Mahojiano Kabambe: Tundu Lissu Vs Jenerali Ulimwengu

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,793
71,207
Fungua link hiyo usikilize mwenyewe na utagundua kuwa uwezo wa Lissu katika kujieleza bila woga haujatetereka wala kutikiswa na yale yaliyomtokea, na hakika atakuwa mwiba mkali sana kwenye kampeni dhidi ya mgombea wa CCM bwana Magufuli kama tuu Chadema watampitisha kuwa mgombea wao.

======

Lissu: Narejea Tanzania kabla ya Julai 28

TUNDU Antipas Lissu, Makamu mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) amesema, atarejea Tanzania mwishoni mwa mwezi huu.

Amesema, atafanya hivyo ili aweze kuhudhuria mkutano wa Baraza Kuu na mkutano mkuu wa chama hicho tarehe 28 na 29 Julai 2020.

Mikutano hiyo, pamoja na mambo mengine, itampitisha mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020

Mchakato wa uchakuaji na urejeshaji fomu za kuwania Urais wa Tanzania unaanza leo Jumamosi tarehe 4 hadi 19,2020.
Wagombea au mawakala wao watakuwa na fursa ya kuchukua fomu kisha kutafuta wadhamini 100 katika kila kanda kumi za chama hicho

Lissu ni miongoni mwa wanachama ambao wamekwisha tia nia hadharani ya kuwania nafasi hiyo ya juu kabisa ya uongozi wa Taifa hilo lililopo Afrika Mashariki

Akihojiwa na mwandishi nguli nchini Tanzania, Jenerali Ulimwengu katika kipindi chake kinachorushwa na JeneraliOnline, Lissu amesema, baada ya safari ndefu ya kutibu majeraha na kupona, sasa yuko tayari kurejea nchini humo.

Amesema anarejea ili kuomba ridhaa ya wana Chadema na Watanzania kumchagua kuwa Rais wa Tanzania ili kuwatumikia kwa kuunganisha nguvu kwa pamoja kwani ana imani mtu mmoja pekee hawezi kuongoza nchini.

Tangu tarehe 7 Septemba 2017, Lissu aliposhambuliwa na watu wasiofahamika akiwa nyumbani kwake Area D jijini Dodoma, mwanasiasa huyo amekuwa nje ya Tanzania kwa matibabu

Siku hiyohiyo usiku, alihamishiwa Hospitali ya Nairobi nchini Kenya kwa matibabu hadi tarehe 6 Januari 2018 alipopelekwa nchini Ubelgiji kwa matibabu zaidi

Hata hivyo, Lissu mwenyewe amekwisha kusema amepona na hatumii dawa zozote na anachosubiri ni kureja nyumbani Tanzania kuendelea na shughuli zake mbalimbali hasa za kisiasa

 
Asante sana kwa kutuletea haya mahojiano.

Baada ya kumsikiza,nimegundua harudi huku akibahatisha kuhusu usalama wake bali kajipanga.Anawapa Polisi wa nchi hii kipaumbele cha kwanza katika ulinzi wake kama raia na pia kama mtia nia wa uraisi anaepaswa kulindwa kwa mujibu wa sheria na pia akiwa mgombea endapo atapitishwa na chama chake. Vile vile ni wazi hategemei tu ulinzi wa Polisi,bali ana Plan "B" juu ya ulinzi na usalama wake.

Kuhusu awamu ya tano na rasilimali madini,teyari keshaonyesha ni jinsi gani awamu hii haina tofauti na zilizopita katika swala zima la sheria zinazoweza kulinda rasilimali hii na kaeleze jinsi hii serikali ilivyokwenda kinyume na sheria ya mwaka 2017 kuhusu rasilimali za nchi,sheria waliyoileta wao wenyewe.

Akipitishwa,ni wazi kwenye kampeni tutasikia mengi.
 
Hoja zote za Lissu zina mashiko isipokuwa tu pale anapojaribu kuipambanisha serikali ya Magufuli na jumuia ya kimataifa. Hao wenyewe wanaoitwa jumuia ya kimataifa ni watu kama mi na wewe, wanafahamu kuwa mkuu wa nchi ni mtu muhimu sana na wakiwa na maslahi yao kwenye nchi wanaanzia kwa huyo huyo mkuu wa nchi ambaye nyie mnamwita majanga au dikteta. Chezeni siasa zenu kwa akili.
 
.Vile vile ni wazi hategemei tu ulinzi wa Polisi,bali ana Plan "B" juu ya ulinzi na usalama wake.
Nashukuru umekumbuka kuiweka hii. Nilianza kuwashwa vidole ili nikurukie shingoni. Hii haiwezi kuwa 'PLAN B', hii ni 'PLAN A', hizo nyingine ndio hizo B.

Yeye, na hasa CHADEMA hawawezi kushindwa kumpa ulinzi mkali sana mgombea wao. Hao polisi hata kama itawalazimu kuweka ulinzi, ulinzi wa hakika kabisa ni ule atakaoweka yeye na/au chama chake.

Kama kuna kichaa yeyote aliyeshindwa maisha yake mwenyewe, ni lazima ajue hawezi kutoka salama akijaribu tena kumdhuru Tundu Lissu.

Hili ndilo linalotakiwa kutangazwa wazi kabisa na kila mtu yeyote ajue kuwa kama anataka vita, basi vita ataipata.

Hawa watu wanafurahi sana kusikia CHADEMA wakilialia. Inabidi sasa waache kulialia, iwe ni 'hard ball' kwa kila atakayetaka mchezo huo.
 
Hoja zote za Lissu zina mashiko isipokuwa tu pale anapojaribu kuipambanisha serikali ya Magufuli na jumuia ya kimataifa. Hao wenyewe wanaoitwa jumuia ya kimataifa ni watu kama mi na wewe, wanafahamu kuwa mkuu wa nchi ni mtu muhimu sana na wakiwa na maslahi yao kwenye nchi wanaanzia kwa huyo huyo mkuu wa nchi ambaye nyie mnamwita majanga au dikteta. Chezeni siasa zenu kwa akili.
"---anapojaribu kuipambanisha serikali ya Magufuli na jumuia ya kimataifa."

Sijui hapa una maana gani. Anaipambanisha vipi serikali ya Magufuli na hiyo jumuia ya kimataifa?

Kueleza maovu inayowafanyia wananchi wake ni kupambanisha serikali na jumuia za kimataifa?

Kwa hiyo watu wakae kimya tu wasieleze, jumuia ya kimataifa isiyajue yanayowasibu kwa kuogopa kwamba hao watu hawawezi kusaidia chochote, hata kukemea tu mabaya, na badala yake watakwenda kumwona kiongozi anayewanyanyasa watu wake ili wanufaike wao?

Hii ni akili toka wapi? Mnataka watu waumie tu humu humu ndani wakiwa kimya ili muendelee kuwaminya zaidi?

Mkeo unamtandika mangumi, unamwonya anyamaze majirani wasisikie kitu, ndio furaha yako?

Bure kabisa.
 
Usalama wake ni jambo la msingi sana, na hapa serikali inawajibu wa kutoa ulinzi kwa Lissu hasa atakapokuwa mikononi mwa vyombo vya usalama, kwasababu ninaamini kuna wakati Lissu anaweza kujikuta chini ya mamlaka ya vyombo vya usalama hasa kutokana na kesi zinazomkabili.

Hili ni jukumu la serikali na serikali lazima ijue huo ni wajibu wake kama wananchi wote tunavyofahamu, hapa hakuna cha plan "A" wala "B".

Simply plan zote zipo kwa serikali, na lolote baya litakalompata Lissu akiwa chini ya vyombo vya usalama serikali itatakiwa kutoa maelezo ya kutosha, kwani Lissu hawezi kwenda na ulinzi wake binafsi mahakamani, au rumande, kama akitakiwa kufanya hivyo.
 
Asante sana kwa kutuletea haya mahojiano.

Baada ya kumsikiza,nimegundua harudi huku akibahatisha kuhusu usalama wake bali kajipanga.Anawapa Polisi wa nchi hii kipaumbele cha kwanza katika ulinzi wake kama raia na pia kama mtia nia wa uraisi anaepaswa kulindwa kwa mujibu wa sheria na pia akiwa mgombea endapo atapitishwa na chama chake.Vile vile ni wazi hategemei tu ulinzi wa Polisi,bali ana Plan "B" juu ya ulinzi na usalama wake.

Kuhusu awamu ya tano na rasilimali madini,teyari keshaonyesha ni jinsi gani awamu hii haina tofauti na zilizopita katika swala zima la sheria zinazoweza kulinda rasilimali hii na kaeleze jinsi hii serikali ilivyokwenda kinyume na sheria ya mwaka 2017 kuhusu rasilimali za nchi,sheria waliyoileta wao wenyewe.

Akipitishwa,ni wazi kwenye kampeni tutasikia mengi.
Tundu Lissu tu ndie anayeifaa Tanzania kwa nyakati hizi za sasa.
 
Mwambie Mwenyekiti ampe nafasi Lissu..
Maana kashambana kwa yeye m/kiti kutaka kujiteua...
Mambo yenu ni magumu mpaka mnachanganyikiwa. Jana mnatumia jeshi la magereza kuwapambia bendera mjini Leo mtatumia polisi kupanga viti ukumbini na kesho JWTZ kuwaimbia kwaya wajumbe wa mkutano mkuu. Maana ya "kugombea kuongoza vyombo vya dola" itakuwa imetimia.
Hivyo pambana na hali yenu, haya ya Chadema huyawezi
 
Magufuli amefanya mengi mazuri ila namna yake ya utawala ndio imeudhi na kuumiza wengi anasahau yeye mwenyewe ni mhanga wa vitisho vya kuuwawa mpaka akaomba ulinzi wa Ben Mkapa ? Nisahihi kabisa kusema Magufuli ni bahati mbaya Sana kwa taifa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom