Mahojiano kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa lissu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahojiano kesi ya kupinga matokeo ya ubunge wa lissu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Isango, Mar 29, 2012.

 1. I

  Isango R I P

  #1
  Mar 29, 2012
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 295
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kesi inavyoendelea Cosmas Kasangani:

  Katibu wa CCM Wilaya ya Urambo Wakili wa watoa maombi, Bwana. Wasonga.Mimi ni wakili nitakuongoza kukuuliza maswali na wewe utamjibu jaji:

  Naitwa Cosmas kasangani, umri wangu miaka 54, naishi halmahauri ya wilaya ya urambo, tangu 2011., Nilihamia huko Novemba na kabla ya hapo nilikuwa naishi Singida mjini.Huko kazi yako ni ipi?Mimi ni katibu wa Chama cha Mapinduzi, Wilaya ya Urambo, kazi ambayo naifanya hadi sasa.Umesema ulikuwa unakaa Singida, ulihamia lini na ulikuwa unafanya kazi gani? Nilihamia 2009, na nilikuwa katibu wa CCM, Singida vijijini.

  Ukiwa kama katibu ulikuwa unafanya majukumu gani?

  Mimi nilikuwa msimamizi wa kazi zote za CCM, wilaya ya Singida.

  Tusaidie: Mwaka 2010 kulikuwa na kazi gani muhimu.

  Mheshimiwa jaji, Mwaka huo ulikuwa mwaka wa uchaguzi mkuu wa udiwani, ubunge na urais.

  Ulishiriki uchaguzi mkuu?

  Ndiyo:

  Ulishiriki kama nani?

  Nilishiriki kama katibu wa CCM wilaya. Ambapo mojawapo ilikuwa kuratibu shughuli za uchaguzi, kupokea na kusimamia maelekezo ya Uchaguzi, toka kwa msimamizi kwenda kwenye chama, na kwa wagombea.

  Katika Uchaguzi huo, eneo lako la kazi lilikuwa lipi.

  Eneo langu lilikuwa na wilaya ya singida, yenye majimbo matatu, Singida Mashariki, Singida magharibi na Singida kaskazini.

  Uchaguzi huo katika jimbo la mashariki ulihusisha ngazi ngapi?

  Ulihusisha Udiwani, ubunge na Urais.

  Kulikuwa na vituo vya kupigia kura?

  Ndiyo.

  Ili useme hiki ni kituo cha kupigia kura kuna nini?

  Kuna wasimamizi, wasimamizi wasaidi, kuna Askari, kunakuwa na vifaa vya kupigia kura, Mihuri, masanduku ya kupigia kura na mawakala.

  Hivi vituo vya Jimbo la Singida vilikuwa vingapi?

  Vilikuwa 124.

  Kulikuwa na mawakala wangapi kila kituo?

  Kulitakiwa kuwa na wakala mmojamoja kutoka kila chama kinachoshiriki uchaguzi.

  Katika Jimbo hili la Singida mashariki, kulikuwa na vyama vingapi vilivyoshiriki uchaguzi?

  Kulikuwa na vyama vitatu vilivyoshiriki uchaguzi kwa nafasi ya Ubunge.

  Vitaje.

  CHADEMA, CCM NA CUF.Mheshimiwa jaji, ninaomba kukaa, nashindwa kusimama muda mrefu

  JAJI: Kaa tu

  Chadema walikuwa na mgombea gani?

  TUNDU LISSU. CCM walikuwa na Jonathan Njau, na CUF alikuwa Abdala Mukhandi.TUNDU LISSU 13,787, ndiye aliyetangazwa mshindi.NJau 12,602, na Abdala wa CUF 139.CCM iliweka mawakala 124, mmoja kila kituo.

  Ili usema kuwa CCM imeweka wakala, mlitumia utaratibu gani?

  Chama kwa ushirikiano na mgombea wanaandaa orodha ya mawakala, inayopelekwa kwa msimamizi wa uchaguzi.

  Je ninyi mlifanya vile?

  Ndio mheshimiwa jaji.

  Una orodha?

  NDIYO.

  Nani aliandaa hiyo orodha?

  Niliandaa mimi Cosmas Kasangani, katibu wa wilaya.

  Ungependa sehemu ya karatasi uliyo nayo iwe sehemu ya ushahidi?

  NDIYO: (Jaji anapewa orodha, anakagua)

  Wajibu maombi wameulizwa na wamesema hawana pingamizi na orodha, imepokelewa

  Hiyo orodha yako na barua yako iliandaliwa lini?

  Iliandaliwa 18/10/2010.

  Taja Kumb. NO.

  CCM/WSV/UCH/2010/1/78.

  Barua hiyo iliandikwa kwa msimamizi wa Uchaguzi na niliambatanisha orodha ya majina ya mawakala. Hapa nimeweka majina ya mawakala wa singida mashariki tu.

  Ulisema vyma vingine navyo vilishiriki, je kulikuwa na mawakala?

  NDIYO.

  Je katika kumbukumbu zako, vyama vilivyokuwa na mawakala vilikuwa vyama gani?

  CHADEMA, CUF, APPT MAENDELEO, TLP na CCM.

  Katika uchaguzi, kuna kuwa na mambo mengi. Kuna mazuri na dosari, hatutaki kupoteza muda wa mahakama, tusaidie kama uliona dosari zipi ulizoona wakati wa uchaguzi.

  Mh. Jaji, Dosari ni CHADEMA na Mgombea wake, aliaandaa barua na kuwatambulisha mawakala wa TLP, NCCR mageuzi, APPT maendeleo, na CUF

  Kwanini wewe unasema kwamba ni mgombea wa kwanza ndiyo aliandaa hizo barua?

  Kwa sababu ya barua zenyewe zinavyofanana.

  Je unazo?

  NDIYO: Hizi hapa ninazo.

  Una barua za vyama gani?

  CHADEMA, NCCR mageuzi, Appt Maendeleo, TLP, na CUF.Hizi zinafana kiuandishi .

  TUNDU LISSU Anasimama kuweka pingamizi.Anasema Hawezi kuzungumzia content za barua kabla hazijaingizwa kama kumbukumbu katika hati za mahakama
   
 2. dhahabuinang'aa

  dhahabuinang'aa Senior Member

  #2
  Mar 29, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nakuja kamanda wangu ISANGO leo nimechelewa kutokana na majukumu ya kikazi.
  naja tuko pamoja.
   
 3. MESTOD

  MESTOD JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2012
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 4,641
  Likes Received: 142
  Trophy Points: 160
  nimeshindwa kuisioma.
   
 4. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  kalale
   
 5. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,869
  Likes Received: 6,608
  Trophy Points: 280
  Endelea Kamanda..
   
 6. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  OUR man our MP Tundu Lissu
   
 7. gambachovu

  gambachovu JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,865
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Inachosha.. Haikupangiliwa..
   
 8. dhahabuinang'aa

  dhahabuinang'aa Senior Member

  #8
  Mar 29, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 134
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wakuu huyu shahidi ataendelea kuhojiwa na mh TUNDU LISU kesho saa tatu asubuhi.
   
 9. Edson Zephania

  Edson Zephania Verified User

  #9
  Mar 29, 2012
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 507
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mkuu asante kwa taarifa lakini jatahidi kuipangilia vizuri
   
 10. monongo

  monongo JF-Expert Member

  #10
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 25, 2011
  Messages: 370
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  huyo shahidi wa uongo abanwe tu mpaka aeleweke.
   
 11. Somji Juma

  Somji Juma Verified User

  #11
  Mar 29, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,497
  Likes Received: 2,034
  Trophy Points: 280
  ahh.!unakua kama mwanafunz wa darasa la nne C bwana..
  upangiliaj gani huo.?unatupa tabu kusoma au we huoni.?
   
 12. R

  Real Masai Senior Member

  #12
  Mar 30, 2012
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mpangilioo c mzuri ila ujumbe umefika
   
Loading...