Mahojiano maalum na mkurugenzi wa Zoa Zoa, Dkt. Elizabeth

Ambakucha

JF-Expert Member
Aug 16, 2019
277
445
MAHOJIANO MAALUM NA MKURUGENZI WA ZOA ZOA, DK. ELIZABETH

Mwishoni mwa wiki, wana habari walifanya mazungumzo ya dakika arobaini na tano (45) na Mkurugenzi Mtendaji wa Grace Product Limited, watoaji wa bidhaa za Zoa Zoa, Dk. Elizabeth Kilili.

Katika mahojiano hayo yaliyolenga kujua ukuaji wa bidhaa zake, utoaji wa ajira kwa Watanzania na malengo, Dk. Elizabeth alionekana kuguswa zaidi na tatizo la ajira kwa Watanzania.

Awali, alipoulizwa kama mwaka 2022 ana bidhaa yoyote mpya, alisema:

"Tumetoa dawa ya meno, inaitwa Zoa Zoa ya Meno. Hii ni bidhaa yetu mpya kabisa na imetengenezwa na mimea asili ya hapa nyumbani Tanzania, ukiwemo mmea wa Alovera (Shubiri).

"Dawa hii, ni nzuri kwani kinywani haikai kama chokaa na wala haina chengachenga zinazobakia baada ya kupiga mswaki kama baadhi ya dawa zilivyo.

"Inatakiwa kutumiwa kwa siku mara tatu. Kila baada ya mlo mkuu, unapiga mswaki na Zoa Zoa ya Meno, matokeo yake ni meno kuwa meupe sana na huondoa harufu, hasa kwa wale watu wenye harufu sugu kinywani."

Swali: "Hii Zoa Zoa ya Meno inakuwa bidhaa ya ngapi miongoni mwa bidhaa zote za Grace Products?"

Dk. Elizabeth: "Ni ya kumi na mbili. Tuna sabuni za kuogea, mafuta ya nywele, losheni, shampoo, sabuni ya kuoshea uso, mafuta ya watoto wadogo nakadhalika."

Swali: "Zoa Zoa imeajiri Watanzania wangapi?"

Dk. Elizabeth: "Hilo la ajira ndilo lilitusukuma kupanua wigo wa bidhaa zetu, kwani tuliamini kampuni ikiwa kubwa, ajira zitakuwepo kwa kiasi fulani kwani ajira ni changamoto sana katika jamii.

"Kwa hiyo vijana wenye ajira za kudumu Ni sabini na tano (75). Lakini pia tuna vibarua ambao bado hawajaingia kwenye ajira ya kudumu kutokana na sifa. Watakapofikia, nao wataajiriwa."

Swali: Bidhaa zenu zinapitia kwenye mamlaka husika?"

Dk. Elizabeth: "Hiyo ni lazima. Awali tulikuwa tunapeleka bidhaa kuhakikiwa na Mamlaka ya Dawa na Chakula (TFDA, sasa TMDA), baadaye Serikali ikaamua bidhaa za aina yetu zipitie Shirika la Viwango Tanzania (Tanzania Bureau Standard, TBS)."

Swali: imewahi kukumbana na mkono wa serikali kuhusu lolote ambalo ulikiuka kwenye bidhaa zenu?"

Dk. Elizabeth: (kicheko). Ndiyo, wakati tunaanza hatukuwa na utaalam kama tuliyonao sasa ambapo tumebobea. Tuliwahi kufungiwa kwa miezi sita na kutakiwa kurekebisha mambo fulani. Tuliporekebisha ndiyo tukaruhusiwa mpaka leo hii."

Swali: "Wadada, baadhi yao wanapenda sana kujichubua kwa kutumia vipodozi vyenye uwezo huo. Je, vipodozi vyenu vinachubua?"

Dk. Elizabeth: "Hapana. Nasema hapana. Vipodozi vya Zoa Zoa kamwe havichubui bali vinang'arisha ngozi kwa rangi ya asili ya mtu. Ukikutana na mdada amejikoboa vya kutosha, huyo hajatumia Zoa Zoa."

Swali: "Wazo la kutengeneza vipodozi lilikujia kwa mtindo gani?"

Dk. Elizabeth: "Ilikuwa nife kwa sababu ya kutumia vipodozi vya kuchubua ngozi. Nilinunua vipodozi na kutumia, nukaanza kuharibika uso. Yaani ilikuwa hatari. Ilibidi niende Hospitali, daktari akaniambia ili nijinusuru mimi, mume wangu na mtoto itabidi niache. Ina maana sumu ya kipodozi ingeweza kusababisha madhara hadi kwa watu wa karibu.

"Ndipo nilipoanza kupata wazo la kutengeneza kipodozi kwa kutumia mimea asili ili niondoe ile hatari kwenye ngozi yangu. Sasa baada ya kutengeneza na kutumia na matokeo kuwa mazuri, nilipata wazo la kutengeneza kwa wingi na kuwauzia wengine. Ndivyo nilivyoanza."

Swali: " Unatumia mimea au matunda gani asilia kutengenezea vipodozi vya Zoa Zoa?"

Dk. Elizabeth: "Mazao ya nyuki, Avocado (maparachichi), maziwa, Nazi, michaichai, n.k. Ila tunatengeneza kwa utaalamu wa kiwango cha kimataifa ndiyo maana nilipewa Udaktari wa heshima."

Swali: Unakutana na ugumu gani kwenye biashara hii?"

Dk. Elizabeth: "Hakuna biashara isiyo na ugumu. Lakini kubwa kwetu ni baadhi ya wateja kuiga bidhaa zetu, hasa sabuni ya Zoa Zoa Manjano. Kitendo hicho kimetufanya kubadilika kwenye vifungashio. Boksi la sabuni ya Zoa Zoa Manjano lina mwinuko kwenye neno Zoa Zoa, wakati sabuni feki halina. Huo ni utofauti mkubwa."

"Ugumu mwingine ni baadhi ya watu wananunua vipodozi siyo Zoa Zoa, wakitumia wakatoka mabaka wanasema ni Zoa Zoa. Sisi Zoa Zoa hatuna bidhaa zenye nembo nyingine na wala hatuna vipodozi vya kuchubua ngozi. Kama mnavyoniona mimi, natumia losheni za Zoa Zoa lakini rangi ya ngozi yangu iko vilevile."

Swali: "Wewe ni daktari wa binadamu au wa heshima kama walivyo wengine waliyoupata kwa heshima?"

Dk. Elizabeth: "Udaktari wangu ni wa heshima kutokana na biashara zangu hizi nikatunukiwa Doctor of Public Administration & Business Management."

Swali: "Nini malengo yenu kwa mwaka 2022?"

Dk. Elizabeth: "Kuzidisha ubora zaidi katika bidhaa. Tuna malengo ya kutengeneza vifungashio vyetu wenyewe hapa nchini badala ya kuagizia nje. Na tumeanza, baadhi ya bidhaa vifungashio vimeandikwa Grace Natural Products, Neema juu ya Neema "

Mwisho.


IMG_2216 (1).JPG
 
Good
.
Ila iyo brand name ya "zoa zoa" innamchelewesha .....kwenye kiswahili Cha kibiashara Ina maana nyingi sana
 
Serikali ya Samia ni wakati muafaka sasa kuirudisha TFDA maana TBS imeshindwa kusimamia masuala mazima ya ukaguzi na udhibiti wa ubora wa chakula na vipodozi nchini.

Hivyo kuhatarisha afya za watanzania.

#MaendeleoHayanaChama
 
Back
Top Bottom