Mahojiano kati ya Andrew Chenge na Mwandishi wa TheGuardiantv leo

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
8,572
2,000
MWANDISHI: Nimesikia tetesi kwamba umehamia ACT Wazalendo. Unaweza kuthibitisha ni kweli au si kweli?

CHENGE: Kama ni tetesi mimi nathibitishaje? Mimi siyo mtu wa kuthibitisha tetesi, wewe nenda hukohuko ulipopata source zako.

MWANDISHI: Vipi utamuunga mkono Mgombea aliyeletwa na Chama cha Mapinduzi kwenye jimbo lako?

CHENGE: Hebu acha Upumbavu wako. Unajua mi sipendi mambo ya kipumbavu? Nakwambia kabisa mimi huwa sipendi upumbavu wenu. Wewe ulinipa uanachama wa CCM wewe? Acheni mambo ya mchezo mchezo.

MWANDISHI: sasa tutegemee nini ukiwa unaenda kustaafu Siasa?

CHENGE: Nasema hivi, wewe siyo mtu wa kunihoji wewe. Fanya kazi yako na mimi nifanye mambo yangu.!

Mzee baba, Nyoka mwenye makengeza kamwaga povuu kama looote!.

Usitufokee!

118248259_3274319465993056_8025904583877126273_n.jpg
 

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
8,938
2,000
Chenge amecheleweshwa sana. Alitakiwa awe ndani kwa makosa ya uhujumu uchumi yasiyo na dhamana. Ashukuru chama tawala ni CCM. Na kama kumuunga mkono mgombea aliyeteuliwa na CCM badala yake ni mambo ya upumbavu, akawaambie hao viongozi wake wa CCM kuanzia mwenyekiti wake, sio waandishi wa habari.
 

mukaruka mzee

JF-Expert Member
Jan 22, 2020
742
500
Hayo majibu ya Mh. Andrew Chenge ndiyo majibu sahihi kwa waandishi wasiofahamu namna ya kuendesha MAHOJIANO. Inabidi warudi shule au darasani kabla ya kuhojiana na watu wa aina ya Mh. Chenge, watu wanaojua the right and appropriate questions for them and how to react.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom