Mahojiano Azam Two TV: Funguka na Naibu Spika Dr. Tulia Ackson

mcubic

JF-Expert Member
Mar 3, 2011
10,307
6,514
Tido: Jina lako limekua haraka sana kuliko wengine je ulipata msaada wowote?

Tulia: Hapana, nilichukua hatua nwenyewe mambo mengine yakanikuta

Tido: Ulikuwa naibu mwanasheria mkuu, je kwa wakati huo ulikuwa CCM?

Tulia: Katiba imekataza baadhi ya makundi, sheria na taratibu ziliniruhusu kuwa kwenye pande zote mbili ( mwanachama na mwanasheria ). Pia mimi ni mwalimu chuo kikuu na walimu wengi ni wanachama wa vyama mbali mbali.

Tulia: " Mimi sipendelei serikali ila nafuata taratibu na kanuni"

Tido: "Unajisikiaje unapoambiwa kuwa upo hapo kuitetea CCM au Serikali."

Tulia: "Sijisikii vibaya, kuna watu hawafurahii kuwa na nafasi hii niliyonayo, hata mimi pengine nisingefurahi kwa mwingine kuwa na nafasi hii"

Tulia: "Sijisikii vibaya, kuna watu hawafurahii kuwa na nafasi hii niliyonayo, hata mimi pengine nisingefurahi kwa mwingine kuwa na nafasi hii"

Tiddo: " Je unawachukia wapinzani?"

Tulia: " Siwachukii na wala sina sababu ya kuwachukia, sijafanya kosa kwa mujibu wa kanuni na taratibu, pia sielewi kama wao wananichukia"

Tiddo: " Ishara zinaonesha wewe unawachukia wapinzani, kwa kipindi kifupi ulichokaa umewaadhibu wapinzania wengi"

Tulia: "Mimi sitoi maamuzi ya kuadhibu wapinzani, kuna kamati ya maadili wakiwemo wapinzani ndio wanaotoa maamuzi"

Tiddo: "Mbona maamuzi yako ni ya upande mmoja tu?"

Tiddo: " Lakini wewe ndio umekalia kiti, wewe ndio mwenye nguvu.....pia je hakuna wabunge wa ccm waliokiuka kanuni?"

" Wabunge wa upinzani wengi hawakuwa bungeni, hivyo si Tulia anayetoa adhabu"

Tiddo: " Mvutano wako na Ukawa imesababisha wao kususia bunge, je unaonaje hali hiyo"

Tulia: " Siwezi kulisemea hilo, ila wao walikuwa na hoja ya kumuondoa N spika bungeni, labda walikuwa wanasubiri hoja yao ipite"

Tiddo: " Mbona ulikuwa huachii kiti, au ulikuwa unafanya makusudi kuwakomoa wapinzani"

Tiddo: " Je unawachukia wapinzani?"

Tulia: " Siwachukii na wala sina sababu ya kuwachukia, sijafanya kosa kwa mujibu wa kanuni na taratibu, pia sielewi kama wao wananichukia"

Tiddo: " Ishara zinaonesha wewe unawachukia wapinzani, kwa kipindi kifupi ulichokaa umewaadhibu wapinzania wengi"

Tulia: "Mimi sitoi maamuzi ya kuadhibu wapinzani, kuna kamati ya maadili wakiwemo wapinzani ndio wanaotoa maamuzi"

Tulia: " Mimi niliongoza vikao kwa taratibu na kanuni, Spika hakuwepo, hivyo ilinilazimu kuongoza bunge, wenyeviti wanaongoza vikao mpaka pale N Spika, na Spika wasipokuwepo"

Tiddo: " Utamaduni unaonesha hata wenyeviti kuongoza vikao hata spika na N spika wakiwepo, kwa nini hukufanya hivyo?

Tulia: "Nafanya kazi kwa kufuata taratibu, na sio utamaduni"

Tiddo: "Umepelekwa kwenye kamati ya maadili kwa kukiuka kanuni na taratibu za bunge, unazungumziaje suala hilo?"

Tulia: "Nafarijika sana kwa wabunge hao kutumia haki yao kisheria kupeleka mashtaka dhidi yangu"

" Hoja nzito hazitegemei upande wa chama cha siasa, wabunge waliobaki bungeni walifanya mabadiliko makubwa"- Tulia

" Huoni kwamba suala la Lugumi lilikosa msisimko baada ya wabunge wa upinzani kuondoka bungeni?"-Tiddo

" Suala la Lugumi limefanyiwa kazi na kamati ya bunge, kuashiria serikali ihakikishe mapungufu yaliyojitokeza yanapatiwa ufumbuzi"- Tulia

"Watu wengi wanaona hoja inapata msisimko mpaka baadhi ya watu watajwe kwa majina, ikiwa kinyume na hapo hoja inakosa msisimko"-Tulia

"Kuna kundi liliibua suala hili, na wakatoka bungeni, huoni kuwa suala hili halikupewa uzito uliostahili?"-Tiddo

" Suala la Lugumi halikujadiliwa bungeni bali na kamati, hivyo hakuna mbunge atakayesema yy ndio ameliibua"-Tulia

" Hao wabunge waliosusa mie bado ni kiongozi wao, mie ndiye nasaini maombi yao mpaka leo, mpaka hoja ya mashtaka dhidi yangu itakapofanyiwa uamuzi"-Tulia

" Mie sivutani na mtu yeyote, hivyo hakuna hoja itayohitaji maridhiano, hawajanikosea jambo lolote"-Tulia

"Kwa hiyo mwezi wa tisa bado utaendelea kuvutana na wapinzani?...maana bado utaendelea kukalia kiti"- Tiddo

" Sina uhakika, pengine spika atakuwa amerudi"- Tulia

" Je unafurahia kazi yako ya unaibu spika?"- Tiddo

" Kila kazi ina changamoto zake, nafurahia kazi yangu ya kutafsiri sheria, maana nimesomea sheria"- Tulia

*****************************

Kipindi kimeisha.....Ahsanteni
 
Naibu Spika wetu Mh.Tulia yuko hewani muda huu kupitia Azam two akiwa chini ya uenyeji wa mzee Tido kwenye kipindi cha Funguka,kama una wasaa si vibaya kutazama.
 
Huyu mwanamke anakana yeye hajawahi kumwadhibu mtu...

Kudanganya hadharani kazi sana, kametoa macho kanakana kila kitu...
 
Back
Top Bottom