakoruhusiwa kuvua ni katikati ya ziwa. Wavuvi wadogowadogo wakienda huko wanapigwa na wakati mwingine kutumbukizwa majini kwa vile wavuvi wakubwa wanawachukulia wao kama wezi wa nyavu zao. Wavuvi wakubwa wana ‘patrol boats’ na wengine wana silaha za moto.

  Hawa wavuvi wadogo wakivua maeneo mengine, wanakuwa wavuvi haramu – wanakamatwa, nyang’anywa kila kitu (wenye uwezo wanaweza kuhonga na wasio na uwezo wanaishia jela) na kushtakiwa kwa kukutwa na zana haramu za uvuvi au kuvua maeneo yaliyokatazwa na Serikali. Wataishije?

  Hebu angalia jinsi wananchi wanavyohamishwa kupisha mradi fulani au mwekezaji – utadhani wanaosimamia zoezi hilo wameambiwa bila kutumia nguvu zote hizo mwekezaji huyo atakufa. Utaratibu wa kufidia wanaohamishwa mara zote siyo mzuri na unaacha malalamiko mengi kwa wananchi.

  Hebu angalia madini tuliyo nayo na faida tunayopata kama taifa. Nchi nyingine madini haya ndiyo yanayochangia kuborsha huduma za jamii na kuongeza ‘quality of life’ ya wananchi. Siyo hivyo hapa Tanzania.

  Hebu angalia aina ya magari yanayonunuliwa na vigogo wa Serikali. Hata baadhi ya wafadhili wanatushangaa kuendelea kuomba misaada na wakati matumizi yetu ni ya anasa.

  Hebu angalia ‘customer care’ kwenye ofisi za Serikali. Watu wako pale utadhani wamelazimishwa kufanya kazi na wanaona udhia kumdhudumia mteja. Kwenye baadhi ya ofisi utakuta mtu anacheza ‘game’ kwenye komputa au simu na anaona shida kukwambia mteja: “Karibu, nikusaidie nini?” Wengine unakuta wanapiga soga ofisini na hawana muda wa kumsikiliza mteja.

  Angalia ‘behaviour’ ya askari wetu hasa kama wanaendesha gari. Ni wao wa kwanza kutanua kwa vile gari lao lina namba zinazoanza na PT au JWTZ. Itokekee kwa bahati mbaya ugongane na askari wa JWTZ au ukwaruze gari lao utakiona cha moto – makofi, ‘push-up’, viringika etc. Na hawa ndio walinzi wetu! Ila wao wakikwaruza gari lako, wanakuomba samahani na kwa vile huna nguvu yanaisha!

  Yaani kuna mambo mengi sana ambayo yanaonekana hayako sawa na bila kurekebisha haya, maendeleo yatabaki kuwa ndoto Tanzania.

  Ili tuweze kuondokana na ufisadi na wizi uliokithiri wa mali ya umma - mali ya Watanzania – ambao wengi wao wanazidi kuwa maskini na matajiri wanazidi kuneemeka inabidi tubadilike.

  Tuchague viongozi wenye sifa na waadilifu na wanovurunda tuwatoe. Lakini akitokea mtu, taasisi fulani kutoa changamoto tunamkemea au tunaikemea utadhani kuna kosa la uhaini. Hivi hapa Tanzania, nani atamkosoa mwingine? Akijitokeza mmoja tutamshambulia ili akae kimya!

  Ni kweli nchi yetu inaharibika na tunaiharibu wenyewe. Na hasa viongozi kama huyu mhubiri au mwalimu wa dini ninayemzungumzia anawaingizia waumini wake mawazo mfu kama hayo, si na wao wanaamini kabisa kama alivyosema? Jamani tuwe na uchungu na nchi yetu na hali za Watanzania wenzetu!
   
 2. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #2
  Dec 7, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mpigie simu akufafanulie vizuri...
   
 3. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #3
  Dec 7, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Waislamu ni wanafiki kweli kweli. Sijapata ona tokea dunia hii iumbwe. lol
   
 4. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #4
  Dec 7, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kama ilivyo wakristo wanafiki wakubwa toka mwanzo wa dunia?
   
 5. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #5
  Dec 7, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Kumbe Ukristo ndio dini ilikuwa tokea mwanzo wa dunia.

  Wafffuasi wa allah kiumbe, ipo kazi,
   
 6. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #6
  Dec 7, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Uwezo wako kufikiri ni mdogo sana...
   
 7. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #7
  Dec 7, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  His research appears unethical due to lack of religious and scientific merits.

  The islamic ideogy being employed by the so called Shehe/Mtangazaji does not appear to give us any criteria that stipulates his conclusion, and it would probably not prove anything zaidi ya kuonyesha unyonge ndani ya Islam.

  Shehe go and find a life. Maoni ya huyu Shehe are unmeritorious.

   
 8. M

  Magezi JF-Expert Member

  #8
  Dec 7, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Huwa nashangaa shehe yahya anawa danganya watu wake eti kuna pete za bahati kumbe anafanya biashara. Wahubiriea watu wako waende shule siyo wavae pete eti zina bahati, mtaishia kulalamika tu.
   
 9. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #9
  Dec 7, 2009
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Magezi

  Hizo pete atawauzia nyinyi munaoona njia rahisi ya kupata utajiri ni kwa kutumia viungo vya albino au ngozi za watu wengine
   
 10. F

  Future Bishop Member

  #10
  Dec 7, 2009
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 75
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Magobe nafikiri isikupe shida sana, kwani mtu anasema kile kinachoujaza moyo wake ambacho kwa kiasi kikubwa kinatokana na uwezo wa kufikiri na kuchambua mambo anaokuwa nao mtu huyo.

  Mtu yeyote aliye makini ni yule ambaye ndugu yake hata wa damu akikokesea yuko tayari kumshauri na hata kumuonya mbele za watu ili abadirike kwani anakuwa na nia njema naye.

  Mtu makini hana sababu ya kumtetea mtu eti kwa sababu ni kabila moja, dini moja , itikadi moja n.k hata kama mtu huyo amekosea na anaelekea kubaya.

  Watu wanaolezea ubaya wa Mheshimiwa wetu Kikwete na kujaribu kuchambua uongozi wake, naamini kwa kiasi kikubwa hawasukumwi na dini kama ni hivyo asingepata kura nyingi alizopata 2005. Ila inasababishwa na hali halisi inayoonekana sasa, watu hawawezi kuona nchi inaelekea kubaya harafu watu washindwe kusema. Na kwa kusema kwao naamini wanamsaidia kwa yeye kuona mapungufu yake na kumtaka ajirudi.

  Binafsi kinachoniskitisha ni sasa ambapo watu wanaomsema hata kama wanachokisema ni cha ukweli, wanaomtetea wanasema ni kwa sababu hao waliitaka nafasi yake ya urais 2005 na walishindwa. Mie ningeshauri kuwa asiangalie nani amesema lakini ajiulize JE KINACHOSEMWA NI UKWELI? Kama ni kweli achukue hatua. Hakuna mtu mwenye ufahamu kamili atakayekubali kuongozwa na mtu ambaye hawezi kutoa MAAMUZI SAHIHI.
   
 11. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #11
  Dec 7, 2009
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,197
  Likes Received: 1,003
  Trophy Points: 280
  Nani kawaambia hawa mashehe kwamba tz ni nchi ya kidini? Hawajasoma katiba ya nchi hii kwamba haina dini. Hata hivyo sii wao wakulaumiwa sana zaidi ya viongozi wa kiserikali ambao ndio wakiisha kuzidiwa kihoja wanakimbilia misikitini kisiri kuwalalamikia maimamu kwamba wanaonewa sababu ya dini yao. Ebo! Wameapa kuilinda koran au katiba ya nchi? Na hii chokochoko ya udini ni mpango mahsusi unaoratibiwa na usalama wa taifa na bahasha zinasambazwa kwa kwenda mbele
   
 12. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #12
  Dec 8, 2009
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Siyo mimi tu, kwani wote walimsikiliza wataweza kumpigia simu?
   
Loading...