Mahojiano ya Rais Magufuli na vyombo vya nje haya hapa. Nini mtizamo wako? Je, watanzania tujivunie?

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
30,406
54,885
Baada ya kuangalia interview za Tundu Lissu na kuzi-critique sana ni wakati wa kurejea interview ya Rais Magufuli.

Kwa bahati nzuri hii interview ni "two-in-one", kwasababu kuna wauliza maswali ya kiswahili na kiingereza.

Toka enzi za Baba wa Taifa kumekuwa na viwango na matarajio fulani kila Rais wa Tanzania anapozungumza huko nje.

Naomba tutafakari kama JPM aliitendea haki nafasi ya Rais wa Tanzania. Je, waTz tunaweza kutembea vifua mbele kwa jinsi JPM alivyotuwakilisha?

cc Pascal Mayalla, MsemajiUkweli, Mag3, BAK, Mpinzire, tindo
 
Hakuna mwenye akili timamu asiyejua kuwa Rais Magufuli sio polished politician kwa sababu naturally sio mwanasiasa.

Pamoja na kuwa sio mwanasiasa lakini huwezi kumsikia akisema sheria ya ushoga imevunja katiba ya Tanzania.

Suala la ushoga nchini ni taboo.

Tundu Lissu kwenda kwenye vyombo vya habari vya nje na kusema sheria ya kuzuia ushoga nchini imevunja katiba na kama atakuwa Rais wa nchi ataifuta ili tu aungwe mkono na nchi za magharibi ni suala kubwa sana nchini ambalo mwanasiasa mwenye akili timamu hawezi kulifanya.

Hoja sio kuhojiwa na kutoa kutoa majibu bali hoja ni majibu gani unayotoa ambayo yatainufaisha nchi yako kulingana na mazingira ya nchi.

Ushoga kwa Tanzania haukubaliki.
 
Suala la ushoga nchini ni taboo.

Tundu Lissu kwenda kwenye vyombo vya habari vya nje na kusema sheria ya kuzuia ushoga nchini imevunja katiba na kama atakuwa Rais wa nchi ataifuta ni suala kubwa sana nchini.

Hoja sio kuhojiwa na kutoa kutoa majibu bali hoja ni majibu gani unayotoa ambayo yatainufaisha nchi yako kulingana na mazingira ya nchi.

Ushoga kwa Tanzania haukubaliki.

..yeye ametoa TAHADHARI.

..sasa CCM kwasababu mna wabunge wengi ni jukumu lenu kwenda kukazia Katiba na Sheria zetu kuhusu suala la Ushoga.
 
Rais kimombo kinampiga chenga sana M7 alimsaidia sana aise aibu kubwa sana hii
..baada ya kuangalia interview za Tundu Lissu na kuzi-critique sana ni wakati wa kurejea interview ya Raisi Magufuli.

..kwa bahati nzuri hii interview ni "two-in-one", kwasababu kuna wauliza maswali ya kiswahili na kiingereza.

..Toka enzi za Baba wa Taifa kumekuwa na viwango na matarajio fulani kila Raisi wa Tanzania anapozungumza huko nje.

..naomba tutafakari kama JPM aliitendea haki nafasi ya Raisi wa Tanzania. Je, waTz tunaweza kutembea vifua mbele kwa jinsi JPM alivyotuwakilisha?

cc Pascal Mayalla, MsemajiUkweli, Mag3, BAK, Mpinzire, tindo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..yeye ametoa TAHADHARI.

..sasa CCM kwasababu mna wabunge wengi mna jukumu la kwenda kukazia Katiba na Sheria zetu kuhusu suala la Ushoga.
Watanzania wamejua kama Tundu Lissu atachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania atafuta sheria inayokataza ushoga kwa sababu inavunja katiba ya Tanzania.

Tundu Lissu ameenda mbele zaidi na kudai kuzuia ushoga ni kuipa serikali madaraka ya kuchungulia kinachofanywa ndani ya vyumba vya kulala.
 
..baada ya kuangalia interview za Tundu Lissu na kuzi-critique sana ni wakati wa kurejea interview ya Raisi Magufuli.

..kwa bahati nzuri hii interview ni "two-in-one", kwasababu kuna wauliza maswali ya kiswahili na kiingereza.

..Toka enzi za Baba wa Taifa kumekuwa na viwango na matarajio fulani kila Raisi wa Tanzania anapozungumza huko nje.

..naomba tutafakari kama JPM aliitendea haki nafasi ya Raisi wa Tanzania. Je, waTz tunaweza kutembea vifua mbele kwa jinsi JPM alivyotuwakilisha?

cc Pascal Mayalla, MsemajiUkweli, Mag3, BAK, Mpinzire, tindo

Mimi nimeshakubali kuwa Rais Magufuli si mzungumzaji mzuri.

Hivyo kumtegemea kuongea vizuri kwenye mahojiano au mkutano na waandishi wa habari ni kuwa na matarajio yasiyo ya/na uhalisia.

Na kwanza wala hakuteuliwa na chama chake na hakuchaguliwa na Watanzania ili awe amiri mzungumzaji mkuu.

Tatizo letu humu naona sasa tume-descend kwenye trivialities na kuacha kujadili mambo ya msingi.

Sasa imekuwa kama ni mashindano...nani anazungumza vizuri...sijui nani anawafuasi wangapi mtandaoni...nani kaongeza idadi ya wafuasi...na kadhalika.

Upuuzi mtupu.
 
Suala la ushoga nchini ni taboo.

Tundu Lissu kwenda kwenye vyombo vya habari vya nje na kusema sheria ya kuzuia ushoga nchini imevunja katiba na kama atakuwa Rais wa nchi ataifuta ni suala kubwa sana nchini.

Hoja sio kuhojiwa na kutoa kutoa majibu bali hoja ni majibu gani unayotoa ambayo yatainufaisha nchi yako kulingana na mazingira ya nchi.

Ushoga kwa Tanzania haukubaliki.
Naomba uitaje hio sheria ya ushoga ni ya mwaka gani na ni namba ngapi?
 
Mimi nimeshakubali kuwa Rais Magufuli si mzungumzaji mzuri.

Hivyo kumtegemea kuongea vizuri kwenye mahojiano au mkutano na waandishi wa habari ni kuwa na matarajio yasiyo ya/na uhalisia.

Na kwanza wala hakuteuliwa na chama chake na hakuchaguliwa na Watanzania ili awe amiri mzungumzaji mkuu.

Tatizo letu humu naona sasa tume-descend kwenye trivialities na kuacha kujadili mambo ya msingi.

Sasa imekuwa kama ni mashindano...nani anazungumza vizuri...sijui nani anawafuasi wangapi mtandaoni...nani kaongeza idadi ya wafuasi...na kadhalika.

Upuuzi mtupu.

..very good points.

..kwamba hutarajii azungumze vizuri.

..lakini hivi alivyozungumza amefikia matarajio yako hata kama ni madogo?
 
Rais ni lazima awe mahiri katika mambo mengi ya msingi ikiwa ni pamoja na kujua kujibu kwa weledi anacho ulizwa. Huwezi usitafute kazi hiyo
 
Watanzania wamejua kama Tundu Lissu atachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania atafuta sheria inayokataza ushoga kwa sababu inavunja katiba ya Tanzania.

Tundu Lissu ameenda mbele zaidi na kudai kuzuia ushoga ni kuipa serikali madaraka ya kuchungulia kinachofanywa ndani ya vyumba vya kulala.

..sawa.

..sasa ccm mnatakiwa mchukue hatua za tahadhari kwa kwenda bungeni na kukazia katiba na sheria ili ziende sawasawa ktk suala la ushoga.

..bila kufanya hivyo mtakuwa mnamuunga mkono Tundu Lissu na msimamo wake. Ukumbuke wakati anajibu swali hilo aliitaja serekali, and particularly Waziri wa mambo ya nje Dr.Mahiga.
 
..very good points.

..kwamba hutarajii azungumze vizuri.

..lakini hivi alivyozungumza amefikia matarajio yako hata kama ni madogo?

Magufuli kwangu si mgeni!

Nimeshamsikia akiongea mara nyingi sana.

Kumbuka, amekuwepo kwenye siasa za kitaifa katika nafasi mbalimbali tokea mwaka 1995!

Miaka karibu 24 hiyo.

Sikutegemea abadilike awe mtu mwingine ile 2015.

Wewe umeanza kumsikia lini?
 
Suala la ushoga nchini ni taboo. Tundu Lissu kwenda kwenye vyombo vya habari vya nje na kusema sheria ya kuzuia ushoga nchini imevunja katiba na kama atakuwa Rais wa nchi ataifuta ni suala kubwa sana nchini. Hoja sio kuhojiwa na kutoa kutoa majibu bali hoja ni majibu gani unayotoa ambayo yatainufaisha nchi yako kulingana na mazingira ya nchi. Ushoga kwa Tanzania haukubaliki.
Wizara ya Mambo ya Nje imesema kampeni iliyoanzishwa na RC Paul Makonda kukabiliana na ushoga ni mawazo yake binafsi na si msimamo wa Serikali

View attachment 921345

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inapenda kuwajulisha wananchi na jumuiya ya kimataifa kupitia vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi kuhusu masuala ya ushoga yaliyoongelewa na Mhe. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam hivi karibuni.

Katika mkutano wake na vyombo vya habari, Mhe. Mkuu wa Mkoa alitangaza kampeni ya kukabiliana na vitendo vya ushoga katika jiji la Dar es Salaam.

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ingependa kufafanua kwamba, hayo ni mawazo yake na sio msimamo wa Serikali.

Aidha, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ingependa kutumia nafasi hii kukumbusha na kusisitiza kwamba, itaendelea kuheshimu mikataba yote ya kimataifa inayohusu haki za binadamu ambayo imesaini na kuridhia.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaendelea na itaendelea kuheshimu na kulinda haki hizo kama zilivyo katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Imetolewa na:
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dodoma.
04 Novemba, 2018

MsemajiUkweli, mbona unajitoa fahamu? Alichosema Mh. Tundu Antiphas Lissu lina tofauti gani na msimamo wa Serikali kuhusu ushoga? Nafikiri lengo lako ni kututoa tu kwenye mada kama ilivyoletwa na JokaKuu. Habu chukua time, msikilize Rais John Pombe Magufuli akihojiwa huko Uganda halafu ulinganishe na Mh. Tundu Antiphas Lissu akihojiwa BBCHardtalk...ni hilo tu tafadhali!
 
Back
Top Bottom