Lucchese DeCavalcante
JF-Expert Member
- Jan 10, 2009
- 5,471
- 733
Mheshimiwa Joseph Mbilinyi, Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, awali ya yote mimi nikiwa mwakilishi wa Blog ya Mohammed Dewji, Mo blog, ninachukua nafasi hii kukupa pongezi kwa kuaminiwa na wananchi wa jimbo lako, Hongera sana.
MO BLOG : Unawezaje kuizungumzia safari yako ya siasa mpaka hapa ulipofikia katika hatua ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini?
MH SUGU: Kwanza ninachukua nafasi hii kuwashukuru wapiga kura wa Jimbo langu la Mbeya Mjini kwa kuniamini na kunichagua kwa kura nyingi kama ulivyosikia, lakini pia kazi hii ya uchaguzi kwangu na kwa wananchi wa Mbeya mjini imeandika Historia mpya, ambayo hakuna anayeweza kuivuruga.
Nikushukuru pia kwa kunipongeza kwa hatua hiyo, lakini pili ninaomba kukueleza kwamba hatua hii, sio siasa kwangu, bali ni harakati ya miaka 15 il.iyopita kupitia muziki, ambapo walizungumza na kulalamikia mambo kadhaa kuhusu Taifa yalizungumzwa.
Kimsingi ni kuwa tumeamua kuhamisha jukwaa la madai ya msingi kutoka katika muziki mpaka kwenye siasa, ambayo harakati zake zinaonekana kukubalika na kutekelezwa, na chombo hicho ni Bunge, hivyo jukwaa limehamia rasmi Bungeni.
Awali mambo yale ya muziki yalionekana kuwa ya kihuni tuliyazungumza kwenye majukwaa ya muziki, na waliopaswa kuyatekeleza hawakuchukua hatua kwa kuamini ni kama madai ya wahuni, lakini kwa sasa wajue kwamba mambo hayo ni rasmi katika chombo cha kutunga sheria, kwa maana tutayazungumza na kutaka hatua za kuchukuliwa kulingana na mahitaji ya jamii, kwani kwa pamoja hatukuzungumza mambo ya vijana ni malalamiko na mahitaji ya jamii kuhusu maendeleo.....
Fuatilia mahojiano zaidi kwa kutembea link hiii
Fuatilia mahojiano zaidi kwa kutembea link hiii