Mahojiano ya dk slaa na countyr fm(88.5), iringa jana usiku | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahojiano ya dk slaa na countyr fm(88.5), iringa jana usiku

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by PayGod, Oct 29, 2010.

 1. PayGod

  PayGod JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2010
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 1,255
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  MAHOJIANO YA DK SLAA NA COUNTYR FM(88.5)


  [​IMG]
  Mwandishi wa Chanel ten Iringa Daud Mwangosi (kushoto) akimhoji mgombea urais wa Chadema Dk Slaa
  [​IMG]
  Mgombea ubunge jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa (kushoto) akimsikiliza kwa makini mgombea urais wa Chadema Dk Slaa ambaye yupo Studio za Redio Country Fm sasa
  [​IMG]
  mgombea Urais kwa Chadema Dk Willibrod Slaa (kushoto) akijibu maswali ya mtangazaji wa kituo cha Redio Country Fm Bw Ahmed Meena ( Kulia)
  [​IMG]
  Mgombea urais wa Chadema Dk Willibrod Slaa akihojiwa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu katika kituo cha Redio Country fm waweza,Dk Slaa amesema akiingia Ikulu cha kwanza kuuza ndege ya Rais na kununua Helkopta kwa ajili ya matumizi ya Ikulu,

  Hata hivyo Dk Slaa amesema kuwa kamwe hata acha kuendelea kupambana na mafisadi kwa kuogopa kifo na kuwa kifo kipo kamwe hataacha kusema ukweli kwa kuogopa kifo na kuwa atakuwa tayari kuuwawa wakati wowote ila kamwe hatazibwa mdomo.

  UCHAKACHUAJI WA MAJINA YA WAPIGA KURA

  *Kuhusu wapiga kura ambao walijiandikisha katika daftari wa kudumu la wapiga kura ila majina yao hayomo kwenye orodha ,Dk Slaa ametoa muda wa siku mbili zilizobaki kwa tume ya Taifa ya uchaguzi (NEC) kuyarejesha ama kuomba radhi watanzania kwa wizi huo vinginevyo malalamiko yatafikishwa umoja wa mataifa .

  Awataka watanzania ambao walijiandikisha ila majina yao hawayaoni waonane na wagombea udiwani na wale wa ubunge wa majimbo yao ili waweze kutuma taarifa kwake kwa ajili ya kuchukua hatua zaidi.

  KILIMO KWANZA/KIFO CHA DK BALALI

  > Abeza kauli mbinu mbali mbali zinazotolewa na serikali iliyopo madarakani dhidi ya kilimo kwanza kuwa ni kauli zisizo tekelezeka .

  KIFO CHA BALALI

  Pia aulizwa kuhusu kifo cha aliyekuwa gavana wa Benk kuu ya Tanzania Dk Daud Balali kama kweli alikufa ama lah .

  Akijibu swali hilo lililoulizwa kwa njia ya simu Dk Slaa amesema kuwa hata yeye bado yupo njia panda juu ya kifo cha mtuhumiwa huyu wa fedha za EPA kwani alipata kuona picha yake katika gazeti .

  MICHEZO

  Dk Asema kuwa chuo cha Sanaa cha bagamoyo kitakuwa ni chuo kikuu cha michezo iwapo ataingia Ikulu

  Asema kuwa michezo ni ubalozi kwa Taifa letu na ni sehemu ya kukuza utalii pamoja na uchumi kwa Taifa .

  Dk Slaa amesema kuwa lazima chuo hicho kiwe chuo chenye hadhi nzuri kitakachovutia wengi katika kuja kujifunza Tanzania.

  UKIMWI

  Mimi tofauti na Rais Jakaya Kikwete ambaye anasema kuwa UKIMWI unapatikana kwa uzembe ,ila mimi kwanza nitumiea nafasi hii kuwaomba radhi watanzania kwa unyanyapaa huo wa Rais wetu Kikwete badala ya kuwapa pole wagonjwa wa UKIMWI kwa kuwaita wana kihele hele.

  "Mimi ni mmoja kati ya wanaharakati wa masuala la UKIMWI hivyo nipo radhi kuendelea kuwafariji wagonjwa wa UKIMWI na pia ipo sheria ya kuwahudumia watu wenye UKIMWI pamoja na kutengeneza mbinu ya kusaidia wenye UKIMWI"

  Asema kuwa fedha nyingi za UKIMWI zimekuwa zikiliwa na wajanja na kuwa watu wenye UKIMWI wamekuwa hawafikiwi kabisa na fedha hizo za UKIMWI.

  Dk Slaa amesema kuwa serikali yake itaendelea kuwaenzi watu wenye UKIMWI kwa kuanzisha Hospitali maalum ya kuwasaidia watu hao wenye VVU na kuwa hajapendezwa na serikali kuwaita wenye UKIMWI kuwa wana kihelehela.

  Malaria


  Asema serikali ya CCM inafanya usanii kuhusu vyandarua kwa wananchi wake japo fedha hizo zimetolewa na nchi za nje japo kwa upande wake katika jimbo la Karatu japo hakuwa Rais ila bado ameweza kutoa neti kwa kila kitanda katika kaya tofauti na CCM inavyotoa Neti mbili kwa kaya bila kujali idadi ya watu waliopo .

  Adai kuwa Mradi uliofadhiliwa na Japan ulipata kutoa fedha kwa ajili ya kuua mbu ila serikali ya CCM imekula fedha hizo na sasa kuendelea kuwadanganya wananchi kwa neti ili kuendelea kuichagua CCM.

  Asema kuwa serikali yake itaendelea kupambana na ugonjwa wa Malari bila kufanya usanii na kuwa kila kitanda kitapewa neti kama ilivyo katika jimbo la Karatu.

  UKUBWA WA BARAZA LA MAWAZIRI


  Asema kuwa baraza kubwa la mawaziri Tanzania linachangia matumizi mabaya ya fedha za umma na kuwa katiba itakayoundwa ya serikali ya Chadema itazingatia mambo nyeti na kuwa kamwe baraza la mawaziri halitakuwa kubwa kama la baraza la JK ambalo lipo kwa ajili ya kujitengenezea ulaji kwa kwa marafiki wa jirani.

  Asema bado katiba yetu haitamki wazi juu ya mgawanyo wa bunge,mahakama na n.k na kuwa ndio sababu ya kuwepo kwa matamko tofauti tofauti kwa kila kiongozi .

  Dk Slaa asema kuwa katiba ya sasa bado haifai kabisa kwani hata suala la kumchagua Monica Mbega kuwa mkuu wa mkoa ni suala la kuwakomoa wananchi wa jimbo la Iringa mjini.

  "Nasema kuwa Iringa mmepata bahati mbaya kweli kwani muda wa kuwatumikia vema wananchi haupo"

  Dk Slaa asema kuwa kuna hofu kuwa Tanzania itakuja kuongozwa na Rais ambaye atashinda kwa kura moja kutokana na njama za CCM za kuivuruga katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.

  FEDHA ZA KIFISADI.

  Fedha hizo zinapoingia katika mfumo wa matumizi ya fedha za serikali uchumi wa nchi unaendelea kushuka na kuwa hofu zaidi taifa litaendelea kuwa chini kiuchumi.

  Asema kuwa iwapo fedha hizo za ufisadi zitashindwa kuthibitiwa kuna uwezekano wa Taifa kuendelea kuyumba .

  KWANINI Mchungaji Msigwa anafaa kuwa mbunge


  Asema kuwa wananchi wa jimbo la Iringa mjini wasifanye kosa katika kuchagua Chadema kwa tafsiri ya mafiga matatu na kuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo Msigwa anasifa za kutosha kuwa mgombea ambaye atafanya maajabu makubwa .

  Dk Slaa anasema kuwa kila anapopita katika Tanzania wananchi wengi wana endelea kutoa imani kwa Chadema .

  MSIGWA.
  Kesho asubuhi kutakuwa na mkutano wa kampeni katika uwanja wa mwembetogwa na kuwaomba wananchi kutoa kura zao Chadema kwa Dk Slaa.

  Mgombea udiwani kata ya Makorongoni David Kombo

  Asema kuwa kamwe akipata udiwani katika jimbo hilo kamwe hatawaanusha na atafanya kazi kwa nguvu zote.

  Mke wa Dk Slaa

  Awataka wananchi kutoaogopa kumchagua Dk Slaa na kuwa wananchi watoe nafasi zaidi
   
Loading...