Mahojiano: Dina Marios na Mama Hasheem Thabeet

Shadow

JF-Expert Member
May 19, 2008
2,897
671
Mahojiano: Dina Marios na Mama Hasheem Thabeet 08/18/2010
http://www.wavuti.com/4/post/2010/08/mahojiano-dina-marios-na-mama-hasheem-thabeet.html#comments


Mahojiano haya yamenukuliwa yalivyo toka katika blogu ya Dina Marios, mtangazaji wa kipindi maarufu cha Leo Tena katika redio ya Clouds FM. Dina anasema kwa mara ya kwanza amepata fursa ya kuonana na Bi Rukia Thabeet Manka, ambaye ni mama mzazi wa Hasheem Thabeet, mchezaji wa kwanza kutoka Tanzania aliyefuzu kucheza katika ligi ya mpira wa kikapu almaaruf NBA, nchini Marekani. Endelea...

9119717.jpg
Bi Rukia Thabeet Manka katika studio za CloudsFM Dar​
Bi Rukia Thabeet Manka leo ndio ilikuwa mara yangu ya kwanza kuonana nae ana kwa ana kiukweli ni mama mmoja mcheshi sana na mzungumzaji mzuri tu. Fatilia mazungumzo yetu kama ilivyokuwa leo katika leo tena.

Dina: Karibu mama Hashim kwanza tueleze kwa ufupi historia ya Hashim.

Mama Hashim:
Hashim alizaliwa tarehe 26 mwezi wa pili 1987 mkoani Dodoma ambapo ndipo tulikuwa tukiishi kabla ya kuhamia hapa Dar. Nikiwa mjamzito nilikuwa na tumbo kubwa kiasi cha watu kuhisi nimebeba mapacha hata kliniki waliniambia nimebeba mapacha.Wakati wa kujifungua ulipofika nilienda katika hospitali ya wilaya kujifungua wenyewe wakijua ni mapacha wakaniambia niende hospitali ya mkoa.Kufika kule nikaambiwa nirudi tu hospitali ya wilaya nitajifungua salama kwa hiyo nikarudi. Nesi aliyenizalisha namkumbuka mpaka leo Mama Makala baada ya Hashim kuzaliwa alikimbilia kwa dokta kumwambia nimezaa mtoto wa ajabu maana alizaliwa akiwa na mikono mirefu na miguu mirefu yule nesi aliniogopesha mpaka nikahoji kulikoni nilipokuja kumuona mtoto mimi nilimuona wa kawaida tu.

Dina: Baada ya kuzaliwa makuzi yake yalikuwaje?alikuwa akirefuka harakaharaka?

Mama Hashim: Kweli alikuwa akirefuka haraka sana mpaka shule ilibidi nimuanzishe darasa la kwanza akiwa na miaka 5 na bado darasani alikuwa mkubwa kuliko wenzake kiurefu.

Dina: Tumekua tukisikia Hashim akikuzungumzia wewe sana, kwani baba yuko wapi?

Mama Hashim: Mume wangu alifariki mwaka 2004 toka hapo nimekuwa nikiwalea mwenyewe ndio maana Hasheem amekuwa akinitajataja sana mimi. Hasheem ni wa pili kuzaliwa ana dada yake wa kwanza anaitwa Sham halafu yeye ndio anafuata na mwisho ni mdogo wake wa kiume anaitwa Akbar.

Dina: Hashim anavaa kiatu namba ngapi kwa sasa?mara ya mwisho kumnunulia viatu ilikuwa lini?

Mama Hashim:
Hashimu kwa sasa anavaa kiatu namba 38 ya Marekani na namba 54 ya Uingereza.Kiukweli sikumbuki mara ya mwisho kumnunulia kiatu ilikuwa lini ila nakumbuka nilikuwa nikipata sana tabu maana sikuwa nikipata size ya kiatu chake madukani mpaka mtumbani na mtumbani kwenyewe walianza kunifanyia kusudi ilifika wakati mtu anajua sina jinsi lazima kiatu ntanunua anakuuzia Tsh 70,000 mpaka Tsh 100,000.

Dina: Uhusiano wa Hashim na baba yake kabla hajafariki ulikuwaje? ni kitu gani ambacho Hashim amerithi kutoka kwa baba yake ambavyo ukimuona unamkumbuka mumeo?

Mama Hashim:
Uhusiano wa Hashim na baba yake ulikuwa mzuri kiukweli alikuwa anawapenda watoto wake wote. Hashim amechukua hekima za baba yake,ukarimu na upendo baba yao alikuwa mtu wa watu, mpole sana.

Dina: Unafikiri kikwazo kikubwa cha maendeleo ya wanawake Tanzania ni nini?

Mama Hashim: Woga, kutokujiamini nakusema siwezi.

Dina: Aina gani ya mwanamke ungependa mwanao aoe hapo baadae, sifa sipi za mkweo ungependa awe nazo?

Mama Hashim:
siwezi kumchagulia yoyote atakaempenda yeye mie ntampokea.

2670603.jpg
Dina Marios na Bi Rukia Thabeet Manka studioni CloudsFM Dar Es Salaam​
Dina: Ni changamoto zipi ambazo wewe mama na mwanao mmepitia?

Mama Hashim: Kiukweli mwanangu alikuwa anachekwa sana na watu kisa urefu wake,wengine walikuwa wakidiriki kumuita shetani,jini na majina kibao. Kila alipokuwa akipita watu walikuwa wakimshangaa ilikuwa inaniuma sana kama mama ila nilikuwa namshukuru mungu kwa kila kitu….leo hii jini langu ndio huyo ananisaidia mama yake. Yeye mwenyewe ilikuwa ikimsumbua sana kweli mungu ana mipango yake kwa kila mtu.

Dina: Leo hii naamini maisha yamebadilika sio kama ilivyokuwa miaka mitano iliyopita, pia unakabiliwa na changamoto zipi?

Mama Hashim:
Kiukweli watu wana mambo leo hii wapo wanaosema naringa kisa mafanikio ya mwanangu jambo ambalo sio kweli. Kama mzazi nafurahia mafanikio ya mwanangu lakini bado mimi ni yuleyule mama Hashim wa siku zote sibagui wala kuchagua wakubwa kwa wadogo wote wangu.Kabla Hashim hajafikia mafanikio walinibeza mimi mama jini leo kafanikiwa naringa wanadamu huwezi kuwaridhisha ila mimi namshukuru mwenyezi mungu kwa kila kitu.

Dina: Unaonekana ni mama ambae unajipenda, unapenda kuvaa unaweza kuelezea style yako?
Mama Hashim: Dina sina style maalum navaa chochote kinachonipendeza iwe gauni refu au fupi, sketi au suruali ili mradi nipendeze.

Dina: Kama mzazi ambae leo hii unafurahia matunda ya kipaji cha mwanao unawapa ushauri gani wazazi wengine?

Mama Hashim: Kiukweli wakati wanakuja kumchukua Hashim kwenda kusoma na kucheza mpira wa kikapu Marekani wapo walionicheka kwamba kwa nini sijachukua hata pesa au niwaambie waninunulie nyumba au wanipe gari. Mimi niliona kama nikumuuza mtoto hata yeye asingefurahi mimi nilimwambia nenda halafu vyovyote itakavyokuwa mtaniambia. Kweli leo nayaona mafanikio hivyo wazazi kama mwanao ana kipaji msaidie uwe nyuma yake. Mtoto wangu wa mwisho Akbar yeye anacheza sana soka ila dada yao hana kipaji chochote.

Dina: Unaendesha gari gani kwa sasa?
Mama Hashim: Naendesha Range rover alininunulia Hashim.

Dina: Huwa unaenda Marekani kumsalimia mwanao?

Mama Hashim:
Ndio huwa naenda, nimeshaenda kama mara tatu.

Dina: Tungeongea mengi ila kwa leo tuishie hapa, asante kwa kuja mamy.
Mama Hashim: Asante Dina tukijaaliwa siku nyingine.​



credit source: Mahojiano: Dina Marios na Mama Hasheem Thabeet - wavuti
 
Safi sana ila aendelee kuwa mentor wake ili awe na maadili mema na adumu katika kipaji chake hiki. Bado kijana ni mdogo kiumri na ule ambao wengi wanapenda sana mambo ya dunia. Akiweza kuuvuka umri huu salama ni heri sana. Pongezi Manka.
 
Yeah! sometime it is Great to have a humble biggining and start calling the shots.....go go Thabeet:playball:
 
Laiti mwanadamu angelijua kuwa maneno yake ndio yanamfanya mwengine ajitahidi wasingelikuwa wanapita kusemasema watu. Wewe mtu amezaa mtoto mrefu unaanza kumuita mtoto huyo majina ya ajabu ajabu utafikiri wewe mwanao malaika. Sasa mungu amemfangulia mnaanza kulalama. Kweli nimesikitika sana hongera mama endelea kuwa hivyo hivyo na ikiwezekana mwambie hashimu awe muangalifu tu ili usirudi ulikotokea maana ukifilisika wataanza tena kusema binaadamu huwawezi kwa midomo.
 
Back
Top Bottom