Mahojiano kati ya Andrew Chenge na Mwandishi wa TheGuardiantv leo

Mwandishi: Nimesikia tetesi umehamia ACT Wazalendo

Chenge: Kama ni tetesi mimi nathibitishaje mimi siyo mtu wa kuthibitisha , wewe nenda huko huko ulipopata source zako

Mwandishi: Vipi utamuunga mkono Mgombea alieletwa na Chama cha Mapinduzi

Chenge: Ebu acha Upumbavu unajua mie sipendi mambo ya kipumbavu nakwambia kabisa mimi huwa sipendi upumbavu wenu huko ,wewe ulinipa uanachama wa CCM wewe? Acheni mambo ya mchezo mchezo

Mwandishi: sasa tutegeme nini ukiwa unaenda kustaafu Siasa?

Chenge:
Nasema hivi wewe siyo mtu wa kunihoji wewe fanya kazi yako na mimi nitafanya mambo yangu huku

Yapi maoni juu ya mahojiano haya
 
MWANDISHI: Nimesikia tetesi kwamba umehamia ACT Wazalendo. Unaweza kuthibitisha ni kweli au si kweli?

CHENGE: Kama ni tetesi mimi nathibitishaje? Mimi siyo mtu wa kuthibitisha tetesi, wewe nenda hukohuko ulipopata source zako.

MWANDISHI: Vipi utamuunga mkono Mgombea aliyeletwa na Chama cha Mapinduzi kwenye jimbo lako?...
Wanasheria ni wavumilivu sana na huchunga sana ndimi zao. Chenge naona umri imekuwa mkubwa, akili umepungua.
 
Chenge amecheleweshwa sana. Alitakiwa awe ndani kwa makosa ya uhujumu uchumi yasiyo na dhamana. Ashukuru chama tawala ni CCM. Na kama kumuunga mkono mgombea aliyeteuliwa na CCM badala yake ni mambo ya upumbavu, akawaambie hao viongozi wake wa CCM kuanzia mwenyekiti wake, sio waandishi wa habari.
Kinachombeba huyu ni ukabila tuuu ??? Angekua sio msukuma angefia jela
 
Haitakuja tokea kufunguliwa mashtaka tena kama wanataka serikali imlipe tena wajaribu kumshitaki
Mkuu, unajua ni kwa nini kaunga mkono kukatwa huku kuahidi kutoa ushirikiano mchana kweupe?

Zipo nitakwambia!

Kwanza ilikuwa ni 'kuziua' tetesi za kuhamia Act.

Pili ilikuwa ni kujikosha na kujitakasa ili asiendelee kuguswa, apate kupumzika kwa amani!

Ujue kwa utawala huu wana mbinu wanazotumia namna wanavyoanza kumdhoofisha 'mbaya wao' kidomo domo ama kilimi limi, wakishaona amefikia 'stage' wanayoitaka wao ndiyo wanammaliza, mbinu hizo Chenge anazijua.

Embu fikiria Rugemarila na Sigh, walikuwa ni wa kugusa enzi zao, lakini leo je?

Joka la kengeza wakitaka kumshughulikia ni mwepesi kama bua, hana kinga yoyote ama mbinu zozote za kisheria ama za ukwasi anazoweza kuzitumia kumuokoa na gereza zaidi ya kulamba miguu utawala na ndiyo mbinu pekee itayomsaidia na kuwa kinga yake.
 
Ila Chenge anafaa kuwa spika kuliko Ndugai.

Agombee kupitia Chama kingine ili baadae agombee Uspika. Au ahame tu kisha agombee uspika. Ndani ya CCM haweizi kupitishwa mana tulia yupo na Ndugai na wote wanaendesha bunge kama Kamati ya usajili ya club ya mpira inayomilikiwa na mtu binafsi.
 
Lakini kwa nini wamemkata wakati kashinda kura za maoni huu ni uonevu wa wazi kabisa
Naye atakuwa mpumbavu sawa na hao anaowaita wapumbavu kama alishindwa kusoma alama za nyakati.

Huyu hata kwenye kampeni za 2015 Magufuli aligoma kumnadi jukwaani Bariadi, alitegemea nini wakati leo Magufuli ndiye mwenyekiti wa chama?
 
Unataka kusema ni kilaza kuzidi hawa wa clouds na tiiiibiiisiiii wani!??
Hawa sio vilaza, ni kujipendekeza kunawasumbua. Huyo mdada ni balaa mzee, alishindwa kusoma zile asilimia ambazo H. Mwinyi alizipata kwenye NEC, ukiacha hilo alikuwa anaongea vitu vya ajabu sana. Nafikiri atakuwa ni cheap labour yule. Kuna mwingine huko huko Mwanahalisi alimuhoji kubenea sababu za kuhamia ACT, hajiamini kabisa yule kijana.
 
Nani atamuweka Chenge ndani? JPM? sidhani. Chenge ana taarifa za ufisadi wa kila kiongozi wa CCM alioufanya kuanzia 1995 hadi 2010. Sasa jiulize kama hajui ufisadi wa JPM kama kivuko cha Bagamoyo au uuzaji wa nyumba za Serikali kwa vimada.
Ingekuwa hivi wasingemkata
 
Back
Top Bottom