WomanOfSubstance
JF-Expert Member
- May 30, 2008
- 5,457
- 956
Ndugu zangu,
Majanga yanapotupata ndipo tunakumbuka mengi hasa katika kujikinga ili kuzuia yasitokee.Pia kujitafakari kuona je yanapotokea tuko tayari vipi kuyakabili?
Tumeshapata mafundisho lukuki kutokana na majanga ya moto hasa katika majumba ya makazi, maofisi na hata mahoteli.Hili tukio la sasa la kuungua kwa hoteli za Paradise, Oceanic Bay na Malaika limenikumbusha si zamani sana hotel ya Sea cliff nayo iliungua.Kuna kitu kimoja in common katika sehemu zote hizi.Uezekaji wa makuti.Damu inanisisimka SASA HIVI maana nimekumbuka kuwa pale Uwanja wa ndege Julius Nyerere International Airport kuna harakati za kujenga vibanda vya makuti uwanjani na sijui kama waliotoa idhini ujenzi huo wanafanya hivyo "kudumisha mila na tamaduni za mababu zetu" kuezeka kwa nyasi ili watalii wanaposhuka pale waanze kufurahia utalii au ni kutokujali!
Hivi janga la moto likitokea uwanjani pale, tutamlaumu nani na tumeshindwa kujifunza? Sijui wadau hili mnalionaje? Kama kuna wanachama hapa kutoka kwenye mamlaka husika chondechonde simamisheni huu ujenzi wa vibanda vya makuti pale eapoti!Licha ya kuwa ni hatari endapo moto utatokea, pia ni chukizo machoni pa wale wanaopenda umaridadi!