Mahita akubali kumlea mtoto aliyezaa na mtumishi

MaxShimba

JF-Expert Member
Apr 11, 2008
35,782
4,040
Tuesday, 20 September 2011 20:30
Nora Damian
HATIMAYE Mkuu wa zamani wa Jeshi la Polisi (IGP), Omar Mahita amekubali kumhudumia mtoto aliyezaa na mtumishi wake wa ndani, Rehema Shabani. Hatua hiyo imefikiwa baada ya Mahita kulipa gharama za malimbikizo ya matunzo ya kumhudumia mtoto huyo kuanzia mwaka 2003 hadi siku ya hukumu. Jana, Mahita alilipa Sh9 milioni kati ya Sh12 milioni anazotakiwa kulipa na kuahidi kulipa nyingine katika kipindi cha siku 30.

Fedha hizo zililipwa na Wakili wake, Charles Semgalawe kwa kampuni ya udalali ya Nasm Auction Mart ambayo ilipewa jukumu na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni kufuatilia fedha hizo. Kampuni hiyo ilitoa notisi ya siku 14 kwa Mahita awe amelipa fedha hizo, vinginevyo hatua ya kutumia nguvu kukamata mali zake ingetumika. Notisi hiyo ilikuwa inamalizika jana na kwa kuwa sehemu ya fedha hizo ilitolewa na kuhidi kumaliza kiasi kilichobakia ndani ya siku 30, hatua ya kutumia nguvu iliondolewa.

Awali, Mahakama ya Kinondoni ilitoa hukumu ya kuidhinisha kuwa mtoto huyo ni wa Mahita hivyo kumtaka mstaafu huyo wa jeshi la polisi kutoa Sh100,000 kila mwezi kwa ajili ya kumhudumia pamoja na kulipa malimbikizo ya gharama za matunzo kuanzia mwaka 2003 hadi siku ya hukumu.

Katika kesi hiyo, Mahakama ya Kinondoni ilijiridhisha kuwa mtoto huyo ni wa Mahita kutokana na ushahidi wa upande wa mlalamikaji uliowasilishwa mahakamani hapo, ukiwapo wa vipimo vya vinasaba (DNA).

Hata hivyo, baada ya hukumu hiyo Mahita alikata rufaa ambayo ilitupiliwa mbali na Mahakama Kuu.Katika uamuzi wake, Jaji Dk Fauz Twaib alisema kuwa Mahakama ya Kinondoni ilikuwa sahihi na kumwamuru Mahita kulipa gharama za kesi hiyo.

Jaji Twaib alisema kwa mujibu wa barua kutoka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kwenda kwa Mahakama, mrufani hakuweza kufika kwa ajili ya uchunguzi huo mara sita kwa nyakati tofauti.

Jaji Twaib pia aliunga mkono hoja za wakili wa mlalamikaji kuwa ingawa sheria inatamka fidia ya Sh100 lakini mahakama inaweza kuangalia hali ya maisha na uwezo wa mlalamikiwa na hivyo kuweza kuongeza kiwango hicho. Alisisitiza kuwa katika shauri husika, kiwango kilichoamuriwa na mahakama ya chini kilizingatia hali ya kiuchumi hususan gharama za maisha na uwezo wa mrufani kuweza kulipa.
Mahita akubali kumlea mtoto aliyezaa na mtumishi
 
mikatabafeki

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
12,790
4,621
alikua wapi siku zote hizo,ina maana bado hakua willing kumlea huyo mwanae hadi maamuzi ya mahakama, sufisadi kila kona
 
Mzee

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
13,536
5,642
Viongozi wa ccm ubabe kila kona. Amejidhalilisha bila ya sababu ya msingi.
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
42,466
92,798
Na bado kama huyo mama anapata mwanasheria mzuri, anamfungulia kesi ya madai ya kumfanyisha kazi ya ziada ya kumgeuza 'confort' girl wakati aliajiriwa kwa ajili ya kazi za ndani tuu!. Mahakama itamlipisha fidia kama walivyolipwa wale 'comfort' girls wa Japan wakati wa vita kuu ya pili.
 
Kabakabana

JF-Expert Member
Aug 5, 2011
5,553
1,157
yani hawa sisiem kwa ngono siwawezi huyu nae mpaka mtoto ana miaka 8 ndo namkubali pompompo kweli huyu
 
MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,720
70,857
Na bado kama huyo mama anapata mwanasheria mzuri, anamfungulia kesi ya madai ya kumfanyisha kazi ya ziada ya kumgeuza 'confort' girl wakati aliajiriwa kwa ajili ya kazi za ndani tuu!. Mahakama itamlipisha fidia kama walivyolipwa wale 'comfort' girls wa Japan wakati wa vita kuu ya pili.
Mmmh mkuu, hebu rudia tena kwa wakati huu tuone kama kauli zitalingana
 
Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
42,466
92,798
Mmmh mkuu, hebu rudia tena kwa wakati huu tuone kama kauli zitalingana
Na bado kama huyo mama anapata mwanasheria mzuri, anamfungulia kesi ya madai ya kumfanyisha kazi ya ziada ya kumgeuza 'confort' girl wakati aliajiriwa kwa ajili ya kazi za ndani tuu!. Mahakama itamlipisha fidia kama walivyolipwa wale 'comfort' girls wa Japan wakati wa vita kuu ya pili.

Paskali
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom