Mahitaji ya maji yaongezeka, uchumi wa viwanda hatarini kutofikiwa kama hatua hazijachukuliwa

FikraPevu

JF-Expert Member
Jan 2, 2010
303
236
Sera ya Maji ya mwaka 2002 inabainisha kuwa “Maji ni muhimu kwa viumbe vyote duniani, bila maji hakuna uhai. Aidha maji ni muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Kiwango cha maendeleo ya jamii yoyote kinategemea kuwepo kwa maji ya kutosha na yenye ubora unaotakiwa. Katika hali yake ya asili, maji ni sehemu ya mazingira ambapo wingi na ubora wake ndio unaosaidia katika kuamua jinsi maji yatakavyotumika”.

Lakini hali imekuwa tofauti na matarajio ya sera hiyo, ambapo mahitaji ya maji yameongezeka nchini kutokana na ongezeko kubwa la watu na shughuli za kiuchumi na kijamii ambazo zinatumia maji kwa wingi.

Ripoti ya Benki ya Dunia (2017) juu ya Usimamizi Mzuri wa Maji inaeleza kuwa kwa miaka 25 iliyopita idadi ya watu waliopo Tanzania imeongezeka mara dufu, kiwango cha uchumi kimeongezeka zaidi ya mara tatu lakini upatikanaji wa maji hauendani na ongezeko hilo. Matokeo yake vyanzo vya maji vimepungua kwa zaidi ya mita za ujazo 1,700 ikiwa na maana kuwa Tanzania imeungana na nchi nyingine duniani zenye mahitaji makubwa ya maji.

Ripoti hiyo inaeleza kuwa mahitaji ya maji duniani ni makubwa wakati wa kipindi cha ukame na maeneo ya nchi yanayokabiliwa na tatizo la ukame. Mvua nyingi zinanyesha mara moja kwa mwaka na baada ya kutathmini mtiririko wa mahitaji ya mazingira, Tanzania ina mahitaji ya maji yanayofikia asilimia 150 wakati wa kipindi ukame.

Upungufu huu unaathiri uzalishaji wa chakula na umeme na kusababisha uharibifu wa mazingira, hali inayoleta migogoro na ushindani wa kutumia maji miongoni mwa sekta mbalimbali za kijamii na zile za kiuchumi.

Zaidi, soma hapa => Mahitaji ya maji yaongezeka Tanzania, viwanda na ukuaji wa miji vinahatarisha uzalishaji | FikraPevu
 
Back
Top Bottom