Uchaguzi 2020 MAHOJIANO: Tundu Lissu na VOA ya kusimamishwa kampeni na NEC, anakubaliana na Magufuli kuhusu COVID19

kasenene

JF-Expert Member
Jun 6, 2008
1,447
2,000
Mambo aliyoyaongea

Amesema anaendelea vizuri na kampeni zake, wanasema anakosea kwa kuwa anaongea ukweli lakini kwa sababu anayoyaongea ni ya ukweli anashindwa kuitwa kwenye maeneo ya kumuuliza kuhusu anayoyaongea

Aidha mtangazaji aliuliza kuhusu uchaguzi kuwa huru na haki kutokana na mfumo ulivyo

Amesema hawawezi kususia uchaguzi kutokana na mifumo iliyopo kwani hauwezi kumuachia nyani shamba, demokrasia inapiganiwa. Mbali na mfumo wa uchaguzi kuwa tofauti lakini wana haja ya kugombea ili kuutoa mfumo huu

Swali kuhusu watu kumuunga mkono, Rais Magufuli kutokana na mambo makubwa kama kujenga miundo mbinu na kujenga mahusiano

Amulizwa anapingaje hayo mazuri
Lissu amejibu: Hiyo miradi ambayo ameifanya haihalalishi ukandamizaji mkubwa na uharibifu wa uchumi ambao ameufanya kwa miaka mitano. Ametoa mfano wa Ethiopia kuwa na shirika kubwa la ndege lakini raia wake wamekuwa wakikamatwa nchi mbalimbali kwamba wanakimbia nchi yao kutokana na kukosekana na uhuru

Kwa hiyo miundombinu haimpi Magufuli kupendwa, kila mtu anailalamikia kwa kuwa watu wanahitaji kuzungumza, kubadilishana mazawzo na kujadili

Swala la Magufuli kupambana na rushwa

Lissu amejibu: Kuwa ni uwongo kwa kuwa kama angekuwa anapinga rushwa asingejenga uwanja wa ndege kwa kutumia kandarasi ambaye wameoa sehemu moja na amemfanya mtoto wa dada yake kuwa mlipaji mkuu

Amesema rushwa imehamia ikulu ya Magufuli. Amesema wapo waliokamatwa kwa makosa ya uhujumu uchumi lakini wanamnadi kama mgombea wa jimbo moja huko Njombe

Ajibu hoja ya uwanja wa ndege wa Chato kwa kuwa Nyerere na Mkapa hawajajenga Viwanja vya taifa kwao

Mtangazaji ameuliza kuhusu CHADEMA na sera ya mambo ya nje

Lissu amejibu: Amesema wamezungumza sana kuhusu Magufuli kuharibu mahusiano basically na dunia nzima, rafiki pekee tuliye naye ni Burundi

Kwa hiyo serikali ya Chadema itarudisha mahusiano na nchi zote, kwa kuwa chadema hawana adui

Mtangazaji ameuliza, msimamo wa Lissu kuhusu COVID19 kwa kuwa hawafuati miongozo ya kiafya

Amejibu: Nchi za kiafrika hazijapiwa na Covid19 kama nchi nyingine, nchi pekee iliyopigwa na covid19 ni afrika kusini, kwa hiyo covid19 sio tishio kwa nchi zetu kama ilivyo kwa nchi za Ulaya

Amekubali kuwa hali ya corona sio mbaya, sio kwa Tanzania tu, bali kwa nch zote za kiafrika,

Kwa hilo amekiri kukubaliana na Magufuli, lakini anakataa kuwa Magufuli ndio aliikimbiza covid19 wakati kimsingi alijificha kwa wiki sita

Ktk kumalizia
Amesema serikali ya chadema itastawisha uhuru wa habari uhuru wa mahakama nk
 

digba sowey

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
4,846
2,000
Huyu milembe walikosea sana kumruhusu aondoke maana nikiangalia kwa mbali bado naona kuna shida kwenye akili yake.

Eti anasema watanzania maelfu kwa maelfu wanahudhuria mikutano yake hivyo anaamini kuwa wote wanao kuja kwenye mikutano yake lazima wampigie kura,huyu mtu ni wa kupimwa akili,maelfu kwa maelfu wakati wapiga kura wako mamilioni kwa mamilioni,sasa hao maelfu wanatosha kumpa ushindi dhidi ya mamilioni wa CCM? Jibu ni hapana

Huyu mtu kwa waliokaribu yake wanapaswa wamuambie kuwa si kila anayeenda kwenye mikutano yake ni mfuasi wake wengine wanakuja kuangalia mashavu yake yalivyonenepeana,mimi binafsi nimehudhuria mikutano ya Lissu zaidi ya Mara nne lakini mimi si mfuasi wake na nilitumia nauli kubwa kuhufutilia mikutano yake katika mikoa mitatu lakini hata kama jua litabadili uelekeo Leo siwezi mpa kura yangu lissu

Aache kupotosha huyu bwana,waliomtuma awaambie watanzania wamemshitukia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom