Mahoka ! Manji naye aishtaki Kagoda- imebaki Rostamu kuishtaki Dowans ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahoka ! Manji naye aishtaki Kagoda- imebaki Rostamu kuishtaki Dowans !

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Mar 5, 2011.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Mmiliki wa Kagoda akwama kutokea kortini

  Ni katika kesi iliyofunguliwa na Manji


  Kesi iliyofunguliwa na mfanyabiashara wa Dar es Salaam, Yusuf Manji dhidi ya kampuni tata ya Kagoda Agriculture Ltd., jana ilitajwa rasmi katika Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam, huku mmiliki wa Kagoda akishindwa kutokea.
  Katika kesi hiyo ya madai Na. 16 ya mwaka 2011, Manji kupitia kampuni yake ya Quality Finance Corporation Limited (QFC), ameishtaki Kagoda akidai kuwa mwaka 2008 aliikopesha Sh. 18.7 bilioni ambazo imeshindwa kuzirejesha.
  Kupitia kampuni ya mawakili ya Law Associates ya Dar es Salaam, Manji amewasilisha madai makubwa manne, ikiwamo Kagoda kulipa kiasi hicho cha Sh. bilioni 18.7 kama yalivyokuwa katika makubaliano.
  Anataka kulipwa pia riba ya asilimia 18 ya kiasi hicho cha fedha kufikia siku ambayo hukumu ya kesi hiyo itatajwa, gharama za kesi na mengine ambayo mahakama itaona yanafaa.
  Jaji Ama Munis, anayesikiliza kesi hiyo, aliema kesi hiyo itatajwa tena Aprili 24, mwaka huu na kuagiza walalamikaji kutoa ushirikiano wa kuhakikisha Kagoda wanapatiwa taarifa ya kufika mahakamani.
  Kampuni ya Kagoda ndiyo inayotuhumiwa kuchota zaidi ya dola 30.7 milioni kutoka Akanuti ya Madeni ya Nje (Epa), kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
  Manji ndiye aliyeidhamini Kagoda wakati wa kufungua akaunti katika benki ya CRDB Benki, huku mkataba wa mkopo ukionyesha kuwa uliandaliwa 12 Septemba 2005, siku 17 kabla ya Kagoda kusajiliwa.
  Kampuni ya Kagoda ilisajiliwa rasmi kwa Msajili wa Kampuni (Brela), Septemba 29, mwaka 2005.
  Manji anadai kuwa ni yeye kupitia kampuni yake ya Quality Finance Limited (QFCL), alikopeshwa fedha hizo ambazo Kagoda inasema zilikuwa ni sehemu ya fedha ambazo serikali ilikuwa inadaiwa na makampuni ya kigeni.
  CHANZO: NIPASHE

  Twazidi kugeuzwa mazezeta !
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Mar 5, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Tatizo hakuna anayejua mmiliki wa Kagoda nani.. Manji anashtaki hewa tu utadhani zile movies za kichina..
   
 3. K

  Kijallo JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 409
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ee Mungu,cc watanzania 2mefanya kosa gani mbele zako,mpaka unashindwa kutuokoa na uovu huu unaotupata,tunatukanwa,tunanyanyasika,tunaibiwa na wageni pamoja na wTzwenzetu.MUNGU TUOKOE NA MIDOMO YAO,WANAOKULA KEKI ULIYOTUPA WOTE BURE..
   
 4. M

  Mutu JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2011
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  huu mchezo sielewi una mantiki ipi!! somebody help...
   
 5. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  ukarimu wetu ndo ume2fikisha hapa
   
 6. Nzi

  Nzi JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 12,854
  Likes Received: 4,523
  Trophy Points: 280


  Mh! Mimi nadhani Manji anamfahamu mmiliki. Hivi inawezekanaje yeye amdhamini mtu hasiemfahamu?
   
 7. Chapa Nalo Jr

  Chapa Nalo Jr JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2011
  Joined: Dec 8, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 3,193
  Trophy Points: 280
  Wahindi a.k.a mafisadi wana mbinu sana isije ni namna ya kupoteza gemu, hebu tutafakari vizuri, mwishowe itasemwa kagoda haipo na wamiliki hawajulikani kupitia mahakama. Hivyo watu watakuwa wamezibwa midomo na mahakama, kwisha!
   
 8. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #8
  Mar 5, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280

  Manji alidhamini kampuni... msije kushangaa hiyo kesi serikali inaamua kuifuta..
   
 9. r

  rmb JF-Expert Member

  #9
  Mar 5, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 224
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Miye naona huu ni mwanzo mzuri kwa maana ya kwamba sasa tutawajua hao wamiliki wa Kagoda! Manji lazima anawajua hao wamiliki wa Kagoda, maana huwezi kumdhamini mtu usiyemjua hasa linapoingia suala la hela. Siijui sheria vizuri, lakini nadhani mahakama itahitaji mmiliki au mwakilishi wa kampuni, huyo atatusaidia kutupa majibu mazuri ya nani ni Kagoda?
   
Loading...