Mahojiao ya Ruge Mutahaba na MO'S Blog | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahojiao ya Ruge Mutahaba na MO'S Blog

Discussion in 'Celebrities Forum' started by Balantanda, Dec 17, 2009.

 1. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  SWALI: Ruge mutahaba ni nani?
  RUGE: Nimezaliwa Brooklyn New York Marekani mwaka 1970, Primary School nimesoma Arusha School standard 1 hadi 6, kisha nikahamia Mlimani Primary School maeneo ya Chuo Kikuu Dar es Salaam na ndipo nilipomaliza darasa la saba. Kisha nikasoma Forodhani Secondary School form 1 – 4, baadae Pugu High School 5 na 6. baada ya hapo nikarudi Marekani ambako nikaenda kusoma San Jose University California ambako nikachukua BA in Marketing na pia nikawa nakachukua BA in Finance, kozi zote nilisoma ndani ya miaka 5, kind of 2 courses at the same time. Baada ya hapo nikarudi tena Tanzania.
  SWALI: Nini kilichotokea hadi ukajikuta uko cloudz FM?
  RUGE: Wakati nipo Marekani, Joseph Kusaga alikuwa na disco, Clouds Disco, mimi nikawa supplier wake wa vifaa mbalimbali vya music, then hapo tuka-build good friendship. Sasa, niliporudi Tanzania baada ya kumaliza masomo yangu, Joseph Kusaga akanishawishi sana nibaki kutokana na opportunity zilizokuwepo za kuanzisha Radio na kuipeleka katika level nyingine kabisa, ndipo nilipojikuta nipo Clouds Entertainment.
  SWALI: Tuambie kuhusu THT?
  RUGE: Kama Clouds Entertainment tuliamua kuanzisha kampuni ya management ya wasanii ambayo tuliita Smooth Vibes ambayo ndiyo kampuni iliyowatoa wanamuziki kama Lady Jay Dee, Ray C na wengineo. Unajua utakuta kati ya wasanii watano, only mmoja au wawili wana-survive na suddenly utakuta msanii alikuwepo then kapotea. Hii inatokana na kutokuwa na foundation nzuri. Hivyo nikaona ni bora nianzishe House of Talents ambayo sasa kupitia hiyo, tukawa tunawafundisha wasanii misingi ya muziki, kumfundisha msanii how to Manage Industry, Vocal Coaching, Music Business, Music Instrumentation, Dance Classes na kadhalika. Nikagundua kuwa unakuta msanii anaenda kwenye show lakini performance inakuwa mbovu na pia ili msanii aweze ku-last longer kwenye game anatakiwa ajue dancing. Ndio maana THT tukawa na dance classes. THT imewatoa wasanii wengi kamaMaunda Zorro, Mwasiti, Marlaw, Barnaba na wengineo. THT hadi sasa ina miaka minne.
  SWALI: Ukiwa kama mmoja wa wadau wakubwa wa muziki hapa nchini, unadhani muziki wa Tanzania una mwelekeo gani?
  RUGE: Ukichanganya na malengo ya THT, mwelekeo wetu ni mzuri. Sasa hivi wasanii wameanza kutulia, hawakurupuki kutoa nyimbo, wana-take time kujifunza mambo mengi. Tatizo kubwa lililopo sasa hivi ni upande wa mauzo.
  SWALI: Je, umeshawahi kufikiria kufanya kazi nje ya Tanzania?
  RUGE: Kwa ajili ya experience na kuangalia Industry inafanyaje kazi nchi nyingine, yeah. But kimsingi kwa upande wa maisha sifikirii kabisa kuondoka Tanzania.
  SWALI: Profesheni yako ni nini?
  RUGE: I cut across everything! Kifupi just call me mjasiriamali.
  SWALI: Ukipewa nafasi ya kuongea na watanzania wote kwa ujumla, je una ujumbe gani ungewapatia?
  RUGE: Wanalalamika sana as if wao ndio taifa lililolaaniwa kuliko yote. Ukiangalia hakuna taifa lenye freedom na nafasi ya kupata support kama Tanzania kwa sababu ya amani, abundance of resources, always, there’s an opportunity ya kila kitu. Tatizo tunaridhika sana, sasa hebu angalia Distributors wa muziki ni wawili tu. Tumeridhika mapema sana, tuache kuridhika.
  SWALI: Umechangia katika mafanikio ya watu wangapi hadi sasa? Wataje?
  RUGE: Indirectly, nimechangia mafanikio ya watu wote kwenye sector yangu.
  SWALI: Unadhani uliyoyafanya hadi sasa yanatosha? Kamahapana, je ungependa upatiwe support ya aina gani ili ufanikishe kufanya yote unayoyafikiria?
  RUGE: Hapana hayatoshi. Nafikiri, support ambayo ningepewa ni kueleweka. Mimi sio mwanasiasa, nashughulika na entertainment. Entertainment is the third of 5, regardless uchumi uyumbe au usiyumbe entertainment na sala hazitabadilika, zitaendelea kuwepo siku zote kwa kuwa zote ni spiritual. Support ni kueleweka kwa hiki ninachokifanya.
  SWALI: Ungepewa nafasi ya kuchagua mtu mmoja maarufu unayefikiri unaweza kufanya naye kazi hasa katika masuala ya kijamii, ungemchagua nani?
  RUGE: I have people ninaowa-admire sana, people like January Makamba, he’s young, exposed, he understands the needs, in terms of the government he supports a lot. Another person is Mohammed Dewji.
  SWALI: Unamzungumziaje Mohammed Dewji?
  RUGE: Amefanya jambo muhimu kuamua ku-invest in long-term kwenye sports. Ukiangalia alivyofanya kwa vijana wa mbagala ambao sasa ni Africa Lyon. Pia namsifia kwa vitu anavyofanya kwa jimbo lake la Singida mjini. Amekuwa na direct impact kwa watu aliowasaidia. He is a technical person, ni msomi na vitu anavyofanya vingi vinatokana na taaluma zaidi kuliko maamuzi ya kisiasa tu.
  SWALI: Kama una neno lolote la mwisho kwa vijana wa kitanzania?
  RUGE: Ni muda wa vijana sasa kubadilika kwa kuwa asilimia 60 ya watanzania ni vijana, it’s the same ratio uki-compare na nchi nyingine zilizoendelea. Dunia imebadilika sasa na sisi tubadilike.
  Mo blog inamtakia Ruge kila la kheri katika mafanikio na mipango yake ya maendeleo katika maisha.


  My Take


  Nampongeza sana Ruge kwa juhudi anazozifanya katika kuwasaidia Vijana kukuza na kuendeleza vijana wenye vipaji kupitia taasisi yake ya Nyumba ya Vipaji(THT).Pia nimpongeze kwa bidii na juhudi zake katika kuianzisha na kuiendeleza Clouds FM Radio na sasa Clouds Television.Hongera sana Ruge,hakika u mfano wa kuigwa(kwa ujasiriamali wako) na vijana wengi nchini
   
 2. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #2
  Dec 17, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  nampongeza pia, ila ajiepushe na vijana wenye njaa na kiu ya mafanikio hata kwa njia za kifirauni kama rafiki yangu Ephraim KIBONDE.
   
 3. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #3
  Dec 17, 2009
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,604
  Trophy Points: 280
  Nami nampongeza sana RUGE kwa kweli ni mjasiriamali ambae ana vision pamoja na JKusaga wake!!
   
 4. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #4
  Dec 17, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Behind ya anachooongea Ruge NI WIZI WA KAZI NA JASHO LA WASANII
  wanawatumia wasanii kisha wanawadump flat.

  Hata Fisadi ukimfanyia mahojiano hawezi kuongelea failure au kuanika wizi wake hadharani

  RUGE MWIZI NA RAFIKI YAKE KUSSAGA
   
 5. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #5
  Dec 17, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Huyu MO ni MO gani?

  Hii ndiyo culture ya impreciseness niliyokuwa naiongelea. Huyu ni media mogul bongo, anatoa jibu vague kama hili.

  Either anatoa jibu vague kwa sababu hana mtu specific aliyechangia maendeleo yake, au anaye lakini hajui communication skills. Hapa wengine tunaweza kusoma na kuona hubris, kwamba anajiona yeye ni demigod fulani hivi wa entertainment Tanzania ambaye kamsaidia kila mtu.
   
 6. sabasita

  sabasita JF-Expert Member

  #6
  Dec 17, 2009
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 1,508
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Huyo jamaa anayejiita Msanii sounds like a hater. Ruge amefanya kazi kubwa sana kwenye entertainment industry ya bongo.
  Stop hating bana, lol.
   
 7. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #7
  Dec 17, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  MO ni Mbunge Mohammed Dewji
   
 8. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #8
  Dec 18, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  wee kila siku unashinda kwenye jukwaa la siasa Mo Dewji humjui mbunge wa kijijikimoja cha huko singida?.handsome boy mmoja hiviila ansaidia sana kijijini kwake ningewish na Wabunge wote wangekuwa kama MO...

  Ruge ni kweli Ruge anasaidia jamani nimeona mchango wake mkubw akwenye shule yatu ya msingi ya Mlimani anajitahidi sana...big up RM.
   
 9. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #9
  Dec 18, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Kama mtu unatafuta majibu yaliyo imprecise angalia Sunday morning tlak shows kwenye broadcast networks. Wale wageni wengi huwaga hawajibu maswali wale
   
 10. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #10
  Dec 18, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Halafu huyu Mo ni mbunge au blogger? Mbunge gani anapata muda wa kublogu?
   
 11. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #11
  Dec 18, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Najua Mo Dewji, najua ana blog. Lakini pia kuna Mo Ibrahim na Mo Mfutakamba etc.

  Nimeuliza kwa sababu sikuamini kwamba Tanzania mbunge anamuinterview media mogul an interesting reversal of roles to say the very least. The interview questions are mainly fluff, media mogul anatoa majibu fluffier than fluff, watu wanaimba ngonjera na sifa kwa bwana.

  Hata kama mbunge angetaka kujitetea kwamba anawakilisha interests za watanzania kwa interview za aina hii hawezi. .

  Mbunge huyu anafurahisha sana. Amemzidi hata Larry King kwenye u-Larry King.

  Hiki ki-blog ni sehemu ya watu kujikoki tu, na kuijulisha dunia "nilizaliwa Brooklyn" na wengine "nilipelekwa kijijini kwa bibi", nothing substantive.

  Mtu anaulizwa umemsaidia nani bila haya unasema nimesaidia industry nzima? umekuwa 2Pac au Jay-Z? Maana hawa mabingwa ndio wanajulikana kwa kutengeneza reality zao wenyewe na kuishi nazo, angalau wao wanaweza kusema wanauza image, humu bwana anaonekana hubristic tu kwa kusema hivyo.

  As if that is not enough, alipoulizwa profession yako ni nini

  Jamaa anaelewa maana ya profession lakini? Hata kama anaongelea deals anazofanya, kwa hiyo hata mdude unauza?

  Kaulimtu!

  Ndiyo haya haya ya culture of mediocrity na wallowing in a perpetual sea of impreciseness.
   
 12. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #12
  Dec 18, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Anye blog ni assistant (kijana wake) wake siyo MO Mwenyewe bana!....

  More rapid than eagles the flyers came out, They said “We’ll tow you if you don’t get out”
   
 13. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #13
  Dec 18, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Wewe ni mdau nini? Umejuaje?

  Huyu Mo ana undugu na Azim Dewji?
   
 14. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #14
  Dec 18, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hao MO wengine hawana Blog mwenye blog ni MO mmoja tuu Dewji...."check"....

  Mmh huko kwingine sina comment....mmh so yeye kusema amezaliwa Brooklyn imekuumiza roho au?...maana January alisema amekulia kijijini watu mkampiga dongo kuwa kukulia kijijini siyo sofa haya RM anasema amezaliwa Brooklyn watu nako mnaona Hatari!...sasa afanyeje jamani na pia hakumbuki ni watu wangapi amesaidia so far ili kutoumiza wengine kaona ni heri asiwataje majina wale wachache ikabidi ajibu ki uwingi...jaribu ku understand kidogo mtu ana maana gani...

  Na huyo aliye-mu-interview siyo Mo mwenyewe ana assistant wake mmoja huwa ana-interview watu mbali mbali...na huwezi kumfananisha na Larry king larry nimkongwe na hawa wameanza juzi mpe time.....
   
 15. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #15
  Dec 18, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nah miye siyo mdau ila ni mpita njia tuu.....

  sijui kamaanaundugu na Azim Dewji au ni jina tuu
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  Dec 18, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Sasa umejuaje ana msaidizi?
   
 17. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #17
  Dec 18, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Najua anamsaidizi wake ndiyo!....nina insider friends bana wameniambia
   
 18. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #18
  Dec 18, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Julius,

  Tofautisha mtu anapokuwa intentionally imprecise kama a tactic in politics na mtu anayepewa opportunity ya kuji-promote akashindwa kwa kuwa imprecise purposely.

  Wale wa Sunday talk shows wamewekwa pale kama pundits, na watu wanawaangalia kama vile wana crystal balls, na Marekani kauli ya mtu ina matter, ukisema hiki kitakuwa hivi halafu kisiwe, you are on record kwamba ulishindwa ku foresee. Kwa hiyo wale nawaelewa kwa nini wanakuwa imprecise sometimes.

  Huyu Ruge anaulizwa umemsaidia nani, anakwambia the whole industry! Mtu kapewa nafasi ya kuonyesha tangible results za kazi yake in a nuanced form, anakupa a vague, imprecise, half baked overgeneralization.

  Na huyu ndiye media mogul aliyezaliwa Brooklyn, sie wa kajamba nani tuliozaliwa Maneromango na MAlampaka tuki "Kanumba" utatucheka kweli?

  It's a national cancer, kuanzia hawa watu privileged kama Mo na Ruge mpaka huko kwingine ndiyo sitaki hata kusema, maana nitafanya ule mfano wa translation ya "Johannesburg" kuwa "Begi la Yohana" uonekane kama George Bernard Shaw.
   
 19. Binti Maringo

  Binti Maringo JF-Expert Member

  #19
  Dec 18, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 2,805
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0

  Oh well you never cease to amaze me dude...i am very spechless hapa maana hata ukiambiwa nini you got the answer!....wewe ungepewa hii opportunity ya kuw ainterviewd na Ruge na ukaulizwa same swali ungejibu vipi?!.....jifanye wew eruge and you know watu waliowasidia so far.....please!
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Dec 18, 2009
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Sasa wewe una assume kuwa hajawa imprecise kwa makusudi? Kama aliona si vyema kutaja majina ya watu binafsi je? Unless you tell me you were in his head there is no way you can conclude that he didn't give a nebulous answer on a purpose!
   
Loading...