Mahojiano na Mzee Joseph Mfugale; Toka fundi seremali mpaka kumiliki Peacock Hotel - live

B

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Messages
5,998
Points
2,000
B

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined Jan 14, 2010
5,998 2,000
August 2012
Dar-es-Salaam, Tanzania

Mzee Joseph Mfugale began his career as a carpenter in 1967. Although his formal schooling ended after the sixth grade, he went on to run two dry-goods stores, which qualified him for a $30,000 loan from the Tanzanian National Bank of Commerce.

In 1992, Mfugale opened the 27-room Peacock Hotel. In 2006, he self-financed and opened 66 additional rooms and in 2007, Mfugale secured a $2 million loan from the East Africa Development Bank to build an additional 75 luxury suites, a conference center and a spa, Ebony FM Radio/Tv Iringa.

Working with his son, Damasi, Mfugale also secured from the government the operating lease for the Millennium Hotel, an upscale hotel on the outskirts of the Dar es Salaam center. This new property is the Mfugales' first step toward branding the Peacock Hotel as a quality hotel chain.

As part of their company's growth plan, the Mfugales' next step is to develop a luxury hotel and resort on beachfront property on the Kigamboni peninsula near Dar es Salaam. The Mfugales purchased the Kigamboni plot from the government for $100,000. If they don't begin construction by August 2009, the government can exercise its right to take back the land. The Mfugales have also targeted two other areas for hotels: Iringa, southwest from Dar es Salaam, and Arusha, a safari hot spot near Kilimanjaro.

Damasi Mfugale, who earned his MBA from the University of Lausanne in Switzerland and worked for the Omni Hotel in North Carolina and the Savoy in London, plans to move the Peacock Hotel brand into its next growth phase before his father retires.

Video Mzee Joseph Mfungale anaelezea live toka alipoanza ngazi ya 'umachinga' mpaka alipofika hapa , labda mahojiano haya yatatoa mwanga wa kuanzisha biashara ndongo na kuikuza kuwa ya kiwango cha mabilioni ya shillingi bahati ikiwa kwako:

video kwa hisani ya EASB
 
Last edited by a moderator:
CHASHA FARMING

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined
Jun 4, 2011
Messages
6,431
Points
2,000
CHASHA FARMING

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined Jun 4, 2011
6,431 2,000
Ya hawa ndo type ya wakina Muguku, ndo maana siku zote nasema na nitarudia kusmea, UJASIRIMALI ni Mgumu sana na unhitaji uvumilivu wa hali ja juu, Ujasirimali si lele mama, Ila kuwa mfanya biashara ni rahisi sana, haitaji akili ya ziada
 
T

tulizo 2

Member
Joined
Dec 7, 2012
Messages
24
Points
45
T

tulizo 2

Member
Joined Dec 7, 2012
24 45
Ya hawa ndo type ya wakina Muguku, ndo maana siku zote nasema na nitarudia kusmea, UJASIRIMALI ni Mgumu sana na unhitaji uvumilivu wa hali ja juu, Ujasirimali si lele mama, Ila kuwa mfanya biashara ni rahisi sana, haitaji akili ya ziada
Du hapo ndo tunaona hakuna mpaka wa mafanikio ya binaadamu,ni kumuomba MUNGU na kuongeza juhudi tu.
 
Jodoki Kalimilo

Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2012
Messages
10,071
Points
2,000
Jodoki Kalimilo

Jodoki Kalimilo

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2012
10,071 2,000
Ya hawa ndo type ya wakina Muguku, ndo maana siku zote nasema na nitarudia kusmea, UJASIRIMALI ni Mgumu sana na unhitaji uvumilivu wa hali ja juu, Ujasirimali si lele mama, Ila kuwa mfanya biashara ni rahisi sana, haitaji akili ya ziada
Umeelezea vizuri sana kuhusu hizi concepts maana siku hizi kila mtu anakuambia yeye ni mjasirimali bila kuelewa mjasirimali ni sifa ya ziada baada ya kuweza kumudu mikikimiki mbalimbali katika shughuli yako pia kuwa mbunifu ili biashara yako iende na hali halisi ya soko kwa wakati huo
 
CHASHA FARMING

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined
Jun 4, 2011
Messages
6,431
Points
2,000
CHASHA FARMING

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined Jun 4, 2011
6,431 2,000
Mkuu ujasirimali unakuwa Mgumu sana kwa sababu, unatumia zaidi akili zanko, Uvumilivu, Ujuzi, na kazalika, ukiangalia Safari ya Wajasirimali wote Duniani utagundua kwamba ni safari moja ngumu sana lakini yenye mafanikio makubwa sana mbeleeni, na mara nyingi kwenye ujasirimali matunda huja kuonekana baadae sana na huwa ni matunda yasio isha kiurahisi,

Ujasirimali ni tofauti na mimi leo ni na mtaji nataka kuanza kuagiza magari japani na kuuza, hapa kwa kweli haitaji akili nyingi bali pesa tu, ila ni tofauti na wanao tengeneza hayo magari kama TOYOTA ambao saazingine uatakuta hawalali wakikesha kutafuta mbinu mpya,

Na mara zote MJASIRIMALI ukimhoji baada ya mafaniko atakuambia hakutegemea kufika hapo siku moja, hata leo hii ukienda kuwahoji wakina Mengi au jamaa wa Azam watakuambia wakiwa watoto hawakutegemea kama siku moja wangekuja kuwa hapo walipo leo, ila kutokana na juhudi zao na jamii kutambua mchango wao ndo maana wako hapo walipo leo,

Ni tofauti na watu tunao danganayana humu kwa kuuliza na ni Biashara zipi zinalipa na zipi hazilipi, kiukweli huwezi na hutakaa ufanikiwe kwa mtindo huu, tunaingia kwenye biashara kusaka utajiri kitu ambacho ni makosa makubwa kabisa,na mwisho wa hili ni mfanya biashara kuishia kufanya ujanja, kukwepa kodi, kuzalisha bidhaa na huduma ya chini ya kiwango kisa tu anatafuta utajiri, unaweza upata lakini hautakuwa sustainable hata siku moja,

Biashara nzuri ni ile inayo rithiwa vizazi na vizazi, hata leo ukifa Aidea yako itaendelea kufanya kazi, lakini cheki biashara za kisanii, ukifa tu ndo mwisho wa kila kitu na unasahaurika baada ya mwezi, Ila watu kama HONDA, wakian Michael Dell, wakina Thomas Edson, wakina Stevu, walisha kufa lakini familia zao ziatendelea kuenjoy matunda ya kazi zao kwa karne nyingi sana,

So wakuu Ujasirimali si kazi nyepesi kama tunavyo danganywa na hata wanasiasa, na ndo maana Dunia ina wajasirimali wachache sana na wafanya biashara ndo tuko wengi sana na wachuuzi,
 
Ulukolokwitanga

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2010
Messages
8,416
Points
2,000
Ulukolokwitanga

Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Joined Sep 18, 2010
8,416 2,000
Hii stori ni ya zamani. Uki update kidogo na kuweka Version 2012 utatusaidia sana wengine kujifunza toka kwa Mfugales, the Self Made Millionaires...

By the way i know the guys, they really mean Business
 
bluetooth

bluetooth

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2011
Messages
4,153
Points
2,000
bluetooth

bluetooth

JF-Expert Member
Joined Jan 12, 2011
4,153 2,000
huyu mtu ni kichwa ... a real entreprenuer
 
Tusker Bariiiidi

Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2007
Messages
5,224
Points
2,000
Tusker Bariiiidi

Tusker Bariiiidi

JF-Expert Member
Joined Jul 3, 2007
5,224 2,000
Ila kwa sasa Millenium Towers Peacock imefungwa zaidi ya mwaka sasa.
 
B

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2010
Messages
5,998
Points
2,000
B

bagamoyo

JF-Expert Member
Joined Jan 14, 2010
5,998 2,000
Ni kweli ujasiri-mali ni lazima uwe 'mgumu-wa-roho' maana unaanzia mbali sana na sisi vijana tunataka 'kuibuka' vuu bin vuu na vogue Range Rover badala ya kuongeza tena mtaji.
 
Mwanahisa

Mwanahisa

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2012
Messages
1,395
Points
1,195
Mwanahisa

Mwanahisa

JF-Expert Member
Joined Jun 29, 2012
1,395 1,195
Ila tusisahau lazima haya mambo uwe umeazimia kichwani,
Utashi na matamanio yanaanzia kwenye ubongo, lazima uufunze ubongo wako kukiri kile unachokiamini ili kitokee. Ukimuuliza huyu mzee wetu alianza lini kujenga hiyo hoteli yake ya kwanza, utastajabu kua alikua na hilo wazo na jina la hoteli tangu kitambo sana, akaufundisha ubongo wake na akaamini kwa nia na nguvu ndio kikatokea. Ni lazima kua na mawazo mapana sana hata kama utakua unauza genge la mboga mboga za majani.
 
Husninyo

Husninyo

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2010
Messages
23,823
Points
2,000
Husninyo

Husninyo

JF-Expert Member
Joined Oct 24, 2010
23,823 2,000
ngoja niendelee na huu umamantilie kwa bidii zote labda cku moja mambo yatakuwa sukari.
 
Kingdom_man

Kingdom_man

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2010
Messages
406
Points
500
Kingdom_man

Kingdom_man

JF-Expert Member
Joined May 19, 2010
406 500
Mkuu ujasirimali unakuwa Mgumu sana kwa sababu, unatumia zaidi akili zanko, Uvumilivu, Ujuzi, na kazalika, ukiangalia Safari ya Wajasirimali wote Duniani utagundua kwamba ni safari moja ngumu sana lakini yenye mafanikio makubwa sana mbeleeni, na mara nyingi kwenye ujasirimali matunda huja kuonekana baadae sana na huwa ni matunda yasio isha kiurahisi,

Ujasirimali ni tofauti na mimi leo ni na mtaji nataka kuanza kuagiza magari japani na kuuza, hapa kwa kweli haitaji akili nyingi bali pesa tu, ila ni tofauti na wanao tengeneza hayo magari kama TOYOTA ambao saazingine uatakuta hawalali wakikesha kutafuta mbinu mpya,

Na mara zote MJASIRIMALI ukimhoji baada ya mafaniko atakuambia hakutegemea kufika hapo siku moja, hata leo hii ukienda kuwahoji wakina Mengi au jamaa wa Azam watakuambia wakiwa watoto hawakutegemea kama siku moja wangekuja kuwa hapo walipo leo, ila kutokana na juhudi zao na jamii kutambua mchango wao ndo maana wako hapo walipo leo,

Ni tofauti na watu tunao danganayana humu kwa kuuliza na ni Biashara zipi zinalipa na zipi hazilipi, kiukweli huwezi na hutakaa ufanikiwe kwa mtindo huu, tunaingia kwenye biashara kusaka utajiri kitu ambacho ni makosa makubwa kabisa,na mwisho wa hili ni mfanya biashara kuishia kufanya ujanja, kukwepa kodi, kuzalisha bidhaa na huduma ya chini ya kiwango kisa tu anatafuta utajiri, unaweza upata lakini hautakuwa sustainable hata siku moja,

Biashara nzuri ni ile inayo rithiwa vizazi na vizazi, hata leo ukifa Aidea yako itaendelea kufanya kazi, lakini cheki biashara za kisanii, ukifa tu ndo mwisho wa kila kitu na unasahaurika baada ya mwezi, Ila watu kama HONDA, wakian Michael Dell, wakina Thomas Edson, wakina Stevu, walisha kufa lakini familia zao ziatendelea kuenjoy matunda ya kazi zao kwa karne nyingi sana,

So wakuu Ujasirimali si kazi nyepesi kama tunavyo danganywa na hata wanasiasa, na ndo maana Dunia ina wajasirimali wachache sana na wafanya biashara ndo tuko wengi sana na wachuuzi,
watu wenye akili kama wewe wamebaki wachache sana. Well said
 
N

nyabaheta

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2012
Messages
248
Points
0
N

nyabaheta

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2012
248 0
Wadau,mimi nadhani hawa matajiri wetu huwa hawatoi siri zao zote,kwa sehemu kubwa tunapeana matumaini feki,kwamba kama sina elimu naweza kufanikiwa.
So far huyu mzee ni wa pili kumsikia baada ya Bakhresa kwamba ni watu waliotoka kimaisha lakini hawana shule,lakini tuna uhakika kuwa kinachosemwa kuhusu wao ni kweli?kwamba walianza hivyo walivyoanza au kuna dili chafu walipiga pembeni wakafika hapo walipo,tuambiane ukweli.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
akohi

akohi

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2012
Messages
782
Points
250
akohi

akohi

JF-Expert Member
Joined Jul 13, 2012
782 250
Hakuna anaeweza kutoka bila kupiga deal, tusidanganyane nadhani tatizo kubwa hapa ni namna ya kuendeleza Kile ulichonacho maana binafsi naona kuna mambo makubwa manne
.
1. Kuna Wale wenye uwezo wa kufanya biashara Ila tatizo mtaji.
2. Kuna Wale wenye mtaji Ila hawana uwezo au skills za kibiashara
3. Au hana vyote viwili kwa maana ya skills na mtaji
4. Na wenye vyote viwili kwa maana Ana mtaji na uwezo wa kusimamia biashara.

Hao tunaowasema Leo lazima walikua na kianzio (mf: morgage) na mbeleni wakakopa bank au wamesaidia na ndugu jamaa au marafiki na ndo Leo wako hapo Ila sio Rahisi kuanza na kuku watano halafu unasema iko siku utakuwa Kamba Mengi hehehe.

Binafsi nashauri tusifikilie Kuwa matajiri maana itatuweka katika matatizo. Fanya shuguri zako kwa imakini na ishi maisha ya kawaida tu, mtaji utakuwa wenyewe kadri siku zinavyozidi maana changamoto za maisha ni nyingi sana.
Google chat: alfredmkohi
 
M

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Messages
4,527
Points
2,000
M

Malila

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2007
4,527 2,000
ngoja niendelee na huu umamantilie kwa bidii zote labda cku moja mambo yatakuwa sukari.
Njoo uwahi kiwanja hapa Rhino cement, nimepata u-supervisor pale nitakupigia pande uwe unahudumia VIP lounge yetu.
 
CHASHA FARMING

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined
Jun 4, 2011
Messages
6,431
Points
2,000
CHASHA FARMING

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined Jun 4, 2011
6,431 2,000
Hakuna anaeweza kutoka bila kupiga deal, tusidanganyane nadhani tatizo kubwa hapa ni namna ya kuendeleza Kile ulichonacho maana binafsi naona kuna mambo makubwa manne
.
1. Kuna Wale wenye uwezo wa kufanya biashara Ila tatizo mtaji.
2. Kuna Wale wenye mtaji Ila hawana uwezo au skills za kibiashara
3. Au hana vyote viwili kwa maana ya skills na mtaji
4. Na wenye vyote viwili kwa maana Ana mtaji na uwezo wa kusimamia biashara.

Hao tunaowasema Leo lazima walikua na kianzio (mf: morgage) na mbeleni wakakopa bank au wamesaidia na ndugu jamaa au marafiki na ndo Leo wako hapo Ila sio Rahisi kuanza na kuku watano halafu unasema iko siku utakuwa Kamba Mengi hehehe.

Binafsi nashauri tusifikilie Kuwa matajiri maana itatuweka katika matatizo. Fanya shuguri zako kwa imakini na ishi maisha ya kawaida tu, mtaji utakuwa wenyewe kadri siku zinavyozidi maana changamoto za maisha ni nyingi sana.
Google chat: alfredmkohi

Wewe hujui unacho ongea,UTAJIRI SIKU ZOTE NI MATOKEO, hata hao leo hii ukiwauliza watakumbia hawakutegemea kuwa hapo walipo,
-So unabisha huwezi anza na kuku wa tano mwisho wasiku ukaja kuwa bilonare?

- Wewe unazania kuwa bilionare ni mpaka uanze na kuku wangapi?

- Na unachamganya mambo hapa, Mkuu Entreprenership ni strategies, huwezi kuwa na spirit ya Ujasirimali halafu ushindwe kuanzisha biashara, wewe unazungumzia biashara za kuchuuza,

- Haijarishi ulianza vipi lakini kinacho takiwa ni matoke,

- Yule jamaa wa Kenya Muguku, alisaidia na baba yake pesa za kununua hao kuku wasio zidi kumi, ila mwisho wa siku akaja kuingia kwenye Orodha ya matajiri wakubwa wa kenya na mtu pekee Kenya nzima mwenye share nyingi kwenye Equite Bank ukiachilia makampuni mengine,

So si kila mtu ni amepiga dili, watu wana determination, sio usanii

NA MWISHO NI KWAMBA, ENTREPRENERSHIP SKILLS HAIFUNDISHWI MAHALI POPOTE PALE, WEWE UNAZUNGUMZIA SKILLS ZIPI
?

-
 
Kubota

Kubota

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2012
Messages
533
Points
250
Kubota

Kubota

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2012
533 250
Suala hapa siyo jinsi mtu alivyopata mtaji, maana kila mtu hupata mtaji kivyake! Suala ni pale watu wanapokuwa na fursa za kupata mtaji lakini hawazitumii kuwa matajiri, mfano wafanyakazi na wasomi wengi pesa nyingi sana zinapita mikononi mwao lakini ni masikini, wakulima wa Tumbaku pesa nyingi zinapita mikononi mwao, kwenye machimbo ya madini kadharika, na hata wajasiria mali wengi wanapata pesa nzuri tu lakini hawakui na kuwa matajiri! Ili kuwa matajiri tujifunze nyendo zao kuna mengi wanayofanya ambayo yanawafanya wawe hivyo ambavyo wengine hawafanyi ndiyo maana hawatajiriki! Bahati hutokea kwa wale ambao wako ulingoni tayari. Kudhania tu kuwa eti utajiri ni matokeo ya uchawi au madili machafu tu hapo ni kutafuta majibu rahisi kwa swali GUMU kama hili la kutaka kuwa tajiri! Utajiri ni muziki mnene acheni matajiri waitwe matajiri!

Wadau,mimi nadhani hawa matajiri wetu huwa hawatoi siri zao zote,kwa sehemu kubwa tunapeana matumaini feki,kwamba kama sina elimu naweza kufanikiwa.
So far huyu mzee ni wa pili kumsikia baada ya Bakhresa kwamba ni watu waliotoka kimaisha lakini hawana shule,lakini tuna uhakika kuwa kinachosemwa kuhusu wao ni kweli?kwamba walianza hivyo walivyoanza au kuna dili chafu walipiga pembeni wakafika hapo walipo,tuambiane ukweli.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Kubota

Kubota

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2012
Messages
533
Points
250
Kubota

Kubota

JF-Expert Member
Joined Oct 21, 2012
533 250
Ila tusisahau lazima haya mambo uwe umeazimia kichwani,
Utashi na matamanio yanaanzia kwenye ubongo, lazima uufunze ubongo wako kukiri kile unachokiamini ili kitokee. Ukimuuliza huyu mzee wetu alianza lini kujenga hiyo hoteli yake ya kwanza, utastajabu kua alikua na hilo wazo na jina la hoteli tangu kitambo sana, akaufundisha ubongo wake na akaamini kwa nia na nguvu ndio kikatokea. Ni lazima kua na mawazo mapana sana hata kama utakua unauza genge la mboga mboga za majani.
Mwanahisa nakubaliana na wewe! Utajiri wanaoutamani wengi ni ule wa kumea na kukua kama uyoga! Bahati mbaya utajiri wa aina hiyo huwa haudumu, hauna foundation, ni mfano wa kujenga ghorofa refu lenye msingi mwembamba. Utajiri huwa na msingi mnene na hukua kama ilivyoanza mbegu ya msufi au mbuyu ni ndogo kama mbegu ya bamia! Ni suala la kuwa na subira, uvumilivu na nidhamu ya hali ya juu! Ni suala la kujifunza daima kutokana na hasara na maanguko mengi yatokeayo ambayo kwa wengine wengi hukimbia mapambano! To be rich is a life long process, utajiri kuna miiko mingi ya kuijua na matajiri wengine wamefundishwa hayo ama walizaliwa na maono hayo!

Hata kama matajiri hawakuwahi kudhani wangefika hapo walipo leo lakini walikuwa na ndoto au kiu ya kufika hatua kubwa zaidi! Tusikae kufikiri tu kuwa mambo yatatokea yenyewe tu bila kudhamiria, kupanga na kuamua kuchukua hatua!
 
CHASHA FARMING

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined
Jun 4, 2011
Messages
6,431
Points
2,000
CHASHA FARMING

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined Jun 4, 2011
6,431 2,000
True, Watu wengi huwa hatuna foundation ya Biashara zetu, watu hutafuta Utajiri wa fasta fasta, kwa njia mabzao huwa si nzuri ikiwemo, Kuuza vitu fake, kuwapunja wateja, kuchakachua, kupandisha bei na kazalika, na hii ni ili tu atajirike, Biashara zisizo kuwa na foundation hufa mara tu mwenye nayo anapo either kufa au kuugua, na hii ni kwa sababu biashara yake haikuweka msingi mzuri,

Na aina ya hizi biashara tunazo fanya sio endelevu kwa sababu dunia ya sasa ina competition kubwa sana ya ndani na nje ya Nchi
 
Forum statistics

Threads 1,285,938
Members 494,834
Posts 30,879,769
Top